Kwa nini Serikali inawakamata Makahaba Lakini Haiwakamati Mashoga?

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Ni jambo la ajabu na Hatari kwa Jamii ya Watanzania pale ambapo Serikali haijawahi kuwakamata Mashoga pamoja na kujitangaza kuwa ni Mashoga lakini kuna Nguvu kubwa ya Jeshi la polisi inaelekezwa kuwakamata Makahaba !!!!

Juzi hapa tulishuhudia gazeti la Nipashe likiandika habari kuwa polisi wenye silaha walimpiga kwa risasi sehemu za makalio binti ambaye alikuwa kwenye tendo la uzinzi na mwanaume maeneo ya Zakiem Mbagala DSM!!!

Pia Gazeti la Habari Leo limeripoti hadhari juu ya Mashoga ambao walijieleza wazi kuwa wanafanya vitendo hivyo na Mawaziri na wabunge na kutokana na uhasama wao wakawa wanaomba ulinzi wa polisi!!!

Sasa ni kwa nini serikali ya CCM haijakemea Ushoga wakati ni kosa la Jinae kama Madawa ya Kulevya???

Kwa nini mkuu wa nchi anatumia nguvu nyingi kukemea biashara ya Madawa ya kulevya lakini anaacha kukemea Ushoga ambao ni hatari kuliko biashara ya madawa ya kulevya???

kwa nini polisi wapo tayari kutuimia silaha na msako mkali wa makahaba lakini wana waacha Mashoga???

Je serikali inaruhusu Ushoga kivitendo na inapinga kinafiki????
 
Mashoga waja na mkakati wa kutambuliwa kikatiba.
mashoga.bmp

SERIKALI imeombwa kuangalia kwa upana suala la mchakato wa uandaaji wa katiba mpya kwa kuweka kifungu kitakachowasaidia mashoga kuondokana na adha na kero ya kunyanyapaliwa.

Ombi hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Bw. Abdul Zungu ambaye ni shoga na mwanaharakati katika tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Alisema kuwa kutokana na hali waliyonayo asilimia watu wengi katika jamii wamekuwa wakiwatenga na kuwanyanyapaa na kusababisha kuishi
kwa hofu na hata kutishiwa kuuawa kwa silaha.
Alisema pia wapo baadhi ya mashoga waliopoteza maisha kutokana na kuuawa na wanapofuatilia huwa kesi zao hazitiliwi maanani kutokana na kukosa utetezi.
"Tuna haja ya sisi kupata mwakilishi katika ngazi za maamuzi na ndio maana tunataka katiba yenye kututambua kama sehemu ya jamii inayopaswa kulindwa na kupata huduma za kibinadamu, " alisema Abdul.
Bw. Zungu alisema wanashangazwa na jamii kuwatenga na kuwanyima
kuwapa huduma muhimu kwa tuhuma kuwa vitendo wanavyofanya havimpendezi Mungu.
"Tunaiomba Serikali iangalie upya kwa kuweka kifungu ambacho
kitatulinda kwani kutokana na hali yetu tumekuwa tukikumbana na
kero mbalimbali ikiwemo ya kutengwa na jamii, " alisema.
Mshiriki huyo alisema kuwa licha ya umoja wao kuwa na sifa mbalimbali lakini wanapofanya maombi ya kazi katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakinyimwa bila ya sababu.
Alidai kuwa si kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kuwapatia maslahi bali kinachofanyika ni kukosa nafasi hizo na kujikuta hawana kazi ya kufanya na badala yake huendeleza
ushoga ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi.
"Kama Mungu angekua hatupendi basi hata leo sisi tusingeweza kuishi hapa duniani nanyi hivyo hakuna sababu ya kututenga kuishi nanyi. Haya ni matwakwa yake," alisema.
Kwa upande wa suala la afya alisema wamekuwa wakinyanyapaliwa hasa pale
wapohitaji huduma hizo na wakati mwingine huduma hizo huzipata
kwa ubabe kwa baadhi ya madaktari ama kutopata kabisa.
Alisema ni vyema Serikali ikawatambua mahali walipo ili nao waweze kuchangia katika mapambano ya kuunda katiba mpya ambayo itajibu mahitaji yao.
"Kama katiba haitatutambua hakuna mtu ambaye anaweza akasimama kidete kututetea na badala yake ushoga utaendelea kila kukicha huku makundi yasiyokuwa na maadili yakiibuka ndani ya jamii," alisema.
Alisema mbali ya kundi lao ambalo linaonekana kutengwa pia kuna makundi mengi ambayo Serikali imeshindwa kuyatambua na kusema katiba nzuri ni ile inayogusa makundi yote ndani ya nchi yao.
Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya alisema njia pekee ya kujibu matatizo ya wananchi ni kupatikana kwa katiba inayotokana na
matatizo ya wananchi wenyewe hivyo hakuna sababu ya kuanza kujadili idadi ya kurasa wakati matatizo hayajainishwa.
"Wakati mwingine utasikia viongozi wa Serikali wakikosoa jitihada za wanaharakati wakidai kuwa wanaleta mlolongo wa mambo mengi ni katiba gani tutakayoandika yenye kuingiza mambo yote hayo?, " alisema
Hata hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya mashoga katika tamasha hilo na kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria ambao hawajapata kuwaona ‘laivu' huku wengine baadhi ya wakiangua kilio na wengine kicheko.
 
IBRAHIMU MOHAMED ‘ANTI SUZY': AELEZA UOZO, HATARI ILIYOKO KATIKA ‘USHOGA'

clip_image002.jpg

UKIMWONA kwa macho, unaweza usiamini kuwa ni mwanamume, namna anavyoongea na anavyotembea, lakini mwenyewe anatambua kuwa anapaswa kuwa mwanamume lakini anakiri kwa sasa ni vigumu kurejea katika hali hiyo, kutokana na kuharibiwa vibaya maumbile yake.

Pamoja na hayo, vitendo vya kujiuza ili kupata fedha, kumsababishia aambukizwe virusi vya Ukimwi na sasa ameamua kujitangaza hadharani ili wanaume wasimfuate ingawa anadai bado wapo wanaomfuata.

Nilikutana naye kwenye Tamasha la 10 la Jinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), akiwa na wenzake zaidi ya 20, kwa namna watu walivyokuwa wakiwashangaa, hasa yeye, nilishawishika kumshawishi mkuu wangu wa kazi tumtafute tupate undani wa sababu ya kuwa shoga.

Baada ya kukubali kuhojiwa, alifika ofisi za gazeti hili na kuzungumza kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo namna wanaume wenye pesa wanavyowatumia mashoga kuwatafuta watoto wadogo wa kiume ili wawaingilie kinyume cha maumbile, jambo alilodai sasa limeshika kasi nchini.

Ungana na mwandishi wa makala haya ujue kisa hiki kinachoonesha na namna jamii ya Kitanzania hasa wazazi inavyopaswa kujua ili kujipanga kupambana na utamaduni huu wa Kimagharibi unaotaka kuangamiza kizazi cha kiume cha Kiafrika hivi sasa.

Mwandishi: Karibu ofisini kwetu, tunashukuru umekubali kuzungumza nasi ili jamii ifahamu madhara ya ushoga na kilichokufanya uingie huko, labda kwa kuanza utueleze historia fupi ya maisha yako hadi kuwa hivyo ulivyo.

Anti Suzy – Mimi naitwa Ibrahimu Mohamed, nimezaliwa Bugando, Mwanza, wazazi wangu hasa baba yangu ni mhamiaji kutoka nje ya nchi, mama yangu ni Mnyamwezi wa Urambo, Tabora. Historia yangu ni kwamba mimi mwenyewe ni mwanamume, lakini nimezaliwa na homoni za kike; nilijigundua niko hivyo tangu wakati wa utoto wangu.

Anti Suzy – Katika familia yetu, tumezaliwa watoto watano; wawili wa kike na watatu wa kiume, nikiwemo mimi, mimi ni kitinda mimba. Wazazi wangu na ndugu zangu, wote wako hai hadi leo.

Mwandishi – Pamoja na kueleza ulizaliwa na homoni nyingi za kike, wataalamu wa afya wanasema zipo dawa, wazazi wako hawakukupeleka hospitali? Na ilikuwaje ukaamua kuwa shoga wakati maadili yetu Watanzania hayaruhusu?

Anti Suzy – Hili swala la kujiingiza kwenye masuala ya kishoga, kwa kweli wazazi wangu hawakupendezewa; pili, hata dada na kaka zangu hawakupendezewa.

Baba yangu licha ya kwamba hakuwa na kipato kikubwa, alijaribu kunipeleka kwenye hospitali kuangalia hali yangu ilivyo….. …Kila alivyonipeleka kwa madaktari anaambiwa nimezidiwa na homoni za kike, wakamwambia si kwamba huyo mtoto ameharibika bali amezidiwa na homoni za kike, yaani homoni za kiume ni chache sana hivyo kinachotakiwa apelekwe nje ya nchi akafanyiwe operesheni apate nguvu za kiume. Ilishindikana kutokana na kipato cha baba kuwa kidogo…. ….Basi nikaendelea na masomo ya shule vizuri.

Namshukuru Mwenyezi Mungu, nimesoma hadi darasa la saba, lakini wakati nasoma nilikuwa nafanya mambo haya ya ushoga kisirisiri bila wazazi kujua.

Mwandishi – Labda turudi nyuma kidogo, ulizaliwa lini?
Aunt Suzy – Nimezaliwa Julai 5, 1986. Hadi sasa nina miaka ishirini na tano.

Mwandishi – Ok, ulianza kushiriki lini hayo mambo ya ushoga?
Aunt Suzy – Mimi mchezo huu kwa kweli, mh, nimeuanza toka niko shule ya msingi.

Mwandishi – Ulikuwa darasa la ngapi?
Anti Suzy – Nilikuwa darasa la tatu.

Mwandishi – Darasa la tatu?
Anti Suzy – Ndiyo darasa la tatu, nilikuwa bado mdogo na mchezo huu walinianzisha Waarabu ambao wametuzunguka pale Mwanza.

Mwandishi – Kwa hiyo, huyo Mwarabu ndiye aliyekufanya uwe hivyo? Mbona umesema umezaliwa na homoni za kike?
Anti Suzy – Sisi tuliishi Magomeni Kirumba mjini Mwanza na majirani zetu. Lakini kutokana na kipato cha wazazi kuwa kidogo na hakukuwa na shughuli za kufanya, nikajaribu kwenda kutafuta kama ajira wakati ninasoma, nikitoka shule naenda kwa huyo Mwarabu kufanya kazi za nyumbani.

Mwandishi – Wazazi wako walikuruhusu kufanya hizo kazi?
Anti Suzy – Ilibidi waniruhusu, nilipopata hiyo kazi niliwaambia wazazi hasa mama kwamba nimepata kazi kwa huyo Mwarabu (jina tunalihifadhi). Mama akaniuliza kazi gani mwanangu?

Waarabu wana tabia mbaya, nikamwambia mama hapana hawezi kunidhuru, akanikanya, akaniambia hata kama hela ni ndogo, atakuwa ananisaidia ili nisifanye hiyo kazi.

Mwandishi – Ikawaje?
Anti Suzy – Niling'ang'ana nikaifanya kwa siri kutokana na yule Mwarabu alikuwa ananipa hela, akawa ananipa hela nyingi tu.

Akaninunulia simu kwa mara ya kwanza nikamwambia kutokana na mimi kuwa bado mdogo, nikienda na simu nyumbani, wazazi watashtuka, nikawa naficha hizo fedha alizokuwa akinipa naenda nazo shule… ….Kwa hiyo kama nikihitaji sare za shule, nitawaambia wazazi, hela kidogo wanayonipa ninachanganya na ile niliyopewa na Mwarabu na kununua sare nzuri za shule, wazazi walijua ni fedha zao nanunulia, kumbe hela nyingi nilikuwa napewa na yule Mwarabu… ….Nilikuwa naondoka nyumbani siku za mapumziko ya mwisho wa wiki naenda kwa Mwarabu kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na Jumatatu naendelea na shule kama kawaida, lakini yule Mwarabu naendelea naye na mchezo huo kisirisiri.

Mwandishi – Alikuwa hana mke?
Anti Suzy – Alikuwa na familia…Mke wake alikuwa mfanyabiashara hivyo hakuwa anakaa pale nyumbani, hivyo mimi nilikuwa kama mfanyakazi.

Yule Mwarabu akaniambia mchezo kati yangu na yeye iwe siri, nisimwambia mtu yeyote na akaniahidi kunipa hela yoyote ntakayokuwa nahitaji…. ..Baba hakuwa na muda na mimi kwa kuwa alikuwa mfanyabiashara ndogo hakai nyumbani na kipato chake kilikuwa si kikubwa.

Alishanichukia hakutaka kuniona na mama yangu ni mama wa nyumbani, nikiangalia hali ya nyumbani na ahadi za Mwarabu, basi ikawa siri yangu.
SHOGA 'ANTI SUZY' AFICHUA SIRI NZITO

SHOGA maarufu jijini Dar es Salaam, Ibrahim Mohamed ‘Anti Suzy' (25) ameibuka na kutoa siri nzito kuhusu mambo yanayofanywa na mashoga kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo
nchini kuwaharibu watoto wadogo wa kiume.

Ametoa tahadhari huku akidai kuwa kama Serikali kwa kushirikiana na watu wengine
haitachukua hatua, kizazi cha kiume cha Watanzania siku zijazo kitapotea katika dunia hii kutokana na ukweli kwamba wimbi la uwepo wa mashoga linazidi kuongezeka kwa kasi.

Anti Suzy ambaye ni mkazi wa Jangwani, pia amejitangaza kuwa ni muathirika anayeishi na Virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 10 sasa na akasema mashoga wengi wameshaambukizwa virusi vya Ukimwi kama yeye na wanaishi kwa
matumaini, hivyo kwa kuwa nao ni binadamu, wasingependa kuona watoto
wadogo wa kiume wakiharibiwa kama walivyofanyiwa wao.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za gazeti hili zilizopo Mtaa wa Samora, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Anti Suzy alisema hivi sasa wanaume wenye fedha akiwataja kwa jina maarufu la ‘mapedejee' wanatumia fedha zao
kuharibu watoto wadogo huku wengi wao wakijijua kuwa ni waathirika wa Ukimwi.

"Najua kuwa na Ukimwi si mwisho wa maisha lakini si vizuri mtu ukijijua kuwa umeathirika,
ukamwambukiza mwenzako kwa makusudi, kwa kweli sasa hivi hali ni mbaya, wanaume wenye pesa ‘mapedejee' wanapenda sana watoto wadogo wa kiume," alisema na kuongeza:

"Wazazi wawe macho sana, sasa hivi mashoga wa rika langu ukienda ukumbi wa starehe au baa, wakijua wewe ni shoga, anakutafuta mtu anakuomba simu ili umtafutie mtoto
mdogo kwa gharama yoyote.

"Mashoga watu wazima hivi sasa hawana soko, wanasakwa watoto wadogo walioko mitaani na hata shuleni,kama Mwalimu hana utu anaweza hata kuuza mtoto wako kwa sababu ya fedha, mtu yuko radhi kukupa pesa yoyote umtafutie mtoto mdogo wa kiume.

"Wanawapenda pia watoto wa kiume wanaochipukia kwenye ushoga ambao siku hizi ndiyo wapo kibao (wengi), watoto wanaharibika sana, wanaowatafuta wanapewa mpaka laki mbili hata zaidi kwa mtoto mmoja".

Huku akiwataja kwa majina (yanahifadhiwa), Anti Suzy alisema mapedejee hao wana fedha nyingi hivyo wana ushawishi mkubwa, lakini alitoa angalizo kuwa si watu wote wanaoitwa pedejee wana mchezo huo, ingawa alikiri kuwa wengi wao hujitangaza kwa jina hilo wanapotaka kutafutiwa watoto au mashoga wapya kutoka nje ya mkoa kwa wanaoishi Dar es Salaam.

Akizungumzia ongezeko hilo sambamba na maambukizi ya Ukimwi, Anti Suzy aliyezaliwa
Bugando mkoa Mwanza mwaka 1986 akiwa kitinda mimba kwenye familia yao ya watoto watano, alisema hivi sasa mashoga wengi wameambukizwa ugonjwa huo na wengi wao wanafanya biashara ya kujiuza hivyo wanaendelea kuambukiza watu wengine.

Alisema mwanaume akimkuta shoga baa au katika ukumbi wa starehe kwenye Casino, na pembeni ikiwa kuna mwanamke anayejiuza, humchukua shoga jambo linalofanya
kuendelea kuathirika na kuharibiwa vibaya viungo vyao vya siri.

Alidai yeye alizaliwa akiwa na homoni nyingi za kike na wazazi wake walihangaika hospitali bila mafanikio na alipofika darasa la tatu alianza mchezo huo na mfanyabiashara wa kiarabu (jina tunalo) aliyekuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwake akitoka shule ili apate
fedha za mahitaji ya shule, ikiwemo sare.

Anti Suzy alidai mfanyabiashara
huyo alimtorosha kutoka nyumbani
kwao Mwanza na kumpeleka Zanzibar
ambako alikaa naye nyumba ya
wageni (jina tunalo) kwa zaidi ya
mwezi mmoja usiku na mchana
akimwingilia jambo alilokuja kubaini
baadaye kuwa ameharibu maumbile
yake ya kiume. Alisema pamoja na
kuwa na wanaume wengine, alihisi
ndiye aliyemuambukiza Ukimwi.
"Siwezi kusema ni nani kaniambukiza
Ukimwi lakini nahisi ni
yule mwarabu, maana mashoga wengi
nawafahamu wenye Ukimwi
amewachezea sana yeye na pia ameharibu
watoto wengi sana, sijui hivi
sasa yuko wapi lakini kweli ameharibu
watoto sana na kama yupo hai
basi huenda anaendelea kuwaharibu,"
alibainisha Anti Suzy.
Siri nyingine aliyoitoboa Anti
Suzy alidai, akiwa Dar es Salaam alifanya
biashara ya kujiuza na kutembea
na waume za watu wakiwemo
vigogo nchini wanaopenda kutembea
na mashoga kuliko wanawake na
alikuwa na uwezo wa kutembea na
wanaume watano hadi sita kwa siku
wakati mwingine bila kinga, kutegemea
na uwezo na matakwa ya
wanaume hao na mara nyingine aliwalisha
dawa za kulevya na kuwaibia.
"Kweli nilikuwa naiba sana, kuna
jamaa nilimlisha dawa, nikaiba na
kugeuza mkono wa simu ya chumbani,
simu zikapigwa hazipatikani,
wakaja kabla sijatoka, wakamkuta jamaa
amelala anakoroma mimi
nimeshika baadhi ya vitu na pesa, jamani
nilipigwaaa! nilipigwaaa! Lakini
sikujali maana aibu ilikuwa kwake,
ameshachukua malaya (shoga) watu
walimjalia mpaka waandishi wa
habari walimpiga picha," alisema.
Aliwataka wanawake wafuatilie
mienendo ya waume zao kwa kuwa
japo baadhi yao wamejitangaza kuwa
na Ukimwi, lakini wanaume
wamekuwa wakiwataka na wengine
wanawakimbia wake zao na
kuwalazimisha mashoga wawalelee
watoto wao kama alivyoletewa yeye
mtoto wa mwaka mmoja na nusu na
mwanaume aliyekuwa akiishi naye
kama mume wake ingawa sheria za
nchi haziruhusu.
 
IBRAHIMU MOHAMED ANTI SUZY: AELEZA UOZO, HATARI ILIYOKO KATIKA USHOGA

clip_image002.jpg

UKIMWONA kwa macho, unaweza usiamini kuwa ni mwanamume, namna anavyoongea na anavyotembea, lakini mwenyewe anatambua kuwa anapaswa kuwa mwanamume lakini anakiri kwa sasa ni vigumu kurejea katika hali hiyo, kutokana na kuharibiwa vibaya maumbile yake.

Pamoja na hayo, vitendo vya kujiuza ili kupata fedha, kumsababishia aambukizwe virusi vya Ukimwi na sasa ameamua kujitangaza hadharani ili wanaume wasimfuate ingawa anadai bado wapo wanaomfuata.

Nilikutana naye kwenye Tamasha la 10 la Jinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), akiwa na wenzake zaidi ya 20, kwa namna watu walivyokuwa wakiwashangaa, hasa yeye, nilishawishika kumshawishi mkuu wangu wa kazi tumtafute tupate undani wa sababu ya kuwa shoga.

Baada ya kukubali kuhojiwa, alifika ofisi za gazeti hili na kuzungumza kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo namna wanaume wenye pesa wanavyowatumia mashoga kuwatafuta watoto wadogo wa kiume ili wawaingilie kinyume cha maumbile, jambo alilodai sasa limeshika kasi nchini.

Ungana na mwandishi wa makala haya ujue kisa hiki kinachoonesha na namna jamii ya Kitanzania hasa wazazi inavyopaswa kujua ili kujipanga kupambana na utamaduni huu wa Kimagharibi unaotaka kuangamiza kizazi cha kiume cha Kiafrika hivi sasa.

Mwandishi: Karibu ofisini kwetu, tunashukuru umekubali kuzungumza nasi ili jamii ifahamu madhara ya ushoga na kilichokufanya uingie huko, labda kwa kuanza utueleze historia fupi ya maisha yako hadi kuwa hivyo ulivyo.

Anti Suzy  Mimi naitwa Ibrahimu Mohamed, nimezaliwa Bugando, Mwanza, wazazi wangu hasa baba yangu ni mhamiaji kutoka nje ya nchi, mama yangu ni Mnyamwezi wa Urambo, Tabora. Historia yangu ni kwamba mimi mwenyewe ni mwanamume, lakini nimezaliwa na homoni za kike; nilijigundua niko hivyo tangu wakati wa utoto wangu.

Anti Suzy  Katika familia yetu, tumezaliwa watoto watano; wawili wa kike na watatu wa kiume, nikiwemo mimi, mimi ni kitinda mimba. Wazazi wangu na ndugu zangu, wote wako hai hadi leo.

Mwandishi  Pamoja na kueleza ulizaliwa na homoni nyingi za kike, wataalamu wa afya wanasema zipo dawa, wazazi wako hawakukupeleka hospitali? Na ilikuwaje ukaamua kuwa shoga wakati maadili yetu Watanzania hayaruhusu?

Anti Suzy  Hili swala la kujiingiza kwenye masuala ya kishoga, kwa kweli wazazi wangu hawakupendezewa; pili, hata dada na kaka zangu hawakupendezewa.

Baba yangu licha ya kwamba hakuwa na kipato kikubwa, alijaribu kunipeleka kwenye hospitali kuangalia hali yangu ilivyo.. Kila alivyonipeleka kwa madaktari anaambiwa nimezidiwa na homoni za kike, wakamwambia si kwamba huyo mtoto ameharibika bali amezidiwa na homoni za kike, yaani homoni za kiume ni chache sana hivyo kinachotakiwa apelekwe nje ya nchi akafanyiwe operesheni apate nguvu za kiume. Ilishindikana kutokana na kipato cha baba kuwa kidogo. .Basi nikaendelea na masomo ya shule vizuri.

Namshukuru Mwenyezi Mungu, nimesoma hadi darasa la saba, lakini wakati nasoma nilikuwa nafanya mambo haya ya ushoga kisirisiri bila wazazi kujua.

Mwandishi  Labda turudi nyuma kidogo, ulizaliwa lini?
Aunt Suzy  Nimezaliwa Julai 5, 1986. Hadi sasa nina miaka ishirini na tano.

Mwandishi  Ok, ulianza kushiriki lini hayo mambo ya ushoga?
Aunt Suzy  Mimi mchezo huu kwa kweli, mh, nimeuanza toka niko shule ya msingi.

Mwandishi  Ulikuwa darasa la ngapi?
Anti Suzy  Nilikuwa darasa la tatu.

Mwandishi  Darasa la tatu?
Anti Suzy  Ndiyo darasa la tatu, nilikuwa bado mdogo na mchezo huu walinianzisha Waarabu ambao wametuzunguka pale Mwanza.

Mwandishi  Kwa hiyo, huyo Mwarabu ndiye aliyekufanya uwe hivyo? Mbona umesema umezaliwa na homoni za kike?
Anti Suzy  Sisi tuliishi Magomeni Kirumba mjini Mwanza na majirani zetu. Lakini kutokana na kipato cha wazazi kuwa kidogo na hakukuwa na shughuli za kufanya, nikajaribu kwenda kutafuta kama ajira wakati ninasoma, nikitoka shule naenda kwa huyo Mwarabu kufanya kazi za nyumbani.

Mwandishi  Wazazi wako walikuruhusu kufanya hizo kazi?
Anti Suzy  Ilibidi waniruhusu, nilipopata hiyo kazi niliwaambia wazazi hasa mama kwamba nimepata kazi kwa huyo Mwarabu (jina tunalihifadhi). Mama akaniuliza kazi gani mwanangu?

Waarabu wana tabia mbaya, nikamwambia mama hapana hawezi kunidhuru, akanikanya, akaniambia hata kama hela ni ndogo, atakuwa ananisaidia ili nisifanye hiyo kazi.

Mwandishi  Ikawaje?
Anti Suzy  Nilingangana nikaifanya kwa siri kutokana na yule Mwarabu alikuwa ananipa hela, akawa ananipa hela nyingi tu.

Akaninunulia simu kwa mara ya kwanza nikamwambia kutokana na mimi kuwa bado mdogo, nikienda na simu nyumbani, wazazi watashtuka, nikawa naficha hizo fedha alizokuwa akinipa naenda nazo shule .Kwa hiyo kama nikihitaji sare za shule, nitawaambia wazazi, hela kidogo wanayonipa ninachanganya na ile niliyopewa na Mwarabu na kununua sare nzuri za shule, wazazi walijua ni fedha zao nanunulia, kumbe hela nyingi nilikuwa napewa na yule Mwarabu .Nilikuwa naondoka nyumbani siku za mapumziko ya mwisho wa wiki naenda kwa Mwarabu kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na Jumatatu naendelea na shule kama kawaida, lakini yule Mwarabu naendelea naye na mchezo huo kisirisiri.

Mwandishi  Alikuwa hana mke?
Anti Suzy  Alikuwa na familiaMke wake alikuwa mfanyabiashara hivyo hakuwa anakaa pale nyumbani, hivyo mimi nilikuwa kama mfanyakazi.

Yule Mwarabu akaniambia mchezo kati yangu na yeye iwe siri, nisimwambia mtu yeyote na akaniahidi kunipa hela yoyote ntakayokuwa nahitaji. ..Baba hakuwa na muda na mimi kwa kuwa alikuwa mfanyabiashara ndogo hakai nyumbani na kipato chake kilikuwa si kikubwa.

Alishanichukia hakutaka kuniona na mama yangu ni mama wa nyumbani, nikiangalia hali ya nyumbani na ahadi za Mwarabu, basi ikawa siri yangu.
SHOGA 'ANTI SUZY' AFICHUA SIRI NZITO

SHOGA maarufu jijini Dar es Salaam, Ibrahim Mohamed Anti Suzy (25) ameibuka na kutoa siri nzito kuhusu mambo yanayofanywa na mashoga kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo
nchini kuwaharibu watoto wadogo wa kiume.

Ametoa tahadhari huku akidai kuwa kama Serikali kwa kushirikiana na watu wengine
haitachukua hatua, kizazi cha kiume cha Watanzania siku zijazo kitapotea katika dunia hii kutokana na ukweli kwamba wimbi la uwepo wa mashoga linazidi kuongezeka kwa kasi.

Anti Suzy ambaye ni mkazi wa Jangwani, pia amejitangaza kuwa ni muathirika anayeishi na Virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 10 sasa na akasema mashoga wengi wameshaambukizwa virusi vya Ukimwi kama yeye na wanaishi kwa
matumaini, hivyo kwa kuwa nao ni binadamu, wasingependa kuona watoto
wadogo wa kiume wakiharibiwa kama walivyofanyiwa wao.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za gazeti hili zilizopo Mtaa wa Samora, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Anti Suzy alisema hivi sasa wanaume wenye fedha akiwataja kwa jina maarufu la mapedejee wanatumia fedha zao
kuharibu watoto wadogo huku wengi wao wakijijua kuwa ni waathirika wa Ukimwi.

Najua kuwa na Ukimwi si mwisho wa maisha lakini si vizuri mtu ukijijua kuwa umeathirika,
ukamwambukiza mwenzako kwa makusudi, kwa kweli sasa hivi hali ni mbaya, wanaume wenye pesa mapedejee wanapenda sana watoto wadogo wa kiume, alisema na kuongeza:

Wazazi wawe macho sana, sasa hivi mashoga wa rika langu ukienda ukumbi wa starehe au baa, wakijua wewe ni shoga, anakutafuta mtu anakuomba simu ili umtafutie mtoto
mdogo kwa gharama yoyote.

Mashoga watu wazima hivi sasa hawana soko, wanasakwa watoto wadogo walioko mitaani na hata shuleni,kama Mwalimu hana utu anaweza hata kuuza mtoto wako kwa sababu ya fedha, mtu yuko radhi kukupa pesa yoyote umtafutie mtoto mdogo wa kiume.

Wanawapenda pia watoto wa kiume wanaochipukia kwenye ushoga ambao siku hizi ndiyo wapo kibao (wengi), watoto wanaharibika sana, wanaowatafuta wanapewa mpaka laki mbili hata zaidi kwa mtoto mmoja.

Huku akiwataja kwa majina (yanahifadhiwa), Anti Suzy alisema mapedejee hao wana fedha nyingi hivyo wana ushawishi mkubwa, lakini alitoa angalizo kuwa si watu wote wanaoitwa pedejee wana mchezo huo, ingawa alikiri kuwa wengi wao hujitangaza kwa jina hilo wanapotaka kutafutiwa watoto au mashoga wapya kutoka nje ya mkoa kwa wanaoishi Dar es Salaam.

Akizungumzia ongezeko hilo sambamba na maambukizi ya Ukimwi, Anti Suzy aliyezaliwa
Bugando mkoa Mwanza mwaka 1986 akiwa kitinda mimba kwenye familia yao ya watoto watano, alisema hivi sasa mashoga wengi wameambukizwa ugonjwa huo na wengi wao wanafanya biashara ya kujiuza hivyo wanaendelea kuambukiza watu wengine.

Alisema mwanaume akimkuta shoga baa au katika ukumbi wa starehe kwenye Casino, na pembeni ikiwa kuna mwanamke anayejiuza, humchukua shoga jambo linalofanya
kuendelea kuathirika na kuharibiwa vibaya viungo vyao vya siri.

Alidai yeye alizaliwa akiwa na homoni nyingi za kike na wazazi wake walihangaika hospitali bila mafanikio na alipofika darasa la tatu alianza mchezo huo na mfanyabiashara wa kiarabu (jina tunalo) aliyekuwa akifanya kazi za ndani nyumbani kwake akitoka shule ili apate
fedha za mahitaji ya shule, ikiwemo sare.

Anti Suzy alidai mfanyabiashara
huyo alimtorosha kutoka nyumbani
kwao Mwanza na kumpeleka Zanzibar
ambako alikaa naye nyumba ya
wageni (jina tunalo) kwa zaidi ya
mwezi mmoja usiku na mchana
akimwingilia jambo alilokuja kubaini
baadaye kuwa ameharibu maumbile
yake ya kiume. Alisema pamoja na
kuwa na wanaume wengine, alihisi
ndiye aliyemuambukiza Ukimwi.
Siwezi kusema ni nani kaniambukiza
Ukimwi lakini nahisi ni
yule mwarabu, maana mashoga wengi
nawafahamu wenye Ukimwi
amewachezea sana yeye na pia ameharibu
watoto wengi sana, sijui hivi
sasa yuko wapi lakini kweli ameharibu
watoto sana na kama yupo hai
basi huenda anaendelea kuwaharibu,
alibainisha Anti Suzy.
Siri nyingine aliyoitoboa Anti
Suzy alidai, akiwa Dar es Salaam alifanya
biashara ya kujiuza na kutembea
na waume za watu wakiwemo
vigogo nchini wanaopenda kutembea
na mashoga kuliko wanawake na
alikuwa na uwezo wa kutembea na
wanaume watano hadi sita kwa siku
wakati mwingine bila kinga, kutegemea
na uwezo na matakwa ya
wanaume hao na mara nyingine aliwalisha
dawa za kulevya na kuwaibia.
Kweli nilikuwa naiba sana, kuna
jamaa nilimlisha dawa, nikaiba na
kugeuza mkono wa simu ya chumbani,
simu zikapigwa hazipatikani,
wakaja kabla sijatoka, wakamkuta jamaa
amelala anakoroma mimi
nimeshika baadhi ya vitu na pesa, jamani
nilipigwaaa! nilipigwaaa! Lakini
sikujali maana aibu ilikuwa kwake,
ameshachukua malaya (shoga) watu
walimjalia mpaka waandishi wa
habari walimpiga picha, alisema.
Aliwataka wanawake wafuatilie
mienendo ya waume zao kwa kuwa
japo baadhi yao wamejitangaza kuwa
na Ukimwi, lakini wanaume
wamekuwa wakiwataka na wengine
wanawakimbia wake zao na
kuwalazimisha mashoga wawalelee
watoto wao kama alivyoletewa yeye
mtoto wa mwaka mmoja na nusu na
mwanaume aliyekuwa akiishi naye
kama mume wake ingawa sheria za
nchi haziruhusu.
Hili la Ushoga linashangaza sana hapa nchini
 
ushoga unaruhusiwa tz..nyie msimsikilize joka la mdimu alikuwa anawatania tu
 
hata mashoga wanakamatwa sana fikeni mahakama ya jiji mtapata records
 
MMejifungia huko hata hamjui kwamba nao wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Obsession yenu ya kukosoa serikali inawafikisha mahali ambapo hata takwimu hamtafuti, kazi kupiga makelele yenu kwenye nyuzi.
 
Kama Wanakamatwa Kwa nini hao waliojitokeza pale TNGP kuchangia hoja hawakukamatwa???
Naomba utusaidie takwimu au hao wanaachwa kwa sababu walisema wateja wao ni mawaziri???
 
lol mungu aniepushie mbali kijana wangu anaekuwa tumboni
asiwe chakla lol inauma sana
af na dav camroon ndie anaechochea watu waendelee kufanya ushoga
 
HIVI HAMKUFUNDISHWA UFUPISHO???
mnaboa na maelezo elfu huku poit ni moja tuu.......
kaz kukopi kop tuuuuuuu.
 
Back
Top Bottom