Kwa nini Richmond? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Richmond?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngozimbili, Apr 22, 2012.

 1. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 823
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 60
  Kwa muda mrefu watanzania wamekuwa wakipiga kelele kuhusu mkataba unaoitwa wa kinyonyaji wa Richmond.lakini jambo la kushangaza ni kuwa Tanesco imeingia mikataba ya kinyonyaji mingi tu na mingine ni ya kinyonyaji mara 4 ya Richmond.mfano i.p.t.l.,songas,na aggreko.mi nilidhani kama tunapiga vita ufisadi tuupige wote.lakini kila m tz utasikia richmond mpaka watu wakataka kuandamana.lakini baada ya richmond kuchukuliwa na marekani wote KIMYA! Kana kwamba hakukuwa na richmond lakini mtu mmoja hatakiwi kuombwa radhi hata kama maamuzi yake ya kuleta richmond mpaka leo tunakubaliana nayo kwa kutumia umeme wake.HIVI KUNA MCHEZO GANI UNACHEZWA?
   
 2. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  tatizo tunaenenda utafikiri vichwa vimekatika tukipewa kipapatio tunasahau kujiuliza mapaja ya kuku yameend wapi na ndio shida tuliyonayo watanzania,wameongeza bei za umeme lakini mgao uko palepale na ni mwezi wa nne tu ikifika kiangazi itakuwaje.TZ KEEP TALKING!!
   
 3. b

  bakenyile Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani ww hujui kuwa tume iliyoundwa na Bunge ilikuwa ya kuchunguza mkataba wa Richmond? Ndugu maswali mengine uliza baada ya utafiti. Tunazungumzia Richmond kwasababu ndiyo iliyoundiwa tume na ndiyo iliyoanzisha kwa mara ya kwanza Wabunge kuwa wa kweli na wawazi. Lakini labda nikuulize swali mtoa hoja hivi ww katika hili ulifanya nini kuwaunga mkono wabunge waliosema ukweli kuhusu hilo? au nawe ni kati ya wale wanaonung'unika tu na kulaumu kwa hawajui mwisho? Asasi gani ya kirai a iliitisha maandamano? Ila Lowassa amewateka kweli.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,731
  Trophy Points: 280
  ....Mkuu hili bado lina utata mkubwa sana hasa katika bulungutu la shilingi bilioni 95 ambayo Dowans inastahili kulipwa na TANESCO. Pesa hii ilitakiwa kulipwa tangu December, 2010 na ilishafagiliwa kwamba ilipwe na akina Msanii Kikwete, Pinda, Ngeleja, Mwanaheria Mkuu wa Serikali na inasemekana hata magamba walifanya kikao na kuridhia kwamba Dowans/Richmond wanastahili kulipwa bulungutu lao la shilingi 95 billioni plus accumulated interest.

  Watanzania tukaja juu na kupinga kwa kila hali kulipwa malipo hayo ya kifisadi kwa kuwa hakukuwepo na mantiki yoyote ile ya kulipwa hasa ukitilia maanani kwamba Dowans ni kampuni ya kitapeli ambayo haikuwa na HQ Texas kama ilivyodaiwa na fisadi Rostam ilishindwa kutumiza masharti ya mkataba wake wa kufua umeme wakati nchi ilipokuwa gizani. Kesi bado iko mahakamani na natumai kwamba shinikizo la Wabongo ndani na nje ya nchi litahakikisha mafisadi wa Dowans/Richmond hawalipwi hata senti moja ya mradi wa kifisadi ambao ulibarikiwa na msanii Kikwete na rafiki yake EL. Kwa maoni yangu ni ushindi wa aina yake kwa Watanzania kuweza kusimamisha malipo ambayo yalitakiwa yafanyike zaidi ya mwaka mmoja uliopita (December 2010).
   
Loading...