Kwanini Prof. Baregu amenyimwa kazi UDSM?

Swali Kuhusu ya SAUT na Mlimani: Hivi mtu anakuwa mzuri kichwani kutokana na chuo alichosoma au ni juhudi binafsi na ufuatiliaji wa masomo. Ninachojua mimi kuna watu walipata 3 waka-graduate Mlimani na SUA etc, na kuna mwingine alipata 4 karibia na zero, juzi amepata BBA yake ya mlimani. Na kuna watu walikuwa na credits kali wakaenda kusoma vyuo vingine kwa vile walikuwa wanatafuta fani ambazo Mlimani hawafundishi. Sasa je ni mtu au ni chuo? Tusaidiane!
 
Kama kawaida yake serikali ya CCM huwa haithamini wataalamu na badala yake wanafikiria nchi itaendelela kwa siasa na maneno mengi ya uwongo. Profesa Mwesiga Baregu ambaya amekuwa mhadhiri mwandamizi pale UDSM kwa muda mrefu na alipostaafu amekuwa akifanya kazi pale kwa mkataba.Inavyo onekana kwa sababu yeye ni mwanachama wa CHADEMA basi CCM kwa kushirikiana na serikali na uongozi wa UDSM wameamua kutompatia mkataba mpya na hii ni kwa sababu ya msimamo wake mkali dhidi ya uzembe unaofanywa na serikali iliyopo madarakani.

Napenda niseme tu kwamba bila kuthamini wataalamu na kukubali kukosolwa maendeleo hakuna. Hili liko wazi kwa sababu miaka zaidi ya 40 CCM imeendekeza siasa na uwongo ktk kuendesha nchi ndiyo maana wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa na wajinga (hawana elimu).

Sote tunajua kuwa UDSM inakabiliwa na uhaba wa wahadhiri wandamizi, leo mnamyima mkataba profesa Baregu ambaye ni tegemeo kubwa ktk fani ya sayansi ya jamii nani ataziba pengo lake? hapo ndo tutamkumbuka prof. Luhanga ambaye alikuwa hatumii siasa kuendesha UDSM.

Prof. Baregu karibu jiunge hapa SAUT na uendelee kuwapiga bakora tu hao CCM wamefulia.

Ndiyo maana Rwanda wametuacha kwa sababu Kagame anawatumia sana wataalamu waliotoka hapa Tanzania lakini CCM inaona taabu ikikosolewa na wasomi wake.
Hili jambo la kumnyima mkataba Prof Baregu huwa linanipa KICHEFUCHEFU.

Sasa kama mkuu wa UDSM anateuliwa na head of state JE atakuwa na maamuzi ya kitaalamu kweli au ndio atakuwa a rubber stamp. Prof Baregu karibu sana SAUT maana naona nabii hakubaliki kwao.

Nilitegemea wanafunzi wa UDSM basi hata wangeandamana kushinikiza uongozi umpe mkataba lakini wamelala usingizi wa pono, wanafunzi wa vyuo vikuu wa leo kwa kweli wanatia mashaka.
 
Swali Kuhusu ya SAUT na Mlimani: Hivi mtu anakuwa mzuri kichwani kutokana na chuo alichosoma au ni juhudi binafsi na ufuatiliaji wa masomo. Ninachojua mimi kuna watu walipata 3 waka-graduate Mlimani na SUA etc, na kuna mwingine alipata 4 karibia na zero, juzi amepata BBA yake ya mlimani. Na kuna watu walikuwa na credits kali wakaenda kusoma vyuo vingine kwa vile walikuwa wanatafuta fani ambazo Mlimani hawafundishi. Sasa je ni mtu au ni chuo? Tusaidiane!
Mkuu chuo kinasaidia sana, thugh we cant rule out effort za mtu binafsi...mfano wa chuo ni katika uwezo wake wa kusimamia mwanafunzi katika taaluma. Hii unaweza hata kuona katika dissertation, mfano dissertation za law nyingi za Tumani, ukiziangalia wanafunzi wanakopiana dissertation hizohizo....wakati pale Mlimani faculty of law its not the case.
 
inasikitisha sana kuona viongozi wetu hawajakomaa kisiasa, itafika wakati watakuwa wanajutia wanayo fanya.
 
Soma na wewe uwe prof uchukue nafasi ya Mwessiga acha kung'ang'ania apewe contract hata kama kashachoka. Akiona dili haziendi agagombee ubunge
 
chuo udsm ni cha ccm....basi ndio maana viongozi wengi ni mafisadi waliosoma udsm....hakuna elimu bora wala wahadhiri bora pale udsm....bora prof b...uende chuo chochote cha binafsi viko vingi wewe tu...
wasome wengi wazuri tz ni waoga na hawapendi nchi yao.....tumeona wazi...kesho nitawataja wote kwa majina.....

Ndugu yangu acha kujidanganya....ukiongelea chuo hapa nchini ni UDSM.Sikatai kwamba kuna vyuo binafsi vinakuja lakini kwa kweli huwezi kufananisha vyuo binafsi na taasisi za serikali ambazo zimekuwa hapo kwa miaka mingi na zina wataalamu wengi ambao hivi navyosema vyuo vyote binafsi wanaendelea kuwatumia.Kama SAUT,TUAMINI wako safi sana basi wasomeshe wahadhiri wao na waache kutegemea wahadhiri wa-UDSM.

Hoja iliyo mbele yetu ni suala la Baregu kukosa mkataba tena....ni afadhali aliyesema si lazima mtu kuongezewa mkataba kuliko wewe unayebwabwaja.Ufisadi hauna uhusiano wowote na mtu aliposoma.Kuna watu wamesoma kwenye vyuo bora duaniani lakini bado ni mafisadi sembuse hawa mafisadi waliosoma UDSM....acha habari zako mbofu mbofu!
 
Mkuu chuo kinasaidia sana, thugh we cant rule out effort za mtu binafsi...mfano wa chuo ni katika uwezo wake wa kusimamia mwanafunzi katika taaluma. Hii unaweza hata kuona katika dissertation, mfano dissertation za law nyingi za Tumani, ukiziangalia wanafunzi wanakopiana dissertation hizohizo....wakati pale Mlimani faculty of law its not the case.


Semenya.....yaani nimekupa THANKS maana umenigusa sana!Ulicholonga hapo juu ni sahihi kwa asilimia kubwa sana...ushahidi pia hupo!
 
Mkuu chuo kinasaidia sana, thugh we cant rule out effort za mtu binafsi...mfano wa chuo ni katika uwezo wake wa kusimamia mwanafunzi katika taaluma. Hii unaweza hata kuona katika dissertation, mfano dissertation za law nyingi za Tumani, ukiziangalia wanafunzi wanakopiana dissertation hizohizo....wakati pale Mlimani faculty of law its not the case.


Nakubaliana na wewe ila si mia kwa mia. Utambue kuna vipanga vile vile wamesoma DIT, Mzumbe, Nyegezi na IFM pamoja na kwamba vyuo hivyo admission requirements zilikuwa si tight sana. Si kila mtu aliingia vyuo hivyo kwa credits za chini, ila aliingia kwa vile vyuo hivyo vilikuwa vinatoa fani anayoitafuta. Kuna suala la application pia kupotea pale mlimani, au kuchelewa kuomba, wengine wa mikoani hasa nyakati za nyuma , sasa mtu hawezi akakaa anasubiri wakati miaka inaenda. Kuna watu waliingia na one nzuri za combination ngumu katika vyuo hivyo nilivyotolea mfano, na kuna watu waliingia na 2 au 3 za combination rahisi pale mlimani na waka-graduate. Sasa haya mambo ni ya kuangalia kwa marefu zaidi, hatuwezi kuwa generic tu. Kuna watu wanasomea kupata maisha na kuna watu wanatafuta sifa ili wakatangaze kijijini kuwa walifika chuo kikuu na watu wamekwenda na maji kwa mtindo huo. Mtu anakwenda mlimani kusomea kitu ambacho hakilipi mtaani, matokeo yake anakaa hana kazi miaka 3 na anakuwa frustrated na kuanza kunywa gongo halafu chali! Sasa haya mambo ni ya kuangalia, cha muhimu ni kuona mbele! At the end bao la maisha ndio lina-matter! Moreover, kipanga wa one (combination ngumu) ya enzi za Mwalimu ni kipanga tu, hata mkienda kazini, yuko likely kujifunza haraka hata kama alisomea chuo kibovu as long as ana cheti kinachostahili! After all haya mambo ya bussiness studies na humanities, si masomo mahumu sana!

ANGALIZO: Kuhusu chuo kibovu: vyuo vingi Tanzania, curriculum zake is a hard nut to crack, labda tofauti itakuja kwenye usimamizi. Walimu wengine wanaachia wanafunzi kwa sababu tofauti na nyingi, na roho njema ikiwemo. Mwingine ananaamua kumwachia mtu akajihangaikie huko, ajivue lawama ya kummaliza, na wengine wanatoa hela au K, sasa zote ni dynamics na haziko restricted kwa chuo kimoja!
 
we mwehu nini? Waliosoma na wanaosoma udsm wote mwishowe huwa na akili kama za kaputeeeeeeeeeeiiiiiiiiin makamba. Hamna kitu pale zaidi ya ngono na ukimwi. Usitupostie upupu wako humu
Punguza hasira pls. Umesahau kucite reference maana allegations km hizi inaonekana zimekuwa researched. Mwisho umejikuta unageneralise. Pitia CV ya Makamba uione elimu yake. Na hii ya ukimwi tujulishe pls kunatakwimu zipi za chuo zilizotolewa zinaonyesha hivyo. Nashauri tufikiri kuimarisha vyuo vyetu na si kukejeliana na kupuuzana
 
Mitandao ya vyuo vyetu inatia kichefu chefu. Yaani hakuna Profile za wanataaluma wao, achana na vitu vidogo kama picha. Haya ndiyo nimeyapata kwenye website ya UDSM: M.L. Baregu, A.L.A. (UK), B.A. (Brock), M.A. (Dar), Ph.D. (Stanford)(http://www.pspa.udsm.ac.tz/Webpages/Academic%20Staff.html).


Hapo kwenye red; siku nyingine jaribu kutafuta taarifa mwenywe kwenye Google.com ili na wengine tufaidi!!

Kamanda mie nilitype google nikakuta information kama ulizozipata amesoma katika chuo kizuri sikatai ila nachoshangaa mie ni kwanini anganganie UDSM kama hawamtaki. Uzuri wa academic ni kwamba kama UDSM hawakutaki Tumaini wanakutaka. Kama Tanzania hawakutaki Uganda wanakutaka in as along as umefanya utafiti wa kutosha, ufahamu mzuri na ufundishaji makini.

Sasa kama ulipublish katika magazeti tu kufurahisha wanasiasa then unaweza kuenda katika siasa ijapokuwa kwangu kupublish katika magazeti sihesabu kama publication. But kwa nchi kama yetu changa inatosha sasa asingangane na UDSM dunia pana aende kokote anakopaona panafaa kwani tunasoma ili tuwe na maisha mazuri sio kusoma ili usifiwe umesoma sana lakini maisha hamna. Huwezi jua pengine ndio malengo ya Baregu kusifiwa maana duniani tunatofautiana
 
Wakuu,

Taarifa zilizopo ni kuwa UDSM walipeleka jina la Baregu pamoja na majina mengine kwa ajili ya kupata aproval ya Serikali Kuu ili waweze kuongezewa mkataba. Kilichotokea ni kuwa jina la Baregu halikurudi. Baregu mwenyewe alikaririwa akisema kuwa hata alipomuuliza VC hakuweza kumpa sababu kwanini jina lake halikurudi.
 
When one door is closed many more are opened. Prof hakuna kufa moyo vyuo vipo vingi. na hata wanaosema vyuo vingine vipo sub standard nadhani kuna procedure inayotakiwa kufuatwa mpaka kukubalika kuitwa University
 
mimi nashangaa kwanini UDSM wanapoomba ajira za mikataba serikalini wapeleke majina ya watu badala ya idadi ya wahadhiri wanao wataka katika kitivo husika. Hii itasaisia kuondoa chuki binafsi dhidi ya majina husika yaliyopelekwa
 
Ndugu,

Na mimi napenda kuungana na watoa maoni kwa kunjimwa kazi kwa Prof.Baregu ni kwa sababu ni mwanachama wa CHADEMA na Mzalendo(this is politically motivated) Lakini mheshimiwa Baregu ni mhadhiri mahiri ambaye anachambua mambo kwa kina na anaikosoa serikali inapoenda kinyume na matakwa ya wananchi.
Elisante Yona
 
CHADEMA wamsimamishe kuwa mgombea urais mwakani kama anafaa kuwa rais siyo wanang'ang'ania Mbowe na ubaguzi wake wa kikabila. akidhani anajenga chama kuweka wachaga.
 
CHADEMA wamsimamishe kuwa mgombea urais mwakani kama anafaa kuwa rais siyo wanang'ang'ania Mbowe na ubaguzi wake wa kikabila. akidhani anajenga chama kuweka wachaga.

Mkuu unatakaje Chadema wamsimamishe huku wewe mwenyewe huna hakika kama anafaa?
 
Back
Top Bottom