Kwa nini Mungu alimuumba binadamu?

Hiyo dhana ya "Muumba ulimwengu" sio fact ni assertion ambayo imeandikwa kwenye Biblia

So kama Muumba ulimwengu ni fact kwasababu Biblia imeandika

Basi Spider-Man is real because there's also a book about him
 
Mimi na Mungu ni tofauti. Mimi ni binadamu lazima nilete mawazo yangu kwenye vitendo ndio uwezo wangu udhihirike. Mungu ni muweza wa yote hakuna analoshindwa kwaiyo hakuna mantiki ya yeye kudhihirisha chochote.
 
Spiderman au Harry Potter tunajua waandishi wao na waliziandika kama burudani.
Kwa hiyo Biblia na Quran haziwezi kuwa ni hekaya kwasababu waandishi hawajulikani?

Maudhui ya kitabu, uhalisia wake haupimwi kwa kuangalia nani ameandika.

Tunaweza kuyatambua maudhui ya uongo yaliyomo ndani ya kitabu pasipo kuhitaji kumjua mwandishi.
 
Duh, yaani bado unakomalia kuwa vitabu vya dini ni sawa na hekaya za Abunuwasi au Harry Potter?

Kama uhalisia haupimwi kwa kumjua mwandishi basi pima maudhui yaliyomo ndani ya hivyo vitabu.

Na kama ni rahisi kusema ni uongo, nipe kosa moja la kimaudhui kwenye hivyo vitabu linalothibitisha kuwa ulimwengu haukuumbwa na supreme being, acha porojo za kusikia mitaani mzee, leta logic.
 
Jibu ni rahisi tu, HATUJUI.

Hiyo mifano tata ya kisheria si lazima utata wake umaanishe Mungu, vipi kama ni ulimwengu wenyewe ndio ume create hizo pattern ila tumeangukia kwenye majibu potofu ya Mungu kwasababu tumeshindwa ku crack hiyo code kwasababu ya utata wake.

Kwanini usifikirie kuwa, hiyo dhana ya utata uliyoitaja ambayo haiko wazi kwasababu ya utata wake, inaweza kukufanya uwe karibu zaidi kuangukia kwenye majibu potofu (Mungu) ambayo wewe una confidence nayo kuwa ni sahihi?
 
Mwanzo 1:26–28
"Kisha Mungu akasema, 'Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vinavyotambaa juu ya nchi'

Vipi wanaosema alituumba ili tumuabudu??
 
Hilo swali wewe mwanadamu ndio unatakiwa uyatafute majibu yake mpaka uyapate. Umepewa akili. Wewe ukijiuliza hivyo na sokwe watafanya nini maana sokwe hawana akili..
Sokwe wanayo akili.
 
Hiyo dhana ya "Muumba ulimwengu" sio fact ni assertion ambayo imeandikwa kwenye Biblia

So kama Muumba ulimwengu ni fact kwasababu Biblia imeandika

Basi Spider-Man is real because there's also a book about him
View attachment 3650840
Dhana ya uwepo wa Muumba haikutokana na Biblia wala Quran, ilianza kama hoja ya kifalsafa na kisayansi hata kabla ya vitabu vya dini kuandikwa, ni wazi hili hukuwa ukilijua kabisa.

Mantiki yake iko hivi, imwengu una mwanzo hata sayansi kupitia Big Bang Theory inakubali hili, na chochote chenye mwanzo kimesababishwa na kitu kingine kilicho nje yake.

Hauwezi kuwa na ulimwengu tata wenye laws of physics bila kuwa na uncaused cause, biblia au Quran hazikuunda dhana ya Mungu, bali zimeelezea tu na kumpa sifa Muumba ambaye uwepo wake unathibitishwa na ulimwengu wenyewe.

Spiderman hana uhusiano na asili ya ulimwengu, yeye ni tabia tu ndani ya kitabu. Mungu ndiye aliyesababisha hata huyo mwandishi wa spiderman awepo.
 
Alikuwa anapungukiwa nini asipoabudiwa na wanadamu wasipojaribiwa ?
 
Mimi na Mungu ni tofauti. Mimi ni binadamu lazima nilete mawazo yangu kwenye vitendo ndio uwezo wangu udhihirike. Mungu ni muweza wa yote hakuna analoshindwa kwaiyo hakuna mantiki ya yeye kudhihirisha chochote.
Huelewi kabisa wewe, kama yeye ni muweza wa yote, ina maana anakatazwa au anashindwa kuwa na nia ya kudhihirisha utukufu wake? Kivipi yani?

Mbona hoja yako haina mantiki yoyote.
 
Oyaaa! Mzee mwenzangu LIKUD njoo ujionee jinsi Mungu wako alivyokuwa na a.k.a nyingi, mademu wa king Mswati wakasome.

Yaani aliases kibao utafikiri con artist bhana!
 
Kabla ya kutuumba alikuwa anadhihirishaje utukufu na ukamilifu wake ?
Unatakiwa uelewe muda ni sehemu ya uumbaji. Muda ulianza pale ulimwengu ulipoanza, Mungu haishi ndani ya muda, yeye yuko nje ya muda kwake hakuna kabla wala bada.

Kule kwenye umilele, Mungu alikuwa kamili na utukufu wake ulikamilika ndani ya utatu wake bila kuhitaji kitu chochote cha nje, hakukuwa na muda uliokuwa unapita akawa anasubiri kutuumba.

Kitendo cha kuumba ulimwengu ndio kilichoanzisha sekunde, dakika, na miaka tunayoijua sisi leo, kwahiyo wewe swali lako la kabla ya kutuumba alikuwa anafanya nini halina mantiki ya kisayansi wala kifalsafa, kwa sababu hakukuwa na kabla abla ya uumbaji! Umeelewa?
 
Huyo Mungu yupo so insecure kwamba hawezi kujidhihirishia huo utukufu na ukamilifu wake yeye mwenyewe, mpaka aumbe binadamu?
Mtu mwenye uhakika na uwezo wake ndiye anayeamua kuumba na kuweka mifumo tata ya maisha duniani, insecure ni wewe unayeshinda JF ukifanya dhihaka kwenye mambo ya msingi kwa sababu tu unamiliki smartphone.
 
Alikuwa anapungukiwa nini asipoabudiwa na wanadamu wasipojaribiwa ?
Kwa mtazamo wa Qur’an, Mungu hakupungukiwa chochote wanadamu wasipomwabudu wala wasipojaribiwa.

Yeye ni Mkwasi na hahitaji viumbe.

Qur’an inasema:
“Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Allah, na Allah ndiye Mwenye kujitosheleza, Mwenye kusifiwa.” — Qur’an 35:15

Kwa hiyo, ibada ni kwa manufaa ya mwanadamu, si kwa Mungu. Na mitihani ya maisha haimaanishi Mungu anahitaji kitu; ni sehemu ya kuwapima na kuwafichulia matendo yao.


Qur’an 67:2: “...ili awajaribu ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri zaidi.”
 
Mtu mwenye uhakika na uwezo wake ndiye anayeamua kuumba na kuweka mifumo tata ya maisha duniani,
Huyo Mungu wenu hana tofauti na demu ambaye haamini uzuri wake mpaka wanaume wamsifie.

Je huyo Mungu wenu hajiamini na wala haamini utukufu na ukamilifu wake mpaka aumbe binadamu?
insecure ni wewe unayeshinda JF ukifanya dhihaka kwenye mambo ya msingi kwa sababu tu unamiliki smartphone.
Mungu wenu hana tofauti na demu anayetafuta attention za wanaume!

Kama aliumba binadamu ili adhihirishe utukufu na ukamilifu wake, Basi yeye mwenyewe hajitoleshelezi na wala haamini huo utukufu na ukamilifu wake. Akiwa mwenyewe.
 
Akili yako inawaza ujinga muda wote, utawezaje kujenga hoja zenye mantiki sasa?

Jifunze kutofautisha kati ya kuhitaji sifa na kushiriki utukufu kwanza halafu tuendelee.
 
Akili yako inawaza ujinga muda wote, utawezaje kujenga hoja zenye mantiki sasa?

Jifunze kutofautisha kati ya kuhitaji sifa na kushiriki utukufu kwanza halafu tuendelee.
Nakwambia hivi, Huyo Mungu wenu hayupo na wala hajawahi kuwepo.

Mnahangaika sana kumtetea kwa sababu HAYUPO kujitetea mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…