wengine wanachangia ila wamo humu humu wamejaa tele hawajui kutunza wake zao zaidi ya kukimbilia hao wauza bar na kisomo chao cha msaada wa serikali jamani washindwe na wafungiwe tuwataje
Natamani wafunguke ili tujue sababu labda tunaweza okoa baadhi ya familia.
jamani kwa wanamme mlooa
inakuwaje mkeo hadi akuibie pesa? Tena kwa kushirikiana na watoto wake mwenyewe?
Mie nadhani hapa kuna tatizo kubwa zaidi ya pesa. Hapa baba anaonekana kama 'intruder' nyumbani kwake mwenyewe.
Mke aliyemuoa hana tabia ya wizi wala udokozi leo kageukaje mwizi? Au kweli wababa wanapenda kusaidiwa kutunza mke?
Mme ana pesa kama nini anahonga tu afu mke hata hela ya mafuta ya kujipaka hadi auze ubuyu? Why?
Eti mie ndio naambiwa nisuluhishe, nisuluhisheje jamani hii familia?
Nataka niwaambie wakae wa-review kama wana haja ya kuendelea kuishi pamoja vinginevyo bora kila mtu akamate njia yake.
my bro blaine n kurt thanks for calling be blessed.
mdogo wangu Kongosho kwanza pole manake naona jinsi ulivyokuwa nervous sana juu ya hili swala. yawezekana kabisa nimetoa ushauri wangu at late times but naomba tu niseme kwani kuna kitu kimenigusa sana hapo.
kwanza nianze na wewe, Kongosho ndugu yangu unapoitwa kusuluhisha swala la kifamilia kama hili yakupasa uelewe kwamba hutakiwi kwenda ukiwa na negativity wala ukiwa na majiabau tayari. siku zote nenda kwenye kushauri kama vile mtafiti anapoingia maabara ili avumbue kitu, haendi akiwa na majibu bali anakwenda akiwa na focus kwamba mwisho nataka nipate nini? kwa jinsi nilivyousoma uzi huu its like tayari unayo majibu ya nini utakacho pata na kibaya zaid ukaenda ukiwa na focus ambayo kwangu mimi nisinge iwaza kabisa manake siku zote huwa nategemea nipate majibu mazuri. ingawa hili doesn't work out every time.
sasa nirudi kwa familia husika, jamani hivi kweli sawa silazimish watu wawe kama mimi na hili siwez kumwambia mtu afanye kwani lahitaji imani ya kweli tena isiyotetereka kitu ambacho ni kigumu sana miongoni mwa watu.
kutoka kwa huyu mama nimejifunza jambo moja kubwa sana ya kwamba anaweza kukaa na watoto wake waapanga njama za kumuibia baba lakini jamani hivi sasa huyu baba akishajua kuwa mnamsachi akawa akirudi nyumbani wallet ni nyeupe je wataiba wapi tena? manake anao uwezo wa kuzificha hela hata kwenye gari ama kwa kimada ili mkose.
jamani naomba nisiseme nini kifanyike manake...............
platozoom siokwamba naogopa bali najua nitakayosema ni mazito na ambayo pengine wengine hawayawazi kabisa.wale waliaokutana na mimi kwenye maswala ya ushauri wanaweza kukuthibitishia hili. kwa sasa Kongosho amesha kwenda shaurini so haina maana tena.Hapo kwenye red ndipo nimepaona kwanza!
Kwenye blue usiogope mitazamo yabisi ya wengine kuhusu kile unachoamini kwa dhati......Kila mtu ana namna yake anavyopokea ushauri.................Ni heri ushauri "mbaya" wa yule anayeamini kwa dhati ya moyo wake kuliko ushauri wa kizandikii wa kufurahisha baraza au kupakazana usasa wa kuiga!
Endelea.................................
Nimesahau.......ngoja nielekee disco vumbi.......Hali ngumu ya maisha lakini hata kufurahi tushindwe...kha!
Natamani wafunguke ili tujue sababu labda tunaweza okoa baadhi ya familia.