Kwa nini magazeti ya Tanzania leo hayana story hii muhimu

sikiolakufa

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
411
0
Nimejaribu kupitia magazeti leo jumapili sioni hata moja lililocover story ya serengeti ikiwa serikali imenawa mikono kutokana na shinikizo la marekani...embu ona serikali ilijifanya kichwa ngumu...wakenya wakachombeza...barabara ikijengwa itaathiri migration ya nyumbu kwenda kenya....obama ni mkenya...marekani wakapigilia msumari wa mwisho jeneza la tanzania kudadadeki​
 
Daffi

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
3,827
2,000
Wanaogopa maana serikali itaona kama vile imeshindwa na inaogopa
 
Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,334
2,000
Swala la kutoitangaza hiyo stori sifahamu, lakini mimi sikutaka ijengwe! Serikali yetu inaugonjwa wa kudharau ushauri wa wataalamu ndio maana nchi inazidi kudidimia kiuchumi. Wataalamu wameshauri isijengwe sababu itaathiri mazingira, uchumi na utalii halafu serikali ikaleta dharau. Thanx americans for this!
 
Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,085

Kwangu mimi ni furaha kubwa na of course sikuwa ninailewa serikali hii ya viziwi katika hili kwani niliona kama sababu zilukuwa so obvious. Lakini jingine hivi bado tunasubiri watu wa nje watusaidie kuamua hata mambo yetu wenyewe kweli tutafika kwa style hii? Katika hili Obama ana intreset kwa sababu ya asili yake sasa kule ambako hana interest ina maana ndio tutakuwa tunaingizwa mkenge mpaka lini?
 
NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,738
2,000
Binafsi nilitegemea haya toka ubishi ulipoanza. Barabara ilie ilitaka kujengwa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kuonesha misuli (muscle flexing) kwa upande wa serikali. Tunategemea utalii kwa mapato ya kigeni, swala na wanyama si la Tanzania pekee, Kenya imo pia. Kama tungelazimisha hili, ni wazi athari zake zingekuwa far-reaching, in the long term!! Au ni hukumu ya udhaifu wa serikali yetu kiushawishi au kiutendaji.

Acha serikali hii iaibike. Wajifunze kusema vitu pre-maturely kuna gharama yake. Scientific facts will always carry more water than political opinions.
 
JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
0
Magazeti mengi yamejikita kwenye siasi zaidi, labda labda hawakupata matokeo muda muafaka kabla hayajaanza kuchapishwa
 
Maga

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
329
225
Tatizo viongozi wetu hawafokirii kesho, wao wakishiba basi hawajui kuwa matokeo ya maamuzi yao ya leo yataonekana kizazi kijacho, nawashauri viongozi wetu wawe na long term plan
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,874
2,000
Media za TZ kuacha kuandika habari za maana na maslahi kwa watanzania ni kawaida yao . Leo barabara lakini juzi tu wameshindwa kuandika kwa nguvu zote mauaji ya raia wema kule Nyamongo Tarime . Hao waita waandishi wa habari au waharibu habari ?
 
Sabayi

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
2,314
2,000
Hivi nani kawaambia Tanzania kuna waandishi wa habari? Pumba tupu!!!!! Binafsi nilikuwa nataka sana hii barabara ijengwe mi sioni hiyo faida ya utalii cause mapato ya utalii yanatumika kumsafirisha ****** na mkewe nje ya nchi tu kila siku na kununua ma V8 ya viongozi bora tujengewe barabara tupite tu tujue moja
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532

Unashutumu wakati tayari umeambiwa kwamba imeandikwa kweye Guardian. Au hilo si gazeti la Tanzania?
 
Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,279
2,000
Mie pia nilitarajia uamuzi huu tangu mwanzo wa sakata hili. Wapi na wapi Tanzania kuweza kupinga maamuzi ya madola yanayoipatia zaidi ya asilimia 50 ya bajeti yake? Ila naona uongozi wa nchi hii mpumbavu na hauna upeo wa fikra. Tayari uharibifu umekwishafanywa katika mahafali ya kimataifa bila ya sababu yeyote. Sasa kweli Kikwete alikuwa atarajia ataijenga hata kama wahisani wake anaowapelekea bakuli kila siku wakikataa? Huu ni upumbavu wa kitoto. Alitaka awaoneshe Watanzania kuwa yeye ni 'rais' na anaweza kuamua lolote? Ajifunze toka leo kwamba muda wa kuwa unamtegemea mwingine kwa kula yako wewe huko huru.
Kama ana akili ataanza tangu leo kuona kuwa hawategemei wazungu wake anaowaona ni baba na mama zake wa kukimbilia kila anapoharibu uchumi wa nchi yake.
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
Nimejaribu kupitia magazeti leo jumapili sioni hata moja lililocover story ya serengeti ikiwa serikali imenawa mikono kutokana na shinikizo la marekani...embu ona serikali ilijifanya kichwa ngumu...wakenya wakachombeza...barabara ikijengwa itaathiri migration ya nyumbu kwenda kenya....obama ni mkenya...marekani wakapigilia msumari wa mwisho jeneza la tanzania kudadadeki​

Haiwezi kuwa story wakati habari ni ileile kwamba kipande cha 50 kilometa ndani ya Hifadh hakitajengwa; na uamuzi huo ni wa siku nyingi. Labda upya wake ni kuwa wanaharakati waliokuwa wanashikia bango hii isho hawakuwa wameliona hilo na sasa baada ya kutangazwa BBC ndio ikawa habari mpya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom