Kwa nini magazeti ya Tanzania leo hayana story hii muhimu

florian kaijage ni yule mwandishi aliyefukuzwa TFF, amekopi kwa sababu hamna sources mpya kwenye story ile zaidi ya kuweka background
 
Binafsi nilitegemea haya toka ubishi ulipoanza. Barabara ilie ilitaka kujengwa kwa misingi ya kisiasa zaidi na kuonesha misuli (muscle flexing) kwa upande wa serikali. Tunategemea utalii kwa mapato ya kigeni, swala na wanyama si la Tanzania pekee, Kenya imo pia. Kama tungelazimisha hili, ni wazi athari zake zingekuwa far-reaching, in the long term!! Au ni hukumu ya udhaifu wa serikali yetu kiushawishi au kiutendaji.

Acha serikali hii iaibike. Wajifunze kusema vitu pre-maturely kuna gharama yake. Scientific facts will always carry more water than political opinions.

Tanzania haitegemei utalii wowote. Zaidi ya asilimia 80 ya watalii wa nje wanaokwenda Serengeti, Ngorongoro na Kilimanjaro wanaingilia Kenya. Na safari zao zote huwa wanakwenda Kenya, halafu kenya ndiyo inayowaleta kwa jirani Tanzania kwa malipo kidogo tu huku mapato halisi ya utalii yakienda kwenye makapmuni ya utalii ya Kenya kama vile mahoteli na tour operators.

Mapato ya utalii siyo ile fee ya kuingia kwenye mbuga, bali ni yale matumizi ya hao watalii kwenye mahoteli na sehemu nyinginezo wawapo nchini; sasa wao haji Tanzania, kwa hiyo matumzi halis ya utalii yanakwenda Kenya
 
kwangu mimi ni furaha kubwa na of course sikuwa ninailewa serikali hii ya viziwi katika hili kwani niliona kama sababu zilukuwa so obvious. Lakini jingine hivi bado tunasubiri watu wa nje watusaidie kuamua hata mambo yetu wenyewe kweli tutafika kwa style hii? Katika hili obama ana intreset kwa sababu ya asili yake sasa kule ambako hana interest ina maana ndio tutakuwa tunaingizwa mkenge mpaka lini?
ndg zangu hii nchi imekuwa masikini wa pesa na mawazo ndiyo maana kila linalotoka amerika ni sahii, sisi tunalala wao wanafikiri badala yetu.
 
Swala la kutoitangaza hiyo stori sifahamu, lakini mimi sikutaka ijengwe! Serikali yetu inaugonjwa wa kudharau ushauri wa wataalamu ndio maana nchi inazidi kudidimia kiuchumi. Wataalamu wameshauri isijengwe sababu itaathiri mazingira, uchumi na utalii halafu serikali ikaleta dharau. Thanx americans for this!

itaathiri mazingira kivipi? hivi mazingira ni serengeti tu? je sehemu zingine ilizojengwa haiathiri mazingira?
mbona mikumi imejengwa na maisha yanaenda tu? cdhani kama watz tumewekeza vya kutosha
katika utalii kiasi kwamba tuathirike kwa kujengwa barabara hiyo. watz wengi tunahangaika kusafiri
kisa ni serengeti? tena mi naona ni mradi binafsi kama yalivyo madini. tunaishia tu kupata side effects
tu na wachache kunufaika.
 
Back
Top Bottom