Kwa nini maandamano October 29 yalifeli?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,243
Reaction score
79,793
KWA NINI MAANDAMANO OCTOBER 29 YALIFELI?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kwanza nitoe pole kwa yote yaliyotokea. Waliathiriwa na kuathirika kwa kuuawa, kujeruhiwa na kuharibiwa biashara zao.

2. Niliandika uzi kueleza namna gani maandamano ya October 29 yatakavyofeli. Sikuandika kwamba hayatofanyika. Hivyo wale mnaoninukuu basi wekeni kumbukumbu zenu sahihi.

3. Kimsingi nilijua maandamano ya October 29 yasingezidi masaa sita. Na ndivyo ilivyokuwa. Kama mtakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa maandamano yatafeli(kumaanisha yatakuwepo ila hayatafanikiwa) na yakijitahid basi hayazidi masaa sita.

4. Hapa nitaandika kama mchambuzi. So wasomaji kazi yenu ni kusoma. Sitawaamulia namna ya kufikiri, kuelewa, kupokea na kutoa maoni yenu.

5. Nitaeleza kwa nini maandamano ya October 29 yalifeli sio kwa sababu ya kusikia au kuhadithiwa au kuota bali nikiwa shahidi na shuhuda kwa kilichotokea.

6. Sitampendelea mtu wala sitamuonea Mtu. Nitaeleza kichambuzi. Sehemu ya makosa ya waandamanaji nitasema, sehemu ya makosa ya Askari pia nitasema.

7. Hoja za kufeli maandamano nilishazitoa kabla ya maandamano. Lakini hoja chache ndizo zilizojitokeza na kuyafanya yasifanikiwe kwa ground.

8. Hoja ni kama ifuatavyo;
a) Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwa Waandamanaji.
Hii hoja niliitaja kabla ya maandamano na nilisema itakuwa moja ya hoja zitakazofelisha maandamano.

Siku ya maandamano waandamanaji walikuwa na maslahi na malengo yaliyopishana na kukinzana.
I) Wapo waliokuwa wanataka reforms na mabadiliko ya kweli ya nchi. Hawa walikuwepo. Na niliwasikia.

ii) Wapo waliokuwa wanahitaji Kumtoa Rais Samia suluhu Ikulu. Hawa mpango wao ulikuwa kufika Ikulu na kumng'oa Rais. Walikuwa wakiimba hivyo na kusema na walikuwa wanahakika mpaka usiku wangekuwa wamefika Ikulu.

iii) Wapo ambao walikuwa wanahitaji Watu waliotekwa na kupotezwa.

iv) Wapo ambao walikuwa wanaandamana kama mchezo fulani hivi wa maonyesho. Unaweza kushangaa lakini watu hao walikuwepo. Na niliwaona.

v) Wapo ambao walikuwa na matatizo mengi ambayo hayaelezeki. Hawa walikuwa wakilia tuu. Waliiona huenda siku hiyo ingekuwa siku ya mabadiliko ya matatizo yao.

vi) Wapo ambao kwao hiyo ilikuwa fursa ya kufanya Uhalifu kwa kuvunja na kuiba mali za watu. Watu hao walikuwepo.

Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwenye maandamano kuliyafanya yadhibitiwe.

Nilieleza hapa kwenye uzi wangu wa MY SIDE: matukio ya uhalifu yalifanya waandamanaji kugawanyika na kupungua wengine wakarudi nyumbani. Siongei kukisia au kutunga kama zile riwaya zangu. Hapa nazungumzia kilichotokea.

b) Ukosefu wa Uongozi wakati wa maandamano.
Watu wengi wenye malengo hasa ya kiharakati na kutaka mabadiliko bila kiongozi ni ngumu sana kufanikiwa.

I) Yalifeli kwa sababu hakukuwa na chain of command. Hapakuwa na kiongozi wa kutoa maelekezo na kufuatwa.
Hapakuwa na good organization wakati wa maandamano.
Kila mtu alijifanyia anavyojua. Wengine waliimba, wengine walirekodi, wengine walirusha mawe, wengine walichoma moto, wengine walikuwa wanavamia.

ii) mara kadhaa kulikuwa na mabishano baina ya waandamanaji. Wengine wakisema tufanye hivi wengine hapana jamani tusifanye. Wengine wakikataza uharibifu wengine wakishadadia uhalifu na wengine wakifanya.

iii) Kila barabara ya waandamanaji ingepata viongozi huenda mambo yangeenda vizuri. Na viongozi wapatikane siku ya tukio.

iv) ukosefu wa viongozi tafsiri yake ni kushindwa kufanikisha malengo ya maandamano bila kujali kama yalikuwa na nia njema au mbaya.

c) Kundi la Wahalifu liliharibu muelekeo wa maandamano na kuyafanya yafeli kwa haraka.

i) Niliandika maandamano yalianza kidogo kidogo saa tatu kuelekea saa nne.
ii) Mpaka saa nne na nusu maandamano yalikuwa hayana uhalifu na fujo zile za kutisha. Hata Jeshi la Wananchi JW lilikuwa linalinda raia.
Kwa ambao hamkuwepo hata nyie mliona kwenye video ambazo zimepostiwa mitandaoni.

iii) Wahalifu hasa Wezi na wachoma vituo vya mwendokasi, vituo vya mafuta, vituo vya kuhesabia kura n.k. hawa ndio walibadilisha upepo wa tukio zima.
Hayo yalianza saa tano kuelekea saa sita ambapo yalidumu kwa takribani masaa matatu. Kwa kukata kata. Yaani sio ile non stop.

iv) Hivyo kulikuwa na wahalifu wa maslahi yao binafsi yaani kuiba vitu. Lakini kulikuwa na wahalifu wa kutaka kukomoa serikali na watu fulani hawa ndio walichoma vituo vya mwendo kasi na wengine nyumba za ccm, na watu kadhaa mashuhuri.

9. Askari na Polisi nao hawawezi kukwepa Lawama katika tukio hili.

10. Wao ndio wamesomea kazi hiyo na wanaowajibu wa kulinda watu na mali zao.

11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu.

13. Kama walivyofanya JW wakati wa asubuhi kusaidia waandamanaji waandamane ila kwa usalama bila kuumizana, kuharibu mali na kuleta vurugu hata polisi nao wangeweza kufanya hivyo.

14. Hapakuwa na sababu ya kuuana kwa kiwango kile kama hatua sahihi tangu dakika za awali zingefanyika.

15. Polisi wamekosea pakubwa kutumia nguvu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi.

16. Viongozi wa serikali, vyombo vya dola vinapaswa kujua kuwa saikolojia ya Wananchi ni tofauti na saikolojia ya Polisi au Maaskari.

17. Niligundua pia moja ya madhara Makubwa yamesababishwa na tatizo la tofauti za kisaikolojia baina ya Askari na wananchi.

18. Askari na vyombo vya dola wao saikolojia yao inaongozwa kwa kufuata Amri ya mkubwa bila kujali uhalali wake.
Ila saikolojia ya wananchi au raia hawaongozwi na kwa kufuata amri bila maelezo. Utawala wa kiraia unajenga saikolojia ya kuhoji, kutoa maoni na ikiwezekana kupinga ikiwa amri sio halali.
Hao ni wananchi.

19. Hivyo Polisi anavyomchukulia Rais Samia ni tofauti na raia wa kawaida anavyomchukulia Rais Aamua.
Polisi humchukulia Rais kama Boss wake, mkuu wa kazi na Amir jeshi Mkuu.
Wakati mwananchi humchukulia Rais kama kiongozi aliyemchagua ambaye anamlipa pesa kupitia kodi asimamie rasilimali za nchi ikiwemo watu(yeye)

20. Raia haoni shida kumkosoa Rais au kiongozi yeyote wa nchi kwa sababu kisaikolojia mwananchi anajua yeye ndiye amemuweka pale.
Wakati Polisi Rais akikohoa tuu kidogo atafanya tuu bila kuuliza bila kusita.

21. Polisi, vyombo vya dola ni muhimu kuelewa kuwa mazingira yenu ya kazi hayahusiani na mazingira ya wananchi wengine ambao sio Polisi.
Utawala wa kiraia hasa kwa nchi yenye demokrasia kama yetu ni tofauti na utawala wa kijeshi wa kupokea amri tuu.

22. Lazima tuelewe kuwa Kama Polisi na vyombo vya dola vitaleta mambo yao ya kijeshi kwa raia wananchi wengi watazidi kuumia sana kwani jeshini ndio hakuna ukosoaji, hasa kumkosoa na kumpinga kiongozi aliye juu yako.

23. Rais Samia kama kiongozi wa nchi pia ni muhimu kuelewa kuwa yeye ni Amir jeshi lakini hatakiwi kutumia kanuni za jeshi kwa wananchi wa kawaida.

24. Ili kuondoa mgongano kati ya utawala wa kijeshi na utawala wa kiraia ni vizuri utulivu, hekima, utu na uzalendo vitangulizwe mbele.

25. Kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unaposema watu wasiandamane kwa kutumia koti la kijeshi ni kuleta maumivu, mauaji na majeraha kwani lazima wapo wananchi ambao wao hawakusikilizi kama Amri jeshi mkuu bali wanakusikiliza kama raia mwenye cheo cha urais.

26. Sasa Amir jeshi umesema watu wasiandamane. Watu wakafanya hivyo. Automatically utaona wanakudharau jambo ambalo sio lazima liwe kweli.
Sio kwamba wanakudharau nope! Wao wanaona ni haki yao kuandamana na kudai wanachodai. Na wao saikolojia yao wanaamini nchi yao ni ya kidemokrasia

27. Hasira za polisi au vyombo vya dola kufikiri vimedharauliwa na hasira zisizo halali kabisa kwani hakuna wananchi wanaodharau askari wao, jeshi lao, au vyombo vya dola;

28. Isipokuwa Polisi na vyombo vya dola wanataka kutumia kanuni za kijeshi kwa wananchi wanaoamini utawala wa kidemokrasia.
Kutokuelewana huko ndio kunatokeaga mvurugano.

29. Sio tuu katika sakata hilo lililopita. Hata katika masakata mengine.
Zipo hadithi Unakuta baadhi ya wanajeshi wanataka kuishi mtaani kama wanajeshi kwa kutumia falsafa za kijeshi mtaani jambo ambalo wakati mwingine inaripotiwa ikileta shida. Kwamba Mjeshi au Askari anataka ukiongea naye uwe kama unaongea sijui na nani jambo ambalo sio sahihi kabisa.

30. Nikielekea kumaliza, Vyombo vya dola, askari polisi na wengine tukio kama hili lisijirudie. Tunapofanya kazi tusifanye kuonyeshana umwamba, kukomoana, hayo sio maadili ya kazi. Hivyo kilichofanyika hata kama ni kudhibiti uhalifu ulikuwa na ukatili na unyama uliopitiliza.

31. Hii inaweza kuleta matokeo mabaya na kuleta chuki na dhana potofu kuhusu kazi ya uaskari ambayo mimi kama Mtibeli naamini na kujua ni moja ya kazi njema na nzuri katika maisha ya viumbe. Kumbuka hata malaika wa mbinguni ni Askari na wanajeshi.
So ni muhimu kila askari kutafakari na kufanya wajibu wake. Ili kuifanya kazi ya uaskari iheshimiwe na mtu akipita asione aibu kujitambulisha kwa watu kubwa yeye ni Askari Polisi.

32. Mwisho, hakuna namna sahihi ya watu kudai haki zao zaidi ya maandamano. Kuzuia maandamano ni kutengeneza ufa mkubwa wa watu kutafuta njia nyingine ngumu zaidi ambazo sio salama kwa taifa.

33. Ni muhimu maandamano yapewe ulinzi na askari ili kupunguza madhara.
Lazima ijulikane kuna watu wanamadai yao. Ni muhimu kuyasikiliza ili tuende pamoja. Tusiende mbali tukawaacha wengine nyuma wakinung'unika.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster.
Kwa sasa Dar es salaam
 
Watu sijui mnatumia makalio kujenga hoja? Maana sielewi.

Yaani kutoka kuambiwa "hakuna mtanzania hata mmoja mwenye uthubutu wa kuandamana...." mpaka kufikia hatua ya kuogopa hata kutaja idadi ya vifo, yet unaita ni KUFELI!!!. Shame on you
 
Unafanya kazi ya CCM. Huu ujinga kauandike gazeti la Uhuru.
 
Nikikumbuka nyuzi zako sambamba na akina Pascal Mayalla , Lucas Mwashambwa na kibaka Yericko Nyerere mliosema hakuna mtanzania hata mmoja ataandamana hata kuzunguka nyumba yake.

Na sasa mmegeuka wachambuzi wa maandamano mkiyaita yaliyofeli kama wewe na kibaka Yericko Nyerere akiita ni jaribio la mapinduzi lililofeli na Pascal Mayalla akisema ni vurugu za hapa na pale na kidampa Lucas Mwashambwa aliyetimkia mafichoni na kuzima simu baada ya kupata taarifa za uwepo wa Gen Z viunga vya mtaani kwake wakitaka kumsalimia ni dalili tosha hamna tofauti na kinyonga hivyo bora mkae kimya huu mnaoleta sasa hauna hadhi ya kuitwa uchambuzi labda tuuite UCHI WA MBUZI.
 
Mkuu ulisema hakuna anayeweza kuandamana hata mimi nilikuunga mkono ila kilichotokea ni suprise ambayo wengi hatukutegemea kama kuna vijana jasiri vile.

So ni bora tu ukae kimya au utoe pole kwa walioathirika ila kusema yalifeli ni statement ya ajabu sana.

Read the room!!
 
Nikikumbuka nyuzi zako sambamba na akina Pascal Mayalla , Lucas Mwashambwa na kibaka Yericko Nyerere mliosema hakuna mtanzania hata mmoja ataandamana hata kuzunguka nyumba yake.

Na sasa mmegeuka wachambuzi wa maandamano mkiyaita yaliyofeli wengins wakiita ni jaribio la mapinduzi lililofeli na mwingine akisema ni vurugu za hapa na pale ni dalili tosha hamna tofauti na kinyonga.
Asante.
 
Watu sijui mnatumia masaburi kujenga hoja? Maana sielewi.

Yaani kutoka kuambiwa "hakuna mtanzania hata mmoja mwenye uthubutu wa kuandamana...." mpaka kufikia hatua ya kuogopa hata kutaja idadi ya vifo, yet unaita ni KUFELI!!!.
Huyu Jamaa anajipa umuhimu sana sana humu,

Kuna mada aliileta kabla ya maandamano, akidai Familia yake imemkataza kushiriki maandamano,

Leo anasema ameyaona makundi yote na Nia zao akazijua,

Ataandika sana upuuzi humu, lakini msijali, Acha tuendelee kuomboleza ambao tumepoteza ndugu, na wale waliopoteza ndugu na pia hawakupata hata mwili wa kuzika kwa heshima
 
Yale hayakuwa maandamano ulikuwa uhalifu, japo ulipelekea vifo kwa watanzania wenzetu hata wasiohusika.
 
Maandamano hayakufeli, waliofeli ni wale waliotakiwa kulinda waandamanaji i.e Polisi.

Polisi wangetimiza wajibu wao, hakuna mali ya mtu hata moja ambayo ingeharibiwa, wao walipaswa kuwaongoza waandamanaji wa-raise concerns zao wanazozitaka. Badala yake polisi wakajikita na vitisho na kuanza kuwa-shoot raia.

Mpaka jeshi linaingia road kuwalinda waandamaji ina maana intelijensia ya uhakika ilikuwepo kwamba maandamano yapo na walikuwa na wana uhakika polisi wanachoenda kukifanya.

Malengo ya waandamaji yamefikiwa kwa 150%. Kwa sababu kinachoenda kutokea sasa hivi ni reforms, wapende wasipende!
 
KWA NINI MAANDAMANO OCTOBER 29 YALIFELI?

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kwanza nitoe pole kwa yote yaliyotokea. Waliathiriwa na kuathirika kwa kuuawa, kujeruhiwa na kuharibiwa biashara zao.

2. Niliandika uzi kueleza namna gani maandamano ya October 29 yatakavyofeli. Sikuandika kwamba hayatofanyika. Hivyo wale mnaoninukuu basi wekeni kumbukumbu zenu sahihi.

3. Kimsingi nilijua maandamano ya October 29 yasingezidi masaa sita. Na ndivyo ilivyokuwa. Kama mtakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa maandamano yatafeli(kumaanisha yatakuwepo ila hayatafanikiwa) na yakijitahid basi hayazidi masaa sita.

4. Hapa nitaandika kama mchambuzi. So wasomaji kazi yenu ni kusoma. Sitawaamulia namna ya kufikiri, kuelewa, kupokea na kutoa maoni yenu.

5. Nitaeleza kwa nini maandamano ya October 29 yalifeli sio kwa sababu ya kusikia au kuhadithiwa au kuota bali nikiwa shahidi na shuhuda kwa kilichotokea.

6. Sitampendelea mtu wala sitamuonea Mtu. Nitaeleza kichambuzi. Sehemu ya makosa ya waandamanaji nitasema, sehemu ya makosa ya Askari pia nitasema.

7. Hoja za kufeli maandamano nilishazitoa kabla ya maandamano. Lakini hoja chache ndizo zilizojitokeza na kuyafanya yasifanikiwe kwa ground.

8. Hoja ni kama ifuatavyo;
a) Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwa Waandamanaji.
Hii hoja niliitaja kabla ya maandamano na nilisema itakuwa moja ya hoja zitakazofelisha maandamano.

Siku ya maandamano waandamanaji walikuwa na maslahi na malengo yaliyopishana na kukinzana.
I) Wapo waliokuwa wanataka reforms na mabadiliko ya kweli ya nchi. Hawa walikuwepo. Na niliwasikia.

ii) Wapo waliokuwa wanahitaji Kumtoa Rais Samia suluhu Ikulu. Hawa mpango wao ulikuwa kufika Ikulu na kumng'oa Rais. Walikuwa wakiimba hivyo na kusema na walikuwa wanahakika mpaka usiku wangekuwa wamefika Ikulu.

iii) Wapo ambao walikuwa wanahitaji Watu waliotekwa na kupotezwa.

iv) Wapo ambao walikuwa wanaandamana kama mchezo fulani hivi wa maonyesho. Unaweza kushangaa lakini watu hao walikuwepo. Na niliwaona.

v) Wapo ambao walikuwa na matatizo mengi ambayo hayaelezeki. Hawa walikuwa wakilia tuu. Waliiona huenda siku hiyo ingekuwa siku ya mabadiliko ya matatizo yao.

vi) Wapo ambao kwao hiyo ilikuwa fursa ya kufanya Uhalifu kwa kuvunja na kuiba mali za watu. Watu hao walikuwepo.

Kutofautiana kwa maslahi na malengo kwenye maandamano kuliyafanya yadhibitiwe.

Nilieleza hapa kwenye uzi wangu wa MY SIDE: matukio ya uhalifu yalifanya waandamanaji kugawanyika na kupungua wengine wakarudi nyumbani. Siongei kukisia au kutunga kama zile riwaya zangu. Hapa nazungumzia kilichotokea.

b) Ukosefu wa Uongozi wakati wa maandamano.
Watu wengi wenye malengo hasa ya kiharakati na kutaka mabadiliko bila kiongozi ni ngumu sana kufanikiwa.

I) Yalifeli kwa sababu hakukuwa na chain of command. Hapakuwa na kiongozi wa kutoa maelekezo na kufuatwa.
Hapakuwa na good organization wakati wa maandamano.
Kila mtu alijifanyia anavyojua. Wengine waliimba, wengine walirekodi, wengine walirusha mawe, wengine walichoma moto, wengine walikuwa wanavamia.

ii) mara kadhaa kulikuwa na mabishano baina ya waandamanaji. Wengine wakisema tufanye hivi wengine hapana jamani tusifanye. Wengine wakikataza uharibifu wengine wakishadadia uhalifu na wengine wakifanya.

iii) Kila barabara ya waandamanaji ingepata viongozi huenda mambo yangeenda vizuri. Na viongozi wapatikane siku ya tukio.

iv) ukosefu wa viongozi tafsiri yake ni kushindwa kufanikisha malengo ya maandamano bila kujali kama yalikuwa na nia njema au mbaya.

c) Kundi la Wahalifu liliharibu muelekeo wa maandamano na kuyafanya yafeli kwa haraka.

i) Niliandika maandamano yalianza kidogo kidogo saa tatu kuelekea saa nne.
ii) Mpaka saa nne na nusu maandamano yalikuwa hayana uhalifu na fujo zile za kutisha. Hata Jeshi la Wananchi JW lilikuwa linalinda raia.
Kwa ambao hamkuwepo hata nyie mliona kwenye video ambazo zimepostiwa mitandaoni.

iii) Wahalifu hasa Wezi na wachoma vituo vya mwendokasi, vituo vya mafuta, vituo vya kuhesabia kura n.k. hawa ndio walibadilisha upepo wa tukio zima.
Hayo yalianza saa tano kuelekea saa sita ambapo yalidumu kwa takribani masaa matatu. Kwa kukata kata. Yaani sio ile non stop.

iv) Hivyo kulikuwa na wahalifu wa maslahi yao binafsi yaani kuiba vitu. Lakini kulikuwa na wahalifu wa kutaka kukomoa serikali na watu fulani hawa ndio walichoma vituo vya mwendo kasi na wengine nyumba za ccm, na watu kadhaa mashuhuri.

9. Askari na Polisi nao hawawezi kukwepa Lawama katika tukio hili.

10. Wao ndio wamesomea kazi hiyo na wanaowajibu wa kulinda watu na mali zao.

11. Ninaamini Kama Polisi wangeyaelekeza maandamano kwa njia salama yangefanyika bila kupigana risasi.

12. Namaaanisha Polisi wao wakati wa maandamano wangekuwa mbele kuwaongoza wetu. Watanzania ni waelewa kuliko ukitumia nguvu.

13. Kama walivyofanya JW wakati wa asubuhi kusaidia waandamanaji waandamane ila kwa usalama bila kuumizana, kuharibu mali na kuleta vurugu hata polisi nao wangeweza kufanya hivyo.

14. Hapakuwa na sababu ya kuuana kwa kiwango kile kama hatua sahihi tangu dakika za awali zingefanyika.

15. Polisi wamekosea pakubwa kutumia nguvu nyingi hali iliyopelekea kupoteza maisha ya watu wengi.

16. Viongozi wa serikali, vyombo vya dola vinapaswa kujua kuwa saikolojia ya Wananchi ni tofauti na saikolojia ya Polisi au Maaskari.

17. Niligundua pia moja ya madhara Makubwa yamesababishwa na tatizo la tofauti za kisaikolojia baina ya Askari na wananchi.

18. Askari na vyombo vya dola wao saikolojia yao inaongozwa kwa kufuata Amri ya mkubwa bila kujali uhalali wake.
Ila saikolojia ya wananchi au raia hawaongozwi na kwa kufuata amri bila maelezo. Utawala wa kiraia unajenga saikolojia ya kuhoji, kutoa maoni na ikiwezekana kupinga ikiwa amri sio halali.
Hao ni wananchi.

19. Hivyo Polisi anavyomchukulia Rais Samia ni tofauti na raia wa kawaida anavyomchukulia Rais Aamua.
Polisi humchukulia Rais kama Boss wake, mkuu wa kazi na Amir jeshi Mkuu.
Wakati mwananchi humchukulia Rais kama kiongozi aliyemchagua ambaye anamlipa pesa kupitia kodi asimamie rasilimali za nchi ikiwemo watu(yeye)

20. Raia haoni shida kumkosoa Rais au kiongozi yeyote wa nchi kwa sababu kisaikolojia mwananchi anajua yeye ndiye amemuweka pale.
Wakati Polisi Rais akikohoa tuu kidogo atafanya tuu bila kuuliza bila kusita.

21. Polisi, vyombo vya dola ni muhimu kuelewa kuwa mazingira yenu ya kazi hayahusiani na mazingira ya wananchi wengine ambao sio Polisi.
Utawala wa kiraia hasa kwa nchi yenye demokrasia kama yetu ni tofauti na utawala wa kijeshi wa kupokea amri tuu.

22. Lazima tuelewe kuwa Kama Polisi na vyombo vya dola vitaleta mambo yao ya kijeshi kwa raia wananchi wengi watazidi kuumia sana kwani jeshini ndio hakuna ukosoaji, hasa kumkosoa na kumpinga kiongozi aliye juu yako.

23. Rais Samia kama kiongozi wa nchi pia ni muhimu kuelewa kuwa yeye ni Amir jeshi lakini hatakiwi kutumia kanuni za jeshi kwa wananchi wa kawaida.

24. Ili kuondoa mgongano kati ya utawala wa kijeshi na utawala wa kiraia ni vizuri utulivu, hekima, utu na uzalendo vitangulizwe mbele.

25. Kiongozi wa nchi ya kidemokrasia unaposema watu wasiandamane kwa kutumia koti la kijeshi ni kuleta maumivu, mauaji na majeraha kwani lazima wapo wananchi ambao wao hawakusikilizi kama Amri jeshi mkuu bali wanakusikiliza kama raia mwenye cheo cha urais.

26. Sasa Amir jeshi umesema watu wasiandamane. Watu wakafanya hivyo. Automatically utaona wanakudharau jambo ambalo sio lazima liwe kweli.
Sio kwamba wanakudharau nope! Wao wanaona ni haki yao kuandamana na kudai wanachodai. Na wao saikolojia yao wanaamini nchi yao ni ya kidemokrasia

27. Hasira za polisi au vyombo vya dola kufikiri vimedharauliwa na hasira zisizo halali kabisa kwani hakuna wananchi wanaodharau askari wao, jeshi lao, au vyombo vya dola;

28. Isipokuwa Polisi na vyombo vya dola wanataka kutumia kanuni za kijeshi kwa wananchi wanaoamini utawala wa kidemokrasia.
Kutokuelewana huko ndio kunatokeaga mvurugano.

29. Sio tuu katika sakata hilo lililopita. Hata katika masakata mengine.
Zipo hadithi Unakuta baadhi ya wanajeshi wanataka kuishi mtaani kama wanajeshi kwa kutumia falsafa za kijeshi mtaani jambo ambalo wakati mwingine inaripotiwa ikileta shida. Kwamba Mjeshi au Askari anataka ukiongea naye uwe kama unaongea sijui na nani jambo ambalo sio sahihi kabisa.

30. Nikielekea kumaliza, Vyombo vya dola, askari polisi na wengine tukio kama hili lisijirudie. Tunapofanya kazi tusifanye kuonyeshana umwamba, kukomoana, hayo sio maadili ya kazi. Hivyo kilichofanyika hata kama ni kudhibiti uhalifu ulikuwa na ukatili na unyama uliopitiliza.

31. Hii inaweza kuleta matokeo mabaya na kuleta chuki na dhana potofu kuhusu kazi ya uaskari ambayo mimi kama Mtibeli naamini na kujua ni moja ya kazi njema na nzuri katika maisha ya viumbe. Kumbuka hata malaika wa mbinguni ni Askari na wanajeshi.
So ni muhimu kila askari kutafakari na kufanya wajibu wake. Ili kuifanya kazi ya uaskari iheshimiwe na mtu akipita asione aibu kujitambulisha kwa watu kubwa yeye ni Askari Polisi.

32. Mwisho, hakuna namna sahihi ya watu kudai haki zao zaidi ya maandamano. Kuzuia maandamano ni kutengeneza ufa mkubwa wa watu kutafuta njia nyingine ngumu zaidi ambazo sio salama kwa taifa.

33. Ni muhimu maandamano yapewe ulinzi na askari ili kupunguza madhara.
Lazima ijulikane kuna watu wanamadai yao. Ni muhimu kuyasikiliza ili tuende pamoja. Tusiende mbali tukawaacha wengine nyuma wakinung'unika.

Kufikia hapo sina la ziada.

TaikonMaster.
Kwa sasa Dar es salaam
Kwa kiasi kikubwa haya maandamano yanefanikiwa sana pamoja na vijana wengi kudhulumiwa uhai wao lakini ujumbe umefika bold and clear. Sema tu Samuya hana akili, lakini haya angekuwa tu na hata nusu ya akili ya kuendea chooni asingeruhusu hiki kilichotokea kifike hapo. Sasa hivi tungekuwa tunajadili IGP na Mkuu wa TISS kuwekwa ndani, waziri wa mambo ya ndani kuwekwa kando. Huu ujumbe uliotumwa na vijana utakuwa umewazindua. Sasa hivi huku mtaani tule tu umbwa twa ccm hatubweki tena!
 
Uzi wowote ambao nikiona tu mwandishi anaanza kwa maneno ya self defense (kutengeneza backup ya kumlinda) najua hapo hamna kitu zaidi ya bias na uzugaji.

Unaposema maandamano hayakuzidi masaa 6, ulitakiwa utuambie hii umeitoa kwa mujibu wa tafiti gani?

Au lah utuambie fact yako imezingatia muktadha wa eneo dogo ambalo wewe ulikuwepo kwenye hiyo siku.

Lakini ku generalize kusema maandamano hayakuzidi masaa 6, huo ni uongo pure.
 
Kwa kiasi kikubwa haya maandamano yanefanikiwa sana pamoja na vijana wengi kudhulumiwa uhai wao lakini ujumbe umefika bold and clear. Sema tu Samuya hana akili, lakini haya angekuwa tu na hata nusu ya akili ya kuendea chooni asingeruhusu hiki kilichotokea kifike hapo. Sasa hivi tungekuwa tunajadili IGP na Mkuu wa TISS kuwekwa ndani, waziri wa mambo ya ndani kuwekwa kando. Huu ujumbe uliotumwa na vijana utakuwa umewazindua. Sasa hivi huku mtaani tule tu umbwa twa ccm hatubweki tena!

Mafanikio yake ni ile kuonekana yalifanyika

Lakini tukirudi kwenye malengo ni kwamba yamefeli.

Kwa sababu swali litaulizwa, kwa nini watu waandamane?
Kisha litafuata, je madai ya maandamano yamejibiwa walau dai hata moja? Au malengo yamefikiwa?

Ni kwamba hayajafikiwa.
 
Mkuu umejitahidi kuelezea vizuri tena bila kuonyesha unaegemea upande fulani kama wachambuzi wengi uchwara wanavyofanya.

Nasema wachambuzi uchwara sababu kuna chambuzi moja maarufu sijui anaitwa rugby nani nani nilimsikiliza huko YouTube Nikasema hivi mchambuzi au mwanahabari kama huyu hivi anajielewa kweli na kazi yake kama neno lenyewe "uchambuzi" linavyosema au ndio Basi tu kukurupuka mradi kapata Channel ya kueleza tu anachohisi kwake yeye ni sawa Au pia ndio Matokeo ya kulamba asali kama wasemavyo wajuzi.

Nikija kwenye hoja zako kote umeeleza kwa usahihi kabisa kwa kuanzia na hoja no. 1 sababu ya Gen Z Kufeli ni Lack of Clear Leaders hii ni kweli kabisa na sababu kubwa yaweza kuwa ni kutokuwa na Elimu juu ya haya mambo vipi yanatakiwe yafanyike ama wenzetu (nchi nyingine) huwa WANAFANYA Je? Hii ni Assignment kwa siku nyingine

Sasa Viongozi wangekuwepo ndio wangeongoza wafuasi kipi cha Kufanya na kipi sio cha Kufanya ili kutoharibu Lengo mahsusi

PIA sambamba na Hilo la Waongozaji pia hapakuwa na MPANGO KAZI yaani PLAN NZIMA kwamba itafanyika hivi na watakusanyikia wapi, wawe na ujumbe gani kwenye mabango, na kwenye Media wazungumze nini kama hitaji lao la Msingi... Ukikosa hivi tegemea Kufeli tu.

TUJE KWA UPANDE WA POLISI
wao jukumu lao ni kulinda raia na mali zao. Tu assume pia wanafaham Haki ya raia kuandamana japo I'm not sure kwenye hili.

Ila sasa kilichotokea polisi waliona upenyo wa Kufanya ukatili wao baada ya kuona raia WANAFANYA uharibifu wa Mali (hasa za Wakubwa) hapa ndio ikawa piga ua badala ya dhibiti na fikisha kwenye vyombo vya sheria.

Ila kikubwa ni kwamba kuna vingi vya kujifunza hasa hasa kwa raia kama wanahitaji kufikisha kero zao bila kudhuru Uhuru wa wengine nini kifanyike I hope next time hakutatokea kama ilivyotokea mara hii.

UJINGA HUWA NI WAKATI WA KWENDA TUU SI WAKATI WA KURUDI.
 
Uzi wowote ambao nikiona tu mwandishi anaanza kwa maneno ya selfe defence (kutengeneza backup ya kumlinda) najua hapo hamna kitu zaidi ya bias na uzugaji.

Unaposema maandamano hayakuzidi masaa 6, ulitakiwa utuambie hii umeitoa kwa mujibu wa tafiti gani?

Au lah utuambie fact yako imezingatia muktadha wa eneo dogo ambalo wewe ulikuwepo kwenye hiyo siku.

Lakini ku generalize kusema maandamano hayakuzidi masaa 6, huo ni uongo pure.
Uko wapi ule uzi? Alisema wabongo "hawataandamana", you can get something wrong brother, take it easy
 
Back
Top Bottom