Kwanini hospitali zina mchoro na picha ya nyoka?

Sasa mkuu kama nyoka ni Genius kiasi hicho kwa nini wasitumiwe kutafuta Dawa za magonjwa sugu kama Ukimwi na Saratani??? Yaani nyoka anaambukiwa Ukimwi Then Anakuwa karibu na nyoka wengine na Akikaribia kufa wenzake lazima wataenda pori kutafuta Dawa then wanamfuatilia kimya kimya na kumfanyia surveillance hadi kwenye hiyo dawa watakayomleta mwenzao na tayari Dawa ya Ukimwi inakuwa imepatikana kupitia huo MTU utakaoenda kuchumwa na Nyoka wenzake
Sio kwamba anajua tiba za kila gonjwa mkuu, jaribu kuelewa na kufuatilia, wazee huko vijijini wamegundua dawa kwa style hiyo.

Ukimdhuru nyoka vizuri, jibanze tu sehemu utaona, wenzake wakimkuta hivyo lazima wajaribu kumtibu, hivyo walichofanya watu wanawafuatilia kwa makini wanaenda kung'ata mti, au majani gani waje kumtibu mwenzao.

Unaweza kudhani ni uongo ila ndio hivyo.
 
Ile ya muhimbili ni mnyoo (una historia yake na research, kasome) sio nyoka,,

Ila machame hospital nliona wanatumia nyoka na fimbo- hii nahis inahusiana na biblia
Yeah hii nembo inawakilisha Guinea worms "Dracunculus medinensis"ambao miaka hiyo alisumbua sana na dawa mojawapo ilikuwa ni kumtoa kwa kumvingilisha kwenye kijiti na taratibu sana ili asikatike na ndio ikawa mwanzo wa nembo hii ya Afya.
Habari zenu wana Jamvi.
Nimefuatilia sana hili swala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.sasa kwa nini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi AhsanteniView attachment 501467
 
Nafikiri kwa maelezo uliyotoa Fimbo ya Asclepius ndo ukweli na uhalisia wa Alama hii ktk sehem zinazotoa Huduma za Afya Ila Historia ya Fimbo na nyoka wa shaba Imeingizwa maksud ili kuwapotosha Wakristo na kuwavuta japo hawamaanishi Hbr za Musa

unafikiri ila huna uhakika sasa unataka nami niamini fikra zako?
 
Sio kwamba anajua tiba za kila gonjwa mkuu, jaribu kuelewa na kufuatilia, wazee huko vijijini wamegundua dawa kwa style hiyo.

Ukimdhuru nyoka vizuri, jibanze tu sehemu utaona, wenzake wakimkuta hivyo lazima wajaribu kumtibu, hivyo walichofanya watu wanawafuatilia kwa makini wanaenda kung'ata mti, au majani gani waje kumtibu mwenzao.

Unaweza kudhani ni uongo ila ndio hivyo.

sidhani ila naamini ni uongo wa mchana kweupe, wewe umewahi shuhudia au ulisimuliwa.
 
Nyoka ndiye mnyama mwerevu kuliko wote duniani basi hiyo alama itakuwa inamaanisha kuwa hospitali inatumika akili na werevu zaidi kufanya uponyaji.

nyoka ndio mnyama mwerevu kuliko wote duniani? unaweza fafanua? kwa mujibu wa utafiti gani na vigezo vipi vilitumika? naanza kuhisi humu kumekua na waongo wengi siku hizi
 
Ile ya muhimbili ni mnyoo (una historia yake na research, kasome) sio nyoka,,

Ila machame hospital nliona wanatumia nyoka na fimbo- hii nahis inahusiana na biblia

Kuna ambapo wanatumia symbol ya mnyoo kwa maana ya matibabu ya Dracunculiasis (Guinea worm - Dracunculus medinensis), ambapo kijiti/sindano (hata kijiti cha kiberiti kwa mfano) hutumika kumtoa mnyoo na ni ugonjwa uliokuwepo miaka mingi sana na uliokuwa miongoni mwa magonjwa yaliyokuwa chimbuko la elimu ya utabibu. Historia hii nadhani wanafunzi wa Muhimbili wanaifahamu vizuri zaidi maana logo yao ina mnyoo kama ulivyosema.

Lakini maana halisi ya alama iliyoletwa na mleta mada au chimbuko la hata hiyo alama ya Muhimbili (kijiti/sindano na mnyoo) ni historia ya god Asclepius ambaye alama yake ndiyo hiyo ya Rod of Asclepius. Kwa kilatini "Drancunculiasis medinensis" maana yake ni "little dragon from Medina" au "joka mdogo toka Medina", ambapo hilo jina lilikuja baadae sana tangu alama ya Rod of Asclepius ianze kutumika. Kwa enzi hizo jina la mnyoo lilipotungwa, mji wa Medina (kwa wakati huo Medina ilikuwa na watu wengi na mji maarufu na ni mji muhimu sana mpaka leo kwa Waislam) ulikuwa na wagonjwa wengi sana wa hii minyoo. Miaka mingi kabla yake, inasemekana kuwa hata ile hadithi ya Musa kuhusu nyoka ulikuwa unaongelewa huu mnyoo uliokuwa unasumbua sana wakati huo maeneo ya Egypt/Mesopotamia, na wala si nyoka tumdhaniaye leo. Baadae ulisumbua sana Africa ya magharibi ndio kwa kiingereza ukaanza kuitwa Guinea worm.
 
Mkuu Hayo maelezo ya huyo Dr hukumuuliza sasa mnyoo ukifuata fimbo ndo inakuaje labda

Hii style ya kutibu kwa kufuata fimbo/kijiti au kitu kinachofanana ni hivyo, ni kwa ajili ya kumviringisha huyo mnyoo wakati wa kumtoa kwa sababu ni mnyoo mrefu. Hebu angalia hii video hapa chini:

Kuna ambapo wanatumia symbol ya mnyoo kwa maana ya matibabu ya Dracunculiasis (Guinea worm - Dracunculus medinensis), ambapo kijiti/sindano (hata kijiti cha kiberiti kwa mfano) hutumika kumtoa mnyoo na ni ugonjwa uliokuwepo miaka mingi sana na uliokuwa miongoni mwa magonjwa yaliyokuwa chimbuko la elimu ya utabibu. Historia hii nadhani wanafunzi wa Muhimbili wanaifahamu vizuri zaidi maana logo yao ina mnyoo kama ulivyosema.

Lakini maana halisi ya alama iliyoletwa na mleta mada au chimbuko la hata hiyo alama ya Muhimbili (kijiti/sindano na mnyoo) ni historia ya god Asclepius ambaye alama yake ndiyo hiyo ya Rod of Asclepius. Kwa kilatini "Drancunculiasis medinensis" maana yake ni "little dragon from Medina" au "joka mdogo toka Medina", ambapo hilo jina lilikuja baadae sana tangu alama ya Rod of Asclepius ianze kutumika. Kwa enzi hizo jina la mnyoo lilipotungwa, mji wa Medina (kwa wakati huo Medina ilikuwa na watu wengi na mji maarufu na ni mji muhimu sana mpaka leo kwa Waislam) ulikuwa na wagonjwa wengi sana wa hii minyoo. Miaka mingi kabla yake, inasemekana kuwa hata ile hadithi ya Musa kuhusu nyoka ulikuwa unaongelewa huu mnyoo uliokuwa unasumbua sana wakati huo maeneo ya Egypt/Mesopotamia, na wala si nyoka tumdhaniaye leo. Baadae ulisumbua sana Africa ya magharibi ndio kwa kiingereza ukaanza kuitwa Guinea worm.
ndo huo mnyoo ulikuwa unawang'ata wana israel na kufa?
 
Hili swala ni kama lina maelezo ya aina mbili, au tatu tofauti, ila cha msingi ni kuwa imeanzia huko enzi za wahenga wa Kigiriki....kama ni mfuatiliaji wa mambo ya kale utagundua kuwa Wazungu wana mambo mengi sana wanayopenda ku refer na enzi za kigiriki 'ancient greek mythology'...na sio kwenye tiba pekee.

NYOKA...kuna wanaoamini kuwa kwa kuwa Nyoka ndiye kiumbe ambaye ana uwezo wa kujivua gamba, basi lile zoezi huchukuliwa kama kujihuisha...hivyo wanalinganisha na tiba ambayo humrudishia Mgonjwa upya/afya yake...na hiyo fimbo ilikuwa ikibebwa na tabibu (Asclepius).

Pia kwa kuwa Nyoka wana sumu inayoua (baadhi yao), alama yake wanaitumia kama kuonyesha kwamba wao (matabibu) wanaweza kukuponya hata kama umeumwa na Nyoka mwenye sumu kali.

MNYOO...Moja ya tiba za awali ilikuwa kumuondoa mwilini Mnyoo kwa njia ya kukata ngozi sehemu na kumvuta kwa kutumia fimbo, kwa namna ya ku roll mpaka anatoka wote.
 
ndo huo mnyoo ulikuwa unawang'ata wana israel na kufa?
Bahati mbaya sana, hilo swali halina jibu moja au la uhakika. Baadhi ya wanazuoni/waamini na wasioamini dini wanaamini ni huyo mnyoo ndiye alikuwa anaongelewa kwenye kitabu hicho cha Biblia. Kuna maswali mengine magumu/muhimu zaidi ya kuwa kwa nini ni nyoka au mnyoo au mnyama mwingine yeyote na kwanini Mungu alitoa tiba badala ya kinga. Biblia haijatoa majibu. Kwa muda wako, soma hapa na tafakari: SAB, God's Fiery Serpents
 
Sio alama ya nyoka tu, bali huyo nyoka anaonekana kama amewekwa sambamba na fimbo.
Mkuu hiyo ni ishara ya uponyaji na hiyo inatokana na historia ya Musa,
kama ulikuwa haujui basi katika nyakati za nabii Musa kuna kipindi wana wa israel walidhihaki Mungu sasa Mungu akachukia na kuwapa adhabu ya kung'atwa na nyoka, na ilikuwa kwa yoyote yule atakayeng'atwa na hao nyoka basi anafariki, Katika kipindi hiko walikufa watu wengi sana!
Maelfu kwa maelfu,
ndipo hatimae wakasurender na kuanza kumlilia Musa ili aongee na Mungu kusudi awaondoshee ile adhabu,
Ndipo sasa Mungu akamwambia Musa, chukua Fimbo yako kisha uisimamishe pahali penye muinuko, na yeyote atakayeng'atwa na nyoka na akaitazama hiyo fimbo basi atapona papohapo...!
Na ikawa kweli kila aliyeitazama ile fimbo alipona na hakufa, na tangu hapo sasa Mti ukapata sifa ya uponyaji na ukatumika sana kwenye matibabu ya kawaida,
Na ndomana unaona mpaka leo hiyo alama inatumika kuashiria uponyaji, na pia taasisi za afya zanatumia rangi ya kijani katika mavazi na nembo zao ili kuuwakilisha ule mti wa uponyaji (refer dawa nyingi zinatokana na mimea)
.
.
Kwahiyo Nyoka & Fimbo kuwekwa kwenye nembo za vituo vya matibabu na taasisi za afya ni ile ishara ya kumpa matumaini mgonjwa kwamba sasa anakaribia kupona(ndomana maranyingi zinaweka getini au mlangoni pa kuingilia)
Asante mkuu ubarikiwe sana
 
Kama asipo elewa hapa basi hatakuja elewa popote duniani.
 
Hiyo inaitwa the staff of wisdom miungu ya kale kama hermes anaonekana akiwa ameishika hii fimbo.
Hii ni miongoni mwa symbol ambazo tunaziita allegories.Hizi alama huwa ziko on plain sight lakini kuna truths behind them. Kuna nadharia zinafichwa behind hizi allegories.
Mysteries au secret societies kama freemasonry huwa hutumia hizi allegories kukufumba usiye mason usijue falsafa zao hivo hizi ni symbolic philosophy.
In reality hii symbol ya fimbo iliyokuwa coiled na snake imekuwa originated from ancient mysyeries.
Ukisoma kuhusu mystery religions especially greek mystery rekigions unaweza kupata mwanga.
Hiyo alama pia ipo kwenye noti yetu ya shilingi 500
 
Sio alama ya nyoka tu, bali huyo nyoka anaonekana kama amewekwa sambamba na fimbo.
Mkuu hiyo ni ishara ya uponyaji na hiyo inatokana na historia ya Musa,
kama ulikuwa haujui basi katika nyakati za nabii Musa kuna kipindi wana wa israel walidhihaki Mungu sasa Mungu akachukia na kuwapa adhabu ya kung'atwa na nyoka, na ilikuwa kwa yoyote yule atakayeng'atwa na hao nyoka basi anafariki, Katika kipindi hiko walikufa watu wengi sana!
Maelfu kwa maelfu,
ndipo hatimae wakasurender na kuanza kumlilia Musa ili aongee na Mungu kusudi awaondoshee ile adhabu,
Ndipo sasa Mungu akamwambia Musa, chukua Fimbo yako kisha uisimamishe pahali penye muinuko, na yeyote atakayeng'atwa na nyoka na akaitazama hiyo fimbo basi atapona papohapo...!
Na ikawa kweli kila aliyeitazama ile fimbo alipona na hakufa, na tangu hapo sasa Mti ukapata sifa ya uponyaji na ukatumika sana kwenye matibabu ya kawaida,
Na ndomana unaona mpaka leo hiyo alama inatumika kuashiria uponyaji, na pia taasisi za afya zanatumia rangi ya kijani katika mavazi na nembo zao ili kuuwakilisha ule mti wa uponyaji (refer dawa nyingi zinatokana na mimea)
.
.
Kwahiyo Nyoka & Fimbo kuwekwa kwenye nembo za vituo vya matibabu na taasisi za afya ni ile ishara ya kumpa matumaini mgonjwa kwamba sasa anakaribia kupona(ndomana maranyingi zinaweka getini au mlangoni pa kuingilia)
umeeleza vizuri lakini alikuwa nyoka wa kutengeneza wa shaba na haikuwa fimbo ya Mussa.
asante kwa kutusaidia
 
Back
Top Bottom