Kwanini hospitali zina mchoro na picha ya nyoka?

swahiba Senior

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
2,478
3,624
Habari zenu wana Jamvi.

Nimefuatilia sana hili suala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.

Sasa kwanini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi Ahsanteni​

IMG_20170426_152949.jpg
 
Sio alama ya nyoka tu, bali huyo nyoka anaonekana kama amewekwa sambamba na fimbo.
Mkuu hiyo ni ishara ya uponyaji na hiyo inatokana na historia ya Musa,
kama ulikuwa haujui basi katika nyakati za nabii Musa kuna kipindi wana wa israel walidhihaki Mungu sasa Mungu akachukia na kuwapa adhabu ya kung'atwa na nyoka, na ilikuwa kwa yoyote yule atakayeng'atwa na hao nyoka basi anafariki, Katika kipindi hiko walikufa watu wengi sana!
Maelfu kwa maelfu,
ndipo hatimae wakasurender na kuanza kumlilia Musa ili aongee na Mungu kusudi awaondoshee ile adhabu,
Ndipo sasa Mungu akamwambia Musa, chukua Fimbo yako kisha uisimamishe pahali penye muinuko, na yeyote atakayeng'atwa na nyoka na akaitazama hiyo fimbo basi atapona papohapo...!
Na ikawa kweli kila aliyeitazama ile fimbo alipona na hakufa, na tangu hapo sasa Mti ukapata sifa ya uponyaji na ukatumika sana kwenye matibabu ya kawaida,
Na ndomana unaona mpaka leo hiyo alama inatumika kuashiria uponyaji, na pia taasisi za afya zanatumia rangi ya kijani katika mavazi na nembo zao ili kuuwakilisha ule mti wa uponyaji (refer dawa nyingi zinatokana na mimea)
.
.
Kwahiyo Nyoka & Fimbo kuwekwa kwenye nembo za vituo vya matibabu na taasisi za afya ni ile ishara ya kumpa matumaini mgonjwa kwamba sasa anakaribia kupona(ndomana maranyingi zinaweka getini au mlangoni pa kuingilia)
 
Safi sana kwa ufafanuzi mzuri na wenye mantiki ama kweli jf ni kisima cha marifa
 
Pia katika historia ya binadamu inaonyesha katika viumbe vya porini ni nyoka ndio mwenye utambuzi wa miti au mimea ambayo ni dawa.

Mathalani nyoka akipata kadhia ya majeraha yanayiweza mpotezea uhai wake aidha yeye au wenzake hutafuta miti au majani ambayo ni dawa na kujitibu au kumtibu nyoka mwenzao.

Pia kama mdau alivyosema hapo juu, ukisoma biblia fresh, historia ya waizraeli kuna kipindi walipona kwa kumuangalia nyoka wa shaba aliewekwa kwenye fimbo ya musa kama sikosei, hivyo walipohingwa nyoka tu, wakiangalia hiyo fimbo walipona.
 
Habari zenu wana Jamvi.
Nimefuatilia sana hili swala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.sasa kwa nini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi AhsanteniView attachment 501467
Sio nyoka ni myoo, huko nyuma sana ulitokea ugonjwa ambapo minyoo ilisambaa katika mwili wa binadamu, so hakukuwa na tiba yake, so ilitumika sindano kuchoma kwenye sehem myoo ulipo mwilini, ndo ikawa tiba ya kuua, ndio ikachukuliwa kama Alama ya Afya mnyooo na sindano
 
Habari zenu wana Jamvi.
Nimefuatilia sana hili swala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.sasa kwa nini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi AhsanteniView attachment 501467

Hii alama ina historia ndefu na ya kusisimua, hasa ukifuatilia historia za wanaohusishwa na alama yenyewe. Asili yake imetokana hasa kutokana na mungu wa Kigiriki anayeitwa Asclepius, lakini inahusishwa pia na hadithi ya Musa kwenye Biblia. Ipo hivi:

1. Fimbo ya Asclepius (Rod/staff of Asclepius)

Kwa mujibu wa hadithi na imani za wagiriki (Greek mythology), mungu Asclepius alikuwa anashika fimbo kama hiyo yenye nyoka. Mungu huyu ndiye anayehusika na uponyaji/dawa/udaktari. Ni alama ambayo imekuwa inatumika muda mrefu sana na inatambulika vizuri na yeyote aliyesomea udaktari/uuguzi. Alama hii ipo pia kwenye bendera ya World Health Organization (WHO).

320px-Flag_of_WHO.svg.png

Mwanzoni mwa miaka ya 1900, jeshi la Marekani likaanza kutumia alama nyingine yenye nyoka wawili, fimbo/fito na mbawa juu, ambayo imekuwa ikitumika kimakosa (Caduceus, angalia hapa chini). Caduceus ina maana tofauti kabisa na hii ya nyoka mmoja. Caduceus ni alama ambayo asili yake ni mungu Hermes (ugiriki), ambaye yeye alikuwa anahusishwa zaidi na uwakala wa miungu na muunganishi wa ulimwengu wa wafu/roho. Hermes anafahamika zaidi kwa huo uwezo wake wa kuingia na kutoka kwenye ulimwengu wa roho/wafu na kusaidia wale wanaokata roho au wanaotaka kufa waingie kwenye ulimwengu wa wafu/roho bila shida pamoja na mambo mengine mengi. Alikuwa anafahamika pia kwa mambo mengi, ikiwemo udanganyifu wa kujibadilisha ili kuwazuga miungu wenzie ilimradi tu afurahi mwenyewe. Baadae, Warumi walimuhusisha Hermes pamoja na hiyo alama yake na mungu Mercury, ambaye alikuwa ana tabia za kufanana. Kwa hiyo, popote utakapoona hii alama ya Caduceus inatumika na taasisi ya tiba, jua kuwa hawajasoma historia vizuri.

Alama zenyewe hizi hapa:

snakesformedicine.png

Sanamu ya mungu Ascelipus:
256px-_Asklepios_-_Statue_Epidauros_Museum_2008-0.jpg

Sanamu ya Mungu Hermes:
219px-_Hermes_Ingenui_Pio-_Clementino_Inv544.jpg

2. Hadithi ya Musa kwenye Biblia, kitabu cha Hesabu, mlango 21, mstari wa 4 hadi wa 9:
4. Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. 5. Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6. BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. 7. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. 8. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Nadhani hiyo ya hadithi ya Musa kwenye Biblia inajieleza vya kutosha.
 
Back
Top Bottom