Jinsi nilivyonusurika kung'atwa na nyoka wakati nataka kumuokoa

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,627
106,588
Kwasababu zangu binafsi ambazo sitapenda niziseme (but very reasonable) hua siui kiumbe yoyote aliye hai tofauti na mbu. Kiukweli siwapendi na nawaogopa sana nyoka ila hata wao imekua ikiniwea vigumu kuwaua hivyo pindi napokutana nao hua naishia kuwafukuza au kuwapotezea kama wameenda eneo ambalo mimi sifiki au watu wengine.

Sehemu Fulani nilipokua nakaa kulikua na kisima kisicho na maji humo ndani kuna nyoka alikua akishi humo hadi akawa na watoto kwakweli iliniwea vigumu kumuua japo wananchi weye hasira kali walikuja wakateketeza ile familia, Fast-forwarding

Siku moja natembea barabarani usiku nikakutana na nyoka mdogo yupo katikati ya barabara kashindwa kuvuka ajili ya mwanga wa maloli yaliyokua yanapita, mimi nikaenda kwa nia njema kabisa nimsaidie avuke upande wa pili cha ajabu nilipomfikia akainua kichwa juu anaigonge/ng’ate, nikawa namkwepa. Kila nikimfukuza aende upande wa pili anakua ananijia aning’ate kwakweli nikashindwa kumsaidia ikabidi nimuache roli likamgonga. Iliniuma kiasi maana nilikua nina nafasi ya kumsaidia ila nilishindwa.

Unadhani kwanini japo nia yangu ilikua ni njema kumsaidia maisha yake lakini aliniona adui na kutaka kunigonga?

Kwa mujibu wa biblia baada ya wanadamu wa kwanza kufanya maasi Mungu alitoa laana kati ya nyoka na mwanadamu kwa kusema “name nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” kwa mantiki hiyo watu wengi huchukulia kwamba hiyo laana aliyotoa Mungu kati ya binaadamu na nyoka ndio inafanya mwanadamu na nyoka waviziane kumuua mwingine lakini mimi nasema hiyo sio kweli laana hiyo aliotoa Mungu sio sababu bali ilitumika kama fumbo. Maana kubwa aliyomaanisha mungu ni kwamba ujuzi wa mema na mabaya walioupata wanadamu kwa kula tunda/kuasi ndio unaofanya mwanadamu na nyoka wawindane….nitajaribu kulielezea hili kisayansi zaid ili nieleweke vizuri.

Catecholamines

Endocrine Glands
ni mfumo wa tezi ambao wenyewe hutoa hutoa homoni moja kwa moja kwenda kwenye mfumo/mzunguko wa damu wa damu. Adrenal Gland ni tezi iliyopo katika mfumo watezi ambayo inapatikana juu ya mafigo kazi kuu ya tezi hii ni kuweka sawa kiwango cha chumvi na kurekebisha kiwango cha musukumo wa damu. tezi hii hutengeneza homoni mbali mbalimbali kama vile cortisol,epinephrine,catecholamine nk pia hutengeneza homoni ya adrenaline, adrenaline hutengenezwa pia katika medulla oblongata kwa kiwango kidogo

Pindi unapokua na hasira au unapoona kitu cha hatari kama vile nyoka tezi hii ya Adrenal hutoa homoni ya epinephrine, husababisha kutengenezwa kwa homoni ya cortisol, ambayo huongeza shinikizo la damu, sukari ya damu, na kukandamiza mfumo wa kinga.Mwitikio wa awali na miitikio inayofuata huchochewa katika jitihada za kuunda nyongeza ya nishati. Ongezeko hili la nishati huamlishwa na epinephrine kujifunga kwa seli za ini na uzalishaji unaofuata wa glucose.

NB: Adrenaline hufahamika pia kama Epinephrine

mzunguko wa cortisol hufanya kazi kugeuza asidi ya mafuta kuwa nishati inayopatikana, ambayo hutayarisha misuli ya mwili mzima kwa majibu/reaction. Homoni za catecholamine, kama vile adrenaline (epinephrine) au noradrenalini (norepinephrine), husaidia reaction ya haraka ya mwili ambayo huhusiana na maandalizi ya misuli kuchukua hatua kali…..Misuli inapofikia hatua hiyo unapofikia katika hatua hiyo moyo na mapafu huongezeka kasi yaani mapigo ya moyo yataenda haraka na mtu mtu atakua anapumua haraka, huziwia tezi ya Lacrimal ambayo hufanya kazi ya kuzalisha machozi na mate ndio maana ukiwa umeona kitu cha hatari mate na koo hukauka…pia kutetemeka mwili. Baada ya haya yote kutokea mwili ndio mwanadamu ataamua akimbie hatari(flight) au apambane na hatari(fight.
images (69).jpeg


Vomeronasal organ (VNO) ni sehemu/mlango/sense organi ya ziada iliyopo juu ndani yam domo kwa juu ambayo hutumika katika kunusa mara nyingi organ hii hupatikana zaidi katika nyoka na mijusi. VNO wa jina lingine inaitwa Jacobson Gland. Katika nyoka Tezi hii ya VNO ina uwezo mkubwa sana wa kunusa Scent za vitu….Kama nilivyoelezea huko juu kwamba mwanada mu ukiona kitu cha kutisha Adreanal Gland ina activate reaction ya Fight or Flight kumbuka kwamba mwili ukishakua kwenye reaction hiyo hormone mbalimbali zinazoachiliwa (Adrenaline) zinasambaa katika damu yako hivyo basi nyoka kwa kutumia tezi ya VNO/Jacobson gland huweza kuunusa mwili wako na kugundua kwamba mtu huyu ni adaui kwangu nae atajihmi maana atakusikia harafu yako ni tofauti ajili ya hormones hizo.
images (65).jpeg

Mwanzo kwenye mada nimeeleza nilivyotaka kung’atwa na nyoka nikiwa nataka kumsaidia sababu ni kwamba alisikia scent ya mwili wangu iliyotokana na homoni mbalimbali zilizoachiliwa katika kutekeleza reaction ya fight or flight….Kawaida ya nyoka kama yupo ndani usipomuona wala kumkanyaga hawezi kukudhuru kabisa lakini pindi utakapomuona tu basi naye atajitahidi ajihami kwani kama hujamuona mwali wako unakua upo sawa kabisa lakini pindi utakapomuona tu mwili wako utabadirika kwani utakua unajua ile ni hatari.

Kwa mantiki hiyo uadui uliopo kati ya nyoka na mwanadamu unatokana na ujuzi wetu wa kujua baya na jema kwani kujua nyoka huyu ni adui sio mwema ndio huactivate Adrenal gland kama tungekua hatujui jema na baya basi kamwe tusingekua na uadui na nyoka ndio maana mtoto mdogo chini ya miaka miwili anaweza kucheza na nyoka mkali na asing’atwe kamwe lakini kama mama yake atatokea na kumuona mtoto akicheza na nyoka basi anaweza sababisha kweli nyoka akamng’ata mtoto maana mama anajua jema na baya so akimuona nyoka na mtoto ni lazima apige kelelemna wakati huo adrenaline itakua tayari ishasambaa mwilini nyoka ataisikia scent na kujua huyu ni adui kelele za mama zitamtia uoga mtoto kisha aanze kulia maana mtoto atahisi labda kuna hatari ndio maana mama yake anapiga kelele. Ile kuhisi hatari kwa mtoto nako ni adrenal nayo inakua inaanza kufanya kazi so hapo inakua ni utashi wa nyoka mwenyewe atakachoamua.
images (70).jpeg

Hivyo Yule nyoka japo mimi nilikua nina nia njema ya kumsaidia lakini nilimfuata mwili wangu ukiwa katika hali ya fight or flight kwani najua Yule ni mbaya kwangu hivyo nyoka hakuangalia dhamira yangu bali alifuata sense yake ya Jacobson gland.
….
Hii ni theory yang tu kutokana na uelewa wangu wasayansi inawezekana sipo sahihi hivyo basi ruhusa kwenu kunikosoa na kusahihisha pale nilipokosea

-Criston Cole
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom