Kwa nini hatuuzi TAZARA tukajua moja?

May 9, 2012
59
15
Hivi kuna mtu anayo CAG report ya Tazara inasemaje?

Nimedownload BBC video inayotwa African Railway

Ni aibu. Sasa kama serikali na pesa za walipa kodi zimeshindwa kuongeza ufanisi.

Watu wanafanya maintenance kwa kutumia zama za karne ya 18 hivi kweli watawala wetu wana nia na hii reli au?

halafu kuna tu amesema kwenye video kuwa maamuzi yote ya hatma ya Tazara yako Beijing. Je ni kweli haya?

sikiliza hapa:
http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-17060828
 
Unachanganya na reli ya kati

nazungumzia TAZARA sio hiyo reli ya kwenda kwetu Tabora

najua kama unazangumzia tazara.

Kutokana na Ukisoma heading yako ndo maana nimekuuliza hilo swali......

Maana, unatarajia nini kigeni cha mno tazara ikiuzwa? Unadhani huduma tatengemaa? Na sie tunaoenda mbingu kulima mpunga unadhani tutafikaje?


Bado nasisitiza usitarajie makubwa toka kwa hao wanaoitwa 'wawekezaji'
 
niliwahi kufanya kazi kwa muda mfupi TAZARA Dar es salaam,
jambo ambalo hadi leo linanishanganza shirika hilo tangu kuundwa kwake halijawahi kujinunulia kichwa cha kuendesha/KUVUTA mabehewa, Locomotives Engines, DAIMA LINAOMBA MSAADA TOKA CHINA.

Miaka yote ya biashara, shirika limekua likizalisha mamilionea mitaani , huku akaunti zake zikibaki wazi na umaskini mkubwa.
 
Utauzaje Tazara wakati deni na mkataba haujaisha na utaisha miaka 50 ijayo.
 
Tatizo la TAZARA ni muundo wake. Management ya TAZARA imegawanyika equally kwa Tanzania na Zambia. Positions zimetengwa ki nchi.
Wakati umefika kwa mfumo huu ubadilishwe. Watu wawe appointed kutoka kwenye market regardless utaifa wake na kazi hii ifanywe na reputable firm na serikali hizi mbili zikae mbali na utendaji wa shirika hili.
Pasiwe tena na regional office wenye muundo wa sasa hivi.
Hii yote itaweza kufanywa iwapo sheria ya kuunda TAZARA itafanyiwa marekebisho ASAP.
 
Matatizo ya usafiri wa reli nchini yanasababishwa na mgongano wa maslahi. wafanyabiashara wengi wa malori ya kusafirisha mizigo na mabasi ya kusafirisha abiria ni mawaziri na wabunge, usafiri wa treni ukiwa mzuri biashara zao zitadoda maana usafiri wa treni ni nafuu. kwa hiyo viongozi hao wanakosa nia ya dhati ya kuboresha usafiri wa reli.
 
Hivi kuna mtu anayo CAG report ya Tazara inasemaje?

Nimedownload BBC video inayotwa African Railway

Ni aibu. Sasa kama serikali na pesa za walipa kodi zimeshindwa kuongeza ufanisi.

Watu wanafanya maintenance kwa kutumia zama za karne ya 18 hivi kweli watawala wetu wana nia na hii reli au?

halafu kuna tu amesema kwenye video kuwa maamuzi yote ya hatma ya Tazara yako Beijing. Je ni kweli haya?

sikiliza hapa:
BBC News - China's track record on revamping African railways

Mafisadi wale wapi ikiuzwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom