Kwa nini CCM ikihofie CHADEMA?

Kwa nini CCM ikihofie CHADEMA?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741

TANGU kuanzishwa kwa vyama vingi nchini mwaka 1992, tayari chaguzi nne zinazoshirikisha vyama vingi zimefanyika.

Katika chaguzi hizo nne, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kushika dola kwa ushindi wa kishindo katika kiti cha urais, wabunge na madiwani.

Ushindi huu wa kishindo umeendelea kupungua kutoka ngazi ya ubunge na udiwani, ambapo wapinzani wamekuwa wakinyakua viti vya majimbo hata ambavyo vilikuwa vinatajwa kuwa ngome ya CCM.

Kupungua huko kwa viti vya ubunge na udiwani, ni kiashiria kuwahuenda kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini, CCM itaenda katika uchaguzi mkuu mwaka 2015, kikiwa hakina uhakika wa kushinda.

Wapinzani wakuu wa CCM ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambacho kinashikilia rekodi ya pili kwa kuwa na viti vingi vya ubunge na udiwani nyuma ya CCM.

Nafasi ya ushindi katika uchaguzi huo, hasa katika ngazi ya urais imekumbwa na changamoto nyingi.

Wakati CCM imetimiza miaka 36 tangu kuzaliwa kwake, Chadema ina miaka 21 ambapo ndani ya miaka mitano kimeweza kujipambanua kwa Watanzania kama chama chenye sera madhubuti kinachotazamia kuchukua dola mwaka 2015.

Kwa nini CCM ikihofie Chadema na si vyama vingine? Ni mipango na mikakati ya muda mrefu, baada ya kuusoma mchezo wa CCM na kutumia udhaifu wake kujijenga.

CCM imewasahau wananchi wa kawaida na kukumbatia matajiri, Chadema ikaona hao ndio wanafaa na kuwafanya mtaji wao.

Ni ukweli ulio wazi kuwa mtaji wa chama chochote kile ni watu ambao ni wanachama hai.

Kitendo cha Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa wiki iliyopita mkoani Arusha, ni hatua kubwa waliyopiga ambayo imekifanya chama hicho kufikisha idadi ya viti 15 kwenye Baraza la Madiwani, wakati CCM kimebakiwa kuwa na viti 12.

Mbio za Chadema kuifukuzia dola kwa kusimama na miguu yake yenyewe katika uchaguzi mkuu wa tatu ulioshirikisha vyama vingi mwaka 2005, baada ya kuwa msindikizaji kwa mihula miwili ambapo ilimsimamisha Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wakati CCM ilimsimamisha Rais Jakaya Kikwete kwa mara ya kwanza.

Katika uchaguzi wa kwanza wa mwaka 1995, Chadema ilishiriki uchaguzi huo bila ya kuweka mgombea urais, ambapo walikubaliana kumuunga mkono mgombea wa chama cha NCCR-Mageuzi, Augustino Mrema ambaye alikuwa anakubalika sana wakati huo.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, Chadema ilishiriki tena uchaguzi huo kama mwanzo bila kusimamisha mgombea urais na safari hii ushirika ulihamia kwa CUF ambapo walimuunga mkono mgombea wake, Profesa Ibrahim Lipumba.

Mwaka huo, Chadema kilipata asilimia tatu ya kura za wabunge na jumla ya wabunge wanne na kushika nafasi ya nne katika vyama vya upinzani baada ya vyama vya CUF, TLP na UDP.

Baada ya kuchoka kuwa msindikizaji, Chadema ilijisuka upya na kumsimamisha Mbowe, ambaye alishindwa katika uchaguzi huo na hiyo ikawa kama changamoto kwa Chadema.

Chadema wakati huo ikaona ni wakati muafaka kujipambanua kwa wananchi, ambapo ilijieneza nchi nzima hata sehemu ambazo ilikuwa haikubaliki na kuvuna wanachama wengi zaidi.

Katika miaka yote hiyo CCM ilikuwa inaingia kwenye uchaguzi ikiwa na uhakika wa asilimia nyingi tu ya kushinda urais na viti vingi vya ubunge na udiwani bila kuhofia vyama vya upinzani.

Imani hii ya ushindi wa kishindo, inaanza kuyeyuka taratibu baada ya mwaka 2010, Chadema kupata viti vingi vya ubunge na udiwani hata katika majimbo ambayo yalikuwa ngome ya CCM.

Hofu ya kupoteza viti vingi vya ubunge na udiwani si hofu pekee inayoikabili CCM, bali pia inahofia kiti cha urais, haina uhakika nacho.

Tofauti kati ya Chadema na CCM baada ya uchaguzi ni kwamba, CCM hubweteka kwa madai ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi, lakini Chadema wao huchochea moto kwa kufanya mikutano mikoani yenye kauli mbiu za kuvutia kwa wananchi wanaopenda kusikia wanayotaka kusikia.

Mikutano hii imesaidia kuizindua CCM, ambapo nao hutembea mikoa iliyopitiwa na Chadema kujitakasa na kukanusha baadhi ya mambo baada ya jina lake kutiwa doa na Chadema.

Chadema imekuwa ikifanya mavuno katika vyuo vikuu mbalimbali pamoja na kuongeza idadi ya wanachama wanaotoka vyama vingine, wengi wao wakiwa viongozi.

CCM imekuwa ikifanya hivyo, lakini sasa ni kama imejisahau na inaanza upya ilipoishia.

Kujisahau huko kwa CCM kumeipaisha Chadema ambapo sasa ni vigumu kwa kijana wa kawaida kumueleza mambo hasi kuhusu Chadema.

Hii ni changamoto kwa CCM kushtuka na kuwakumbuka wananchi ambao kila uchao wanalalamikia ugumu wa maisha umeletwa na chama hicho.

Ni changamoto pia kwa Chadema kutobweteka kwa kuridhika na mafanikio madogo waliyo nayo.

KWA NINI CCM IKIHOFIE CHADEMA?? - MPEKUZI HURU
 
Kwa kweli hawa jamaa wamejipanga vizuri na ni tishio kubwa sana kwa CCM!
Mkuu TUKUTUKU Hivi vyama vya kisiasa vya Kibongoo vimeamuwa kuanzisha Vikundi vya wanamgambo wa vyama kulikoni? Utafikiri Tanzania hakuna

jeshi la Polisi au Jeshi la wananchi? Majangaa hayo Majangaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Tanzania kwa miaka inayokuja mbele itakuwa kama Lebanon

kutakuwa na Vikundi vingi vya wanamgambo, Natabiri WaKristo nao Wataanzisha Vikundi vyao vya Wanamgambo na Wa-islam nao pia

Wataanzisha Vikundi vyao basi kutakuwa Tanzania hakukaliki kila sehemu kuna vikundi vyenye silaha. Hivyo ndivyo alivyo tuachia Urithi

wa nchi yetu yenye Maziwa Makuu Baba wa taifa Mwalimu Nyerere?
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...
 
Mkuu ZeMarcopolo CCM Tangu ishike Madaraka kwa kuanza mfumo wa vyama vingi kuna maendeleo ya aina gani mpaka sasa hakuna Maji safi Mijini mpaka vijijini? Hakuna umeme Mijini mpaka Vijijini? Umasikini umeota Mizizi nchini Tanzania. Mafisadi wanajilimbikiza Mabillioni ya pesa nchi za nje? Rushwa kila mahali nchini Tanzania kuna kipya gani walichofanya hao CCM? Zaidi ya kuididimiza nchi yetu? Dr .ZeMarcopolo
 
Piga tathmini tokea 1995 hadi sasa ccm imepoteza au kuoengeza majimbo mangapi?siku hazigandi.
 
Kwa hali ilipofikia ni CDM tu ndio inayosababisha Wananchi na Vijana watulie kwa Matumaini kwamba Mwaka 2015 watairudisha Nchi yao kwa Wenyenchi.CDM Inawapa Matumaini yenye kuwatuliza na Kuwafariji.Kwa sasa Wananchi wamepoteza Matumaini kabisa na Serikali ya CCM na wanajiona Mateka katika Nchi yao Wenyewe.Hata Viongozi wa Serikali ya CCM wanakwapua kwa kasi wakishirikiana na Makampuni ya Kigeni kwa sababu hawana Uhakika wa kuendelea kutawala.
 
Polisi wetu hawana weledi (they lack professionalism) wameshindwa kusimamia haki, wamekuwa ni wahalifu na ni hatari zaidi ya magaidi.
Wamepoteza imani na wananchi, na wanatumia silaha za moto zilizo nunuliwa kwa kodi zetu kutumaliza.
Angalia yaliyomkuta bwana Mwangosi Iringa, angalia jinsi polisi walivyohusika moja kwa moja na ulipuaji bomu Arusha.
Kwa misingi hii naiunga mkono CHADEMA waanzishe kundi la kujilinda, maana walinzi wetu wamekuwa si walinzi tena, ila washambuliaji wetu
Mkuu TUKUTUKU Hivi vyama vya kisiasa vya Kibongoo vimeamuwa kuanzisha Vikundi vya wanamgambo wa vyama kulikoni? Utafikiri Tanzania hakuna

jeshi la Polisi au Jeshi la wananchi? Majangaa hayo Majangaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Tanzania kwa miaka inayokuja mbele itakuwa kama Lebanon

kutakuwa na Vikundi vingi vya wanamgambo, Natabiri WaKristo nao Wataanzisha Vikundi vyao vya Wanamgambo na Wa-islam nao pia

Wataanzisha Vikundi vyao basi kutakuwa Tanzania hakukaliki kila sehemu kuna vikundi vyenye silaha. Hivyo ndivyo alivyo tuachia Urithi

wa nchi yetu yenye Maziwa Makuu Baba wa taifa Mwalimu Nyerere?
 
Wahenga walisema hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, wakaongeza kwamba mbio za panya huishia sakafuni kisha wakasiriba zaidi wakidai hakuna bingwa wa milele.Bila shaka yaliyonenwa na wahenga yameanza kutimia!
 
Mungu yuko upande wa wanaodhulumiwa na shetani yuko upande wa wanaojifanya miunguwatu

"WAPIGE TUMECHOKA"
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

FYI chama chako cha CCM kililazimika tu kuukaribisha ujiio wa vyama vingi na haikuwa hiyari yao!
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...

Hapa ndipo ccm inapojisahau, miaka 20 ya kushika dola sawa, ila umesahau kuwa mmekuwepo japo kwa majina tofauti tofauti tangu uumbaji wa tanzania? umesahau kuwa uanzishwaji wa vyama vya upinzani haukuambatana na ugawanyaji wa rasilimali ambazo zilivunwa kwa ushirikiano, bali vyama vya upinzani vimeachwa vijijenge vyenyewe kuanzia sifuri?
 
Vijana wanawapa ugonjwa wa moyo CCM na ndo watakaounda zaidi ya 60% ya wapiga kura wote Tanzania hapo 2015.Ndio mtaji wa CHADEMA huo.
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...
Points of correction:
1;CCM haikuruhusu mfumo wa vyama vingi kwa matakwa yake.mfumo huu ni matokeo ya presha za wenye Dunia kama World bank na IMF.
2;Anguko la USSR pialilikuwa sababu tosha ya CCM kukubali kwa shingo upande mfumo huu.;
3;Uwepo wa demokrasia ya vyama vingi nchini sio favour ys CCM kwa watanzania.Ni haki ya kimsingi kabisa ya watanzania.
4;Lack of civic education kwa Watanzania walio wengi ndiko kulipoipa CCM nafasi ya kuongoza kwa muda huu na wala sio sera nzuri au utekelezaji uliotukuka wa sera hizo.Awareness inaongezeka kwa kasi na watanzania wengi wanajua haki zao....hili ni tishio kubwa kwa CCM.Strategically,miji ya Mwanza,Mbeya,Arusha na baadhi ya majimbo ya Dar kwenda upinzani ni indicator mbaya kwa CCM.
5;Tatizo kubwa la CCM hawana "Think Tank" inayowasaidia kupambana na changamoto na hoja za wapinzani.Ndio maana matumizi ya nguvu na majibu hatari ambayo ni very emotional wanayatoa kila kukicha (Mfano...a)"Na nasema wapigwe tu maana tumechoka sasa;b)"Liwalo na liwe";c)"siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa";d)f@**k you";e)"Ndiyoooooooooooooo".Katibu Mkuu ndio mtendaji mkuu wa chama.Infact katibu mkuu ndio injini ya chama.CCM ilibugi sana kuweka makatibu wakuu wapiga domo kama Makamba na Mukama by then.Hawa hawakuwa caliber ya Dr Wilbrod Slaa/Maalim Seif!Kimkakati walipigwa bao sana wakati ule.CCM inahitaji "a super think tank".sii hawa akina Nape,Mwigulu,Shonza and the likes!....and I cant see that happening very soon...kwa sababu CCM ni rigid na ina-resist change kwa nguvu zote kuliko institution yoyote ninayoifahamu hapa duniani...hata Vatican haiopo hivyo.
 
Piga tathmini tokea 1995 hadi sasa ccm imepoteza au kuoengeza majimbo mangapi?siku hazigandi.

Wewe akili yako ni ya kiwango cha bavicha. Nchi yoyote yenye chama kimoja chama hicho kinakuwa na asilimia 100 ya majimbo. Unapokuja mfumo wa vyama vingi ni LAZIMA majimbo hayo yapungue. Kwa vile wapinzani wako wengi basi walitakiwa kuwa na angalau asilimia 60 ya majimbo na CCM ibaki na asilimia 40. Hivi sasa CCM ina asilimia 70 ya majimbo. Kama akili yako ya bavicha inakudanganya kuwa CCM ni chama dhaifu basi tafuta mtu anayejua hesabu akufundishe tuition ili ujue kuwa CCM inashindana na vyama zaidi ya 10 na imefanikiwa kuwa juu kwa mbali sana kwa robo karne.
 
Hapa ndipo ccm inapojisahau, miaka 20 ya kushika dola sawa, ila umesahau kuwa mmekuwepo japo kwa majina tofauti tofauti tangu uumbaji wa tanzania? umesahau kuwa uanzishwaji wa vyama vya upinzani haukuambatana na ugawanyaji wa rasilimali ambazo zilivunwa kwa ushirikiano, bali vyama vya upinzani vimeachwa vijijenge vyenyewe kuanzia sifuri?

Viongozi wa vyama vya upinzani wanawalaghai wananchi kuwa wanaweza kuboresha maisha ya wananchi haraka haraka. Lakini wao kwa robo karne wameshindwa hata kuitoa CCM madarakani. Je, ipi ni kazi ngumu, kuboresha maisha ya watu au kuitoa CCM madarakani?
 
Mkuu ZeMarcopolo CCM Tangu ishike Madaraka kwa kuanza mfumo wa vyama vingi kuna maendeleo ya aina gani mpaka sasa hakuna Maji safi Mijini mpaka vijijini? Hakuna umeme Mijini mpaka Vijijini? Umasikini umeota Mizizi nchini Tanzania. Mafisadi wanajilimbikiza Mabillioni ya pesa nchi za nje? Rushwa kila mahali nchini Tanzania kuna kipya gani walichofanya hao CCM? Zaidi ya kuididimiza nchi yetu? Dr .ZeMarcopolo

Nchi yetu ina fursa nyingi sana. Kila mwenye macho anaziona na kila mwenye akili ananufaika nazo.
Wapo watu wamekaa chini ya kivuli na vibarazani wanagoja siku kije chama fulani kuboresha maisha yao. Watu hao ni kama vile wamejiingiza kwenye puto la disappointment, its just a matter of time kabla puto hilo halijapasuka.

Kwa mtanzania mwenye bidii, for personal progress, Tanzania has more opportunities than any Europen country can offer. Only USA can compete with Tanzania in terms of opportunies of personal progress.
 
Mkuu
TUKUTUKU
Hivi vyama vya kisiasa vya Kibongoo vimeamuwa kuanzisha Vikundi vya
wanamgambo wa vyama kulikoni? Utafikiri Tanzania hakuna

jeshi la Polisi au Jeshi la wananchi? Majangaa hayo
Majangaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Tanzania kwa miaka inayokuja mbele itakuwa
kama Lebanon

kutakuwa na Vikundi vingi vya wanamgambo, Natabiri WaKristo nao
Wataanzisha Vikundi vyao vya Wanamgambo na Wa-islam nao pia

Wataanzisha Vikundi vyao basi kutakuwa Tanzania hakukaliki kila sehemu
kuna vikundi vyenye silaha. Hivyo ndivyo alivyo tuachia Urithi

wa nchi yetu yenye Maziwa Makuu Baba wa taifa Mwalimu Nyerere?

Vikundi vitaanzishwa sana, na hii inatokana jeshi la polisi kushindwa kutimiza wajibu na kubaki kufanya kaz kwa maelekezo ya wanasiasa wa chama tawala! Polisi watende haki amani itakuwepo.
 
Back
Top Bottom