Kwa nini ahadi za chadema kipindi cha uchaguzi mkuu hazikuwa realistic? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ahadi za chadema kipindi cha uchaguzi mkuu hazikuwa realistic?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba la Nyoka, Dec 7, 2010.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  AHADI YA ELIMU BURE MPAKA FORM SIX NDANI YA MIAKA 5 , HUDUMA ZA AFYA BURE KWA WAZEE NA KUPUNGUZA BEI YA SEMENTI.

  Kwa muundo wa sasa wa nchi yetu, yaani serikali mbili hili jambo lingewezekana kabisa, kwa maana ya kudhibiti ufisadi na kuongeza mapato kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo hatuvitumii ipasavyo mfano madini yetu na rasilimali nyinginezo. Lakini, ifahamike pia kwamba ni Hoja ya Chadema kuwa na SERIKALI TATU, na muundo huu wa serikali yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ni gharama kubwa kiuendeshaji, kwa sababu resources nyingine lazima zitumike kuiendesha hii serikali mpya itakayoundwa, yaani hii serikali ya Tanganyika. Sasa katika hili ni dhahiri kiasi cha fedha cha kuweza kutoa huduma za jamii kitapelekwa katika mambo ya uendeshaji wa serikali mpya yaani ya Tanganyika na hivyo sioni ni kwa namna gani kungekuwa na resource za kutosha kutoa hiyo Elimu bure, Huduma za afya kwa wazee bure, na wakati huo huo kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi. Ifahamike kwamba nia ahadi ya Chadema ya kuwa na katiba mpya ndani ya miaka mitano, na kwa hiyo serikali ya Tanganyika labda ingeanza ndani ya kipindi hiki cha 2010-2015 au miaka ya mbele kutegemea mchakato wa katiba mpya ungemalizika lini.
   
 2. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Naomba evidence yeyote ya kuwa CDM waliahidi serikali tatu............. labda nilikuwa nyuma au mbali, so sikujua.... lakini KAMA HUNA... MIMI NDIO MJINGA HATA KUTHUBUTU KUANDIKA HAYA na kama ndio, BASI NAO WEHU TU.... bora kuwa na msimamo wa mtikila.......... LETA EVIDENCE PLEASE ... evidence... kinyume cha hapo HATA WEWE HAMNA KITU unasikia mambo ya CCM
   
 3. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu Heshima sana mzee
  Nadhani kusema tu kuwa ahadi zile hazikuwa realistic si sahihi kwa sababu hazijafanyiwa majaribio ya implementation popote na kushindwa. Suala la serikali tatu kama uliwasikiliza CDM vizuri utagundua kuwa walikusudia kufumua kabisa muundo wa Serikali wa sasa ikiwa ni pamoja na kufuta wakuu wa mikoa na wilaya, wanaokula shekeli zetu bila kazi za maana. Walikusudia kuwa na Serikali ya Muungano ndogo sana huku wakitumia mfumo wa decentralization katika kuwahudumia wananchi. Katika mazingira kama haya muundo wa Muungano lazima ungetazamwa upya na hivyo wazenji wangelazimika pia kuwa na serikali ndogo sio hiyo iliyopo sasa, unakuwa na Makamu wa rais wawili in a population of 1m for what.
  Kwa kuwa hawakupewa na nec ridhaa ya kuongoza acheni kuanza kusema kuwa ahadi zao hazikuwa realistic, ungewapa nchi washindwe implementation ya ahadi zao then tuhoji, lakini chochote tutakachojadili sasa kuhusu ahadi zile ni porojo tu! Tuna mambo mengi ya msingi kwa watawala walioaminiwa na nec mfano tatizo la mgao wa umeme kuwa sera ya kwanza kutekelezwa na mengine yanayokuja
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  CRAAAAAAAPU CRAAAAAAAPU.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. m

  mams JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kuna siku watapewa kuongoza nchi na hayo mnadhani siyo realistic yatathibitika kuwa realistic na hivyo jiandaeni kutafuta swhemu ya kuficha sura zenu kuwa baada ya hapo hamtakamata dola asilani.
   
Loading...