Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,023
- 9,285
AHADI YA ELIMU BURE MPAKA FORM SIX NDANI YA MIAKA 5 , HUDUMA ZA AFYA BURE KWA WAZEE NA KUPUNGUZA BEI YA SEMENTI.
Kwa muundo wa sasa wa nchi yetu, yaani serikali mbili hili jambo lingewezekana kabisa, kwa maana ya kudhibiti ufisadi na kuongeza mapato kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo hatuvitumii ipasavyo mfano madini yetu na rasilimali nyinginezo. Lakini, ifahamike pia kwamba ni Hoja ya Chadema kuwa na SERIKALI TATU, na muundo huu wa serikali yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Muungano ni gharama kubwa kiuendeshaji, kwa sababu resources nyingine lazima zitumike kuiendesha hii serikali mpya itakayoundwa, yaani hii serikali ya Tanganyika. Sasa katika hili ni dhahiri kiasi cha fedha cha kuweza kutoa huduma za jamii kitapelekwa katika mambo ya uendeshaji wa serikali mpya yaani ya Tanganyika na hivyo sioni ni kwa namna gani kungekuwa na resource za kutosha kutoa hiyo Elimu bure, Huduma za afya kwa wazee bure, na wakati huo huo kupunguza kodi katika vifaa vya ujenzi. Ifahamike kwamba nia ahadi ya Chadema ya kuwa na katiba mpya ndani ya miaka mitano, na kwa hiyo serikali ya Tanganyika labda ingeanza ndani ya kipindi hiki cha 2010-2015 au miaka ya mbele kutegemea mchakato wa katiba mpya ungemalizika lini.