Kwa namna yoyote ile CCM, na NEC wanastahili lawama katika hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa namna yoyote ile CCM, na NEC wanastahili lawama katika hili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by firstcollina, Nov 1, 2010.

 1. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika inauma sana kuona damu ikimwagika, tena ikimwagika bila hatia kwa sababu ambazo zinaweza kabisa kuzuilika. Ninalazimika kusema havyo kwa sababu ya yale yaliyotokea Tandika, Tarime, Mbeya, Mwanza, Na Loyola dar-es-salaam.

  • Hivi inawezekana vip, tukio kubwa kama uchaguzi ambalo limekuwa likiandaliwa kwa takribani miaka mitano kukosa utaratibu mzuri wenye tija kwa maslai ya wananchi!!!????

  • Inawezekanaje katika mikoa mikubwa tena isiyo hata na miundo mbinu mizuri kuweza kukamilisha shughuli nzima ya uchaguzi na kutangaza matokeo kwa wakati muafaka huku sehemu nyingine za mijini zikishindwa!?

  • Kulikoni ndani majiji yetu, Mbeya, Dar-es-salaam, Mwanza, Arusha ambapo ni wazi kimiundo mbinu yapo juu ukilinganisha na sehemu nyingine za nchi inashindikana kutangaza matokeo kwa wakati licha ya urahisi wa teknolojia na miundo mbinu uliopo!?
  Hii inanipa mashaka, na ninashindwa kujizuia kuilaumu CCM na NEC maana naona wanahusika katika kudaiwa maisha ya watu yanayowekwa herani. Wajumbe nisaidieni katika hili.
   
Loading...