Kwa mwenendo huu nikifanya maamuzi ya kuishi mwenyewe itakua tatizo?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Wahenga wanasema two is better than one umoja ni nguvu walipata kusema babu zetu, ila kwangu naona kama hizo formula zote mbili zinaenda kugoma japo sio kupenda kwangu ila naona kwangu one is better.

Japo ni maisha ya upweke, japo ni maisha ya kupanga mipango yako mwenyewe, japo ni maisha ya kupika na kula mwenyewe, japo ni maisha ya kufua na kunyoosha mwenyewe la hasha hakuna budii kuyaishi.

Sio maisha rafiki hata kidogo stress, anxiety, depression, burnout nje nje lakini je ndo ntafanyaje sasa, nlipanga mipango kibao nikajiambia ikitiki hakika ntatafuta mchumba/ mke wa kuishi naye japo imekua ngumu mipango yote kukaa sawa ila bado napambana until the last drop.

Umri unasogea mpaka sasa sina mchumba wa kusema ntaishi naye mbeleni, sina rafiki wa kike nikisema hata nikiumwa atakuja kunisaidia au hata siku nikitaka kula chakula kilichopikwa na jinsia ya kike sina kula ni lazima nizame jikoni au kwa mama Ntilie kazi kweli kweli.

Ukimpata mtu anaangalia huyu ana nini huyu atanipa nini na ndo hivo bado mipango haijakaa sawa mwisho wa siku mdada wa watu anaamua kusepa na kuniacha na majonzi na kuniacha nikiweka nyimbo ya Barua ya Daz Nundaz na kusikiliza siku nzima.

Je nikisema niishi mwenyewe to the rest of my life itakua ni sawa? ila sometimes naogopa je nikiumwa who will help me je nikifika uzeeni who will help me nabaki njia panda hakika kupata mke sio ishu ndogo hata kiduchu.

Hongereni sana nyote mliofanikiwa kupata wake wema na kutengeneza familia bora.

Roma ikisema imesema.
 
Mke mwema hutafutwa Mkuu, mtafute utampata.

WAOMBE NA FAMILIA YAKO WAKUSAIDIE KUTAFUTA BINTI MWENYE MAADILI NAAMINI HAUTOKOSA.

Kuishi peke yako ni jambo sahihi lakini inakupasa uwe na hela sana, lasivyo utatuchukia tunaokwambia KATAA NDOA.

NDOA NI NZURI UKIPATA MWANAMKE MWEMA (USIKATE TAMAA).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Tuwape hongera waliopata wake
Kupata mke ni issue moja na kupata mke mwema ni issue nyingne
Ukipata mke inatosha huo wema utaupata hata kwa wadada wa kazi

Over
Mahusiano ni matamu miaka miwili ya mwanzo baada ya hapo ni maigizo.

Halafu imethibitika wengi wanaopost mahusiano yao kweny social media mapichapicha hawapendani kiukweli ni show offs na maigizo.

dronedrake
 
Just relax, weka vigezo vyako kichwani....relax, jipende, punguza kupenda mitoto ya watu.....utamuona mke mwema anakujia mbio mbio.
Mke mwema huwa hamfuati Mwanaume hata siku moja.

USIMUINGIZE CHAKA MDAU.

Kama anataka kuishi peke yake kama sisi (KATAA NDOA) basi azingatie kuwa na pesa nyingi, maana Kuishi peke yako kunahitaji pesa nyingi tofauti na kuoa.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Mke mwema huwa hamfuati Mwanaume hata siku moja.

USIMUINGIZE CHAKA MDAU.

Kama anataka kuishi peke yake kama sisi (KATAA NDOA) basi azingatie kuwa na pesa nyingi, maana Kuishi peke yako kunahitaji pesa sana.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Anawafata Ila wanamtosa, akirelax universe itamletea ambaye atamfata na watastick.....
 
Wahenga wanasema two is better than one umoja ni nguvu walipata kusema babu zetu, ila kwangu naona kama hizo formula zote mbili zinaenda kugoma japo sio kupenda kwangu ila naona kwangu one is better.

Japo ni maisha ya upweke, japo ni maisha ya kupanga mipango yako mwenyewe, japo ni maisha ya kupika na kula mwenyewe, japo ni maisha ya kufua na kunyoosha mwenyewe la hasha hakuna budii kuyaishi.

Sio maisha rafiki hata kidogo stress, anxiety, depression, burnout nje nje lakini je ndo ntafanyaje sasa, nlipanga mipango kibao nikajiambia ikitiki hakika ntatafuta mchumba/ mke wa kuishi naye japo imekua ngumu mipango yote kukaa sawa ila bado napambana until the last drop.

Umri unasogea mpaka sasa sina mchumba wa kusema ntaishi naye mbeleni, sina rafiki wa kike nikisema hata nikiumwa atakuja kunisaidia au hata siku nikitaka kula chakula kilichopikwa na jinsia ya kike sina kula ni lazima nizame jikoni au kwa mama Ntilie kazi kweli kweli.

Ukimpata mtu anaangalia huyu ana nini huyu atanipa nini na ndo hivo bado mipango haijakaa sawa mwisho wa siku mdada wa watu anaamua kusepa na kuniacha na majonzi na kuniacha nikiweka nyimbo ya Barua ya Daz Nundaz na kusikiliza siku nzima.

Je nikisema niishi mwenyewe to the rest of my life itakua ni sawa? ila sometimes naogopa je nikiumwa who will help me je nikifika uzeeni who will help me nabaki njia panda hakika kupata mke sio ishu ndogo hata kiduchu.

Hongereni sana nyote mliofanikiwa kupata wake wema na kutengeneza familia bora.

Roma ikisema imesema.
Mahali sahihi pa kuwepo wakati ukiumwa ni hospital. Unaweza kuwa na partner na asikusaidie nyakati za maumivu au maswaibu ya ulimwengu.
 
Huyo mke mwema atatokea wapi sasa na jamaa anasema hana hela?

:D :D
Wapo, Nakumbuka mume wangu alinitolea posa hata godoro hana, I was 22.....
Issue sio pesa, issue ni vision....anajiona wapi after 5 years, anafanya nini to achieve....

Na ndo mana nimemwambia arelax, nguvu ya kutafuta mke aiweke kwenye kujitafuta yeye....then universe itamletea mtu sahihi wa kuwa nae kwenye safari ya kujitafuta.

Wanawake tuna macho ya rohoni, tunamuona mwanaume miaka ya mbele....just kutokana na anachokifanya sasa hivi.
 
Anawafata Ila wanamtosa, akirelax universe itamletea ambaye atamfata na watastick.....
Wanawake wema huwa wanatafutwa na ni wachache sana, Mke mwema hawezi kumfuata Mwanaume hata siku moja bali Mwanaume ndio humfuata Mke mwema.

Nimempa options mbili,
1) Atafute au aombe ndugu/familia yake imsaidie kutafuta Mke mwema.

2) Kama anataka kuwa kama sisi Kataa Ndoa basi ahakikishe anapesa nyingi sana, maana kuishi peke yako ni gharama sana.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Brother nakushauri uoe hata binti mdogo tu ambae bado mambo hayajaanza kuchanganya, sio hawa above 25 wengi washakua exposed ni type za kukupima na kina fulani waliowahi kudate nao, kukutathmini kwa mali ulizonazo, n.k.

Nawajua watu wanakaribia 40 wameoa mabinti wa 20 na maisha yanasonga mbele.

Usiwe muoga weka chombo ndani, afu uzuri wa hawa wadogo ni kama vile unawafinyanga kama udongo ili muweze kuishi maisha kulingana na jinsi ulivyo.
 
"mwisho wa siku mdada wa watu anaamua kusepa na kuniacha na majonzi na kuniacha nikiweka nyimbo ya Barua ya Daz Nundaz na kusikiliza siku nzima."

👆Kama unaujua huu wimbo basi wewe ni muhenga mzaliwa wa 1980s
 
Tulia ujipate kijana
Usikimbilie ndoa labda km unajijua unapenda sana chini ya mkanda, hapo ndoa itakuepusha na maradhi, nje ya hapo unaweza kuamua kuishi mwenyewe tu hao watu wengine utawapata tu tena watajileta wenyewe uko mbeleni na utakuwa huru kuchagua aliye sahihi kwako
Kuoa sio emergency, usikimbilie kuoa, jipe muda
 
Wapo, Nakumbuka mume wangu alinitolea posa hata godoro hana, I was 22.....
Issue sio pesa, issue ni vision....anajiona wapi after 5 years, anafanya nini to achieve....

Na ndo mana nimemwambia arelax, nguvu ya kutafuta mke aiweke kwenye kujitafuta yeye....then universe itamletea mtu sahihi wa kuwa nae kwenye safari ya kujitafuta.

Wanawake tuna macho ya rohoni, tunamuona mwanaume miaka ya mbele....just kutokana na anachokifanya sasa hivi.
Well said mamy k
 
Back
Top Bottom