Kwa mtazamo wako, ajira gani inatosheleza mahitaji yako yote?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,302
2,000
Habari wakuu !

Kila kazi ninayogusa hainipi kipato ambacho kinaweza kusolve matatizo yangu na familia yangu kwa 100%.

Pamoja nimeajiliwa , nimejiajiri pia kwenye projects kadhaa zinazoniingizia pesa.

Sinywi pombe , sifanyi ufuska na sina anasa zozote zile lakini ni issue sana pesa kutosheleza mahitaji yangu.

Mtazamo wako ukoje?
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,956
2,000
Mama ntilie, ninakula kila siku na faida ninajenga nyumba, ninanunua nguo, na kupata hela ya tiba nikiugua na kulipia Ada ya watoto.
Inanisaidia kuondokana na maadui watano
Ujinga
Maradhi,
Makazi
Njaa na
Umasikini
 

bush crazy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
582
1,000
Mama ntilie, ninakula kila siku na faida ninajenga nyumba, ninanunua nguo, na kupata hela ya tiba nikiugua na kulipia Ada ya watoto.
Inanisaidia kuondokana na maadui watano
Ujinga
Maradhi,
Makazi
Njaa na
Umasikini
Hakika nakubaliana nawe, kazi inayoweza kukabiliana na hao maadui watano kwa asilimia 70, hiyo humfaa mtu,
Pia ikuwezeshe kuwasaidia baadhi ya wenye uhitaji katika maisha ya Kila siku.
 

Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
13,157
2,000
Una roho ya kutoridhika.

Nakukumbusha kuwa hivi vyote tumavyovitafuta duniani tutaviacha hapahapa.

Jikubali na ridhika na unachopata, kila mtu angeridhika na anachopata leo tusingesikia rushwa, ufisadi, madawa nk

Jichunge usije ukadumbukia huko kisa mali za ulimwengu.

Mpe Mungu nafasi ya kwanza ktk kile eneo.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
20,247
2,000
Kwa wakati huu sawa.
Ukiipata utahangaika tena kutafuta ujira wa laki 6 na kuendelea.
But that's very normal.

Kuna wakati unakuwa desperate mpaka unasema "any job at any amount" ukiipata unajiona bonge la fala na jinsi upp behind time.
Any job at any amount halafu hazitokei vile vile.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom