Kwa mtazamo wako, ajira gani inatosheleza mahitaji yako yote?

Mimi nimeamua kwenda kujiunga na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani nikajipigie mabao kupunguza makali ya maisha.
huwa nataman kujiunga na polis ili nwe traffic lakn nkionaga vile wanawabambikia makosa makonda wa dala dala ili wawape chochote akat wao makonda wamepauka,hata lunch hawajala,wanaamka saa 10 usiku wanalala saaa 5+ huko, nguo zao zmechakaaa, yaan dah huwa nabadili plan asee
 
Unahisi utaendelea kua na options milele?
 
Una roho ya kutoridhika.

Nakukumbusha kuwa hivi vyote tumavyovitafuta duniani tutaviacha hapahapa.

Jikubali na ridhika na unachopata, kila mtu angeridhika na anachopata leo tusingesikia rushwa, ufisadi, madawa nk

Jichunge usije ukadumbukia huko kisa mali za ulimwengu.

Mpe Mungu nafasi ya kwanza ktk kile eneo.

Hii ndio point yenyewe ambayo wengi tunasahau.
 
Nilidhani ungeuliza, ni kipato gani kinatosheleza mahitaji yako?!

Sio waajiri wote hulipa sawa, hatakwa taaluma moja yenye viwango sawa bado vipato huwa tofauti.
 
naamini haijalishi how much you make what matters is how much you save. Au utakua unafanya kazi ya money in---- money out.work done is equal to Zero.
 
Mara nyingi kwa watu wengi mahitaji huongezeka kadiri hela zinavyoongezeka.

Nakumbuka kipindi cha awali kabisa wakati naanza kazi jijini Dar, nilikuwa nafanya mizunguko fulani kwa wateja wetu.

Katika mizunguko hiyo nikawa nimefika ofisi moja jengo la IPS. Sasa katika kusubiri mkutano tukawa tunapiga stories na mabosi na matarishi wa ike ofisi.

Stories zikafikia suala la pesa na kuridhika.

Basi yule tarishi akasema yeye akipata shilingi milioni mia moja tu ataridhika.

Yule bosi akawa anashangaa sana, milioni mia moja tu?

Katika mawazo ya yule bosi shilingi milioni mia moja ni hela ndogo sana. Kwa sababu kwa level yake alikuwa kashaipata na kuitumia, kashachukua mikopo mikubwa, kashalipa kodi kubwa serikalini, kashalipa rent ofisi kubwa mjini, akiipigia mahesabu ya biashara kubwa, shilingi milioni mia moja si nyingi sana.

Kwa yule tarishi ilikuwa hela kubwa sana kwa mahesabu yake. Na yeye angeipata na kuingia kwenye biashara kubwa, pengine angeiona ndogo.

Basi tusichoke kitafuta kwa kadiri ya uwezo wetu na uhalali wa kisheria unavyoturuhusu.
 
Habari wakuu !

Kila kazi ninayogusa hainipi kipato ambacho kinaweza kusolve matatizo yangu na familia yangu kwa 100%.

Pamoja nimeajiliwa , nimejiajiri pia kwenye projects kadhaa zinazoniingizia pesa.

Sinywi pombe , sifanyi ufuska na sina anasa zozote zile lakini ni issue sana pesa kutosheleza mahitaji yangu.

Mtazamo wako ukoje?
Ubunge kipindi kimoja tu kitanitosha
 
FAMILIA yako ina idadi ya watu wangapi.. Na je, unadhani unapaswa kuendelea kuwasaidia hata watu wazima ambao ilibidi uwape njia au uwatafutie NJIA za wao kujisadia wenyewe - ILI UPUNGUZE GHARAMA... Watengenezee njia za vipato hao wengine-ILI shid ikitokea, Mnasolve pamoja so hapo Mzigo hautokuelemea
 
Mara nyingi kwa watu wengi mahitaji huongezeka kadiri hela zinavyoongezeka.

Nakumbuka kipindi cha awali kabisa wakati naanza kazi jijini Dar, nilikuwa nafanya mizunguko fulani kwa wateja wetu.

Katika mizunguko hiyo nikawa nimefika ofisi moja jengo la IPS. Sasa katika kusubiri mkutano tukawa tunapiga stories na mabosi na matarishi wa ike ofisi.

Stories zikafikia suala la pesa na kuridhika.

Basi yule tarishi akasema yeye akipata shilingi milioni mia moja tu ataridhika.

Yule bosi akawa anashangaa sana, milioni mia moja tu?

Katika mawazo ya yule bosi shilingi milioni mia moja ni hela ndogo sana. Kwa sababu kwa level yake alikuwa kashaipata na kuitumia, kashachukua mikopo mikubwa, kashalipa kodi kubwa serikalini, kashalipa rent ofisi kubwa mjini, akiipigia mahesabu ya biashara kubwa, shilingi milioni mia moja si nyingi sana.

Kwa yule tarishi ilikuwa hela kubwa sana kwa mahesabu yake. Na yeye angeipata na kuingia kwenye biashara kubwa, pengine angeiona ndogo.

Basi tusichoke kitafuta kwa kadiri ya uwezo wetu na uhalali wa kisheria unavyoturuhusu.
Mkuu asante kwa maneno mazuri sana sana
 
Back
Top Bottom