Kwa msimamo huu walanguzi wamepewa shushi

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
1,025
1,743
Naomba nimsaidie Naibu Waziri wetu wa Kilimo, Mh. Hussein Bashe kufikiri kwa mara ya pili kuhusu msimamo unaoendelea kutolewa na serikali kuhusu bei ya mazao ya chakula hususani mahindi!

Katika mtazamo wake ambao ndio unaakisi mtazamo wa Serikali kiukweli waziri wetu amepotoka au amepotoshwa! Uzoefu unaonyesha kuwa mazao na hasa mahindi huwa mikononi mwa wakulima kwa muda mfupi sana ambao ni kati ya mwezi Mei hadi Julai, lakini kufikia mwezi wa Agosti haya mazao karibu asilimia 90% ya mahindi huwa yamelanguliwa na walanguzi tena kwa bei ya ulanguzi yenyewe.

Hivyo leo hii serikali inaposema imewaachia wakulima kujipangia bei wenyewe hapa ni sawa na kuwaruhusu walanguzi wawalangue tena wananchi kama jinsi walivyowalangua wakulima. Maumivu haya yanaenda mpaka kwa wakulima wenyewe kuanza kuuziwa mazao yao wenyewe waliyolanguliwa.

Hivyo, kitendo hiki hakiwatendei haki hata wakulima wenyewe vinginevyo serikali ingeweka wazi msimamo huu tangu mwanzoni mwa msimu wa kilimo na sio miezi ya masika, Vinginevyo inaleta tafsiri kuwa kuna uwezekano waziri mwenye mamlaka akawa na maslahi ya moja kwa moja na jambo hili, lakini kinyume na hapo ni kuumiza wananchi bila sababu.
 
Back
Top Bottom