Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Juzi (jumapili) nilishuhudia magari makubwa ya serikali zaidi ya mia mbili yakiwa kwenye mwendokasi yakitoka DSM wanakoishi watumishi wa serikali yakielekea Dodoma wanakofanyia kazi za wizara zilizohamia Dodoma. Hawa watumishi wa serikali makazi yao na familia zao zipo DSM na Wao wapo Dodoma.
Kila ijumaa mchana wanarudi DSM kwa magari ya serikali yanayotumia mafuta kwa fedha za serikali au za walipakodi na kurudi Dodoma Jumapili jioni. Watumishi hawa wapowapo tu Dodoma wengi wakirandaranda maeneo ya Chuo Kikuu Dodoma.
Naamini mojawapo ya hoja za kuhamisha serikali kwenda Dodoma ilikuwa kupunguza gharama na matumizi ya Serikali. Lakini kinachoendelea sasa ni KUONGEZA GHARAMA ZA KUENDESHA WIZARA. Hili inabidi tuliseme.
From intellectual in social network