Kwa mliowahi kuumizwa na ndugu zenu

Kwa mliowahi kuumizwa na ndugu zenu

Nakumbuka nikiwa mdogo ndugu /wazazi kwa namna moja walininyanyasa sana kwani kuna vitu kama mtoto/mdogo walikuwa na uwezo wa kunisaidia ila walinipuuza, hali hiyo iliweza kunijenga nikapambana kwa nguvu zangu zote kujijenga kiuchumi na ilinifanya pia kujitenga sana na watu na ndugu zangu pia, sasa kwa sasa naona maumivu ya kujitenga na ndugu ni makubwa sana naomba msaada wenu wakuu, kwani sijisikii raha ya kumsaidia ndugu yangu kwani walishindwa kunisaidia kipindi ninakomaa kwa hiyo chuki niliyonayo ni kubwa mno mpaka najitahidi kuwaacha na maisha yao ila ndo hivyo ndugu yako lazima kuna vtu vinakuunganisha naye kama misiba, harusi nk nikiwaona napatwa na maumivu zaidi
Je nifanyeje ili niweze kuondokana na huu mzigo??
Mliwasemehe aje walezi wenu pale waliposhindwa kujitoa kwa ajili yako na walikuwa na uwezo??.
Kama mnavyojua leo unaweza kuwa na uwezo ila kesho mambo yamebadilika hapa naona ndugu ambao walinitolea nje kipindi hicho nao wameshuka kiuchumi watt wao na wao wenyewe wanahitaji msaada wangu wa hali na mali je nifanyeje niweze kuwa na roho ya huruma kwao???
legeza moyo ndugu usiwe na chuki ...

wengi tu tumepitia hayo ila unasamehe na kusahau.. tunapita
 
Dear wengine tulifanyiwa mabaya more than that but we forgave na ku moved on with our life .. Cha ajabu God use us to help those who badly hurt us from the past.. And yes I do help them even though they wronged me multiple times but , I have learned to forgive and let God deal with them .. So dear forgive and help them if you can .. Remember you dont do this for them but for God and yourself to become free.. May the Lord help you to be able to forgive and fill you with the Holy Spirit in Jesus name Amen.. Thanks..
 
Huu ndo uzi wa kwanza nakutana nao nlipoingia jf this morning....mamy ..i think kuna vitu unaeza dhani vinakutokea wewe tu..kumbe vipo kwa wengine pia!!!
 
Kisasi
Kulipisha kisasi ya paswa tumwashie Mungu. Imeandikwa Warumi 12:19 "Wapenzi sijilipizie kisasi bali ipiosheni ghadhabu ya Mungu maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa anena Bwana." Mithali 20:22 Yasema "Usiseme mimi nitalipa mabaya mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipishe kisasi kwa ajili ya upendo. Imeandikwa, Mathayo 5:38-39 "Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino lakini mimi nawaambia msishindane na mtu mwovu lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie la pili."

Usifurahi adui wako anapo kuwa na taabu. Imeandikwa Mithali 24:17-18 "Usifurahi adui wako aangukapo wala moyo wako usishangilie ajikwaapo Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akageuza mbali naye hasira yake.
 
Haya maisha acha tu, mtu kama huyo akipata matatizo usipomsaidia hizo lawama zake utajuta kumfahamu
mkuu ishu kama hii haijakutokea wewe tu, nikiwa udogoni nimeteswa sana na kufanyiwa unyanyapaa sana kitu ambacho kimeniathiri kisaikolojia mpaka sasa hivi, ila huwezi tenga ndugu zako, wangekua marafiki ungeweza ila ndugu ni ngumu
mbinu ambayo natumia kupata amani nao na kuwasamehe ni kujaribu kukumbuka yale mazuri yao waliyonitendea, hope na wewe pia lazima kutakua na baadhi ya mazuri waliyokufanyia,
kinyongo sio kizuri kabisa, ukiwa na kinyongo hata uwe tajiri hutaweza kufurahia maisha kwa amani
 
Huu ndo uzi wa kwanza nakutana nao nlipoingia jf this morning....mamy ..i think kuna vitu unaeza dhani vinakutokea wewe tu..kumbe vipo kwa wengine pia!!!

Very true Daddy .. As humans being , we are very easy to think is not fair or to blame when trials come , but wait and hear somebody else who is willing to tell his / her stories hapo ndio utajua yupi kapitia mengi and mabaya zaidi.. Thats why the bible says ; Give thanks in all circumstances for this is the will of God in Christ Jesus for you.. Give thanks to the Lord for He is good , His love endures forever .. Amen.. When we learn to appreciate God through all our trials , for sure He will never leave us nor forsaken us.. Amen.. Thanks..
 
kuna msemo unasema undugu lawama, mwingine unasema undugu sio kufanana ni kufaana. kuna pia tenda wema nenda zako usingoje shukurani, pia shukurani ya punda ni mateke, pia bora lawama kuliko fedheha. mwana akinyea mkono, haukatwi.

Nina ndugu amabae ziku zote chake chake na cha wenzake chake, akiwa na shida anaweka mabango ndugu wamsaidie, akiwa kwenye neema anaweka nyodo hajui kutoa hata shukrani, amenitesa, nimemsaidia sana katika shida.

Kila ninaporudi nchini kutoka huku ughaibuni ninakotafuta maisha huwa siji mikono mitupu, lazima nae atapata chochote. lakini siku zote analipa fadhila kwa mateke mpaka inafikia kuwaza kuwa sina haja ya kurudi Bongo asilani, sijawahi omba msaada kwake hata siku moja na wala sihitaji msaada kwake ila nahitaji appreciation tu.

Huwa ananiumiza to the maximum lakini Mungu amenipa moyo mkuu, japo kuwa ya yote, kila aangukapo katika shida na kutindikiwa, huwa kamwe asilani sijawahi mtupa, na nitaendelea kum support siku zote.
 
mimi nadhani huyu mdau angependa sana kuwasamehe lakini anashindwa kwa hiyo mpeni jinsi atakavyoweza kubadilisha mawazo yake ya kukumbuka mabaya yao
 
mkuu principle rahisi kama ukiamua kusamehe samehe endelea kuwasaidia.. ila jua hata uwalambe makalio hahawezi ona msaada wako bado watalalamika... sasa muhimu ukiamua kuwasaidia saidia bila kujali watakushukuru vipi.......... nyingine ni kuendelea kukaa nao mbali vitu muhimu vya kushiriki to me ni matatizo kama msiba . maafa na mambo kama hayo.. harusi si muhimu sana kushiriki......... kama unampango wa kuoa harusi kubwa na ndugu wawepo hapo ndipo utaumiza kichwa mpaka uzimie iala kama huna mpango wa kuolewa wala kuoa huku hakuna sherehe we endelea na maisha yako tu.. msiba watakuja tu
 
Hapa nashindwa kusaidia MTU ambae alishindwa kunisaidia kipindi nipo udogoni na walikuwa na nafasi ya kunisaidia

Pole sana mleta uzi ila hawa ndugu wamekuwa nyota yako ya mafanikio Kwa kukosa msaada kutoka kwao umekuwa mtu wa kujitegemea na umegundua Huna pa kutegemea endapo utapata Shida Hilo no jambo la kushukuru sana Kwa kugundua chuki na roho mbaya za nduguzo unga li Mdogo sisi wengine tulipewa Upendo feki udogoni kufikia ukubwani unapatwa na jambo linlohitaji msaada kutoka Kwa nduguzo wa karibu ndio wanakuwa wa kwanza kujiweka mbali na wewe kabisa Kwa hiyo ndugu yangu wewe cha kufanya Ni kuwa samehe na kuwasaidia pale tu inapobidi tena msaada wako usiwe wa kuilazimisha nafsi hakikisha nafsi yako iko radhi kutoa msaada wewe toa kumbuka Ke chuki zao na roho mbaya zao wewe umejua kusimama mwenyewe . Endelea kumuomba Mungu akupe wepesi katika hili
 
mimi nadhani huyu mdau angependa sana kuwasamehe lakini anashindwa kwa hiyo mpeni jinsi atakavyoweza kubadilisha mawazo yake ya kukumbuka mabaya yao
kusamehe naamini ataweza kusamehe ila kusahahu si jambo rahisi kabisa... labda ajifunze kupotezea hata pale anapokumbuka
 
Unazungumzia ndugu mie mama yangu mzazi pamoja na yote ninayo mfanyia lakini amekuwa akinitangaza ubaya mbaya hata kufikia kusema ninatuma vibaka wakaibe police ndio hela ninayompa na anapokea sina kinyongo naomba moja Kati ya mawili mungu anichukue duniani halafu ataonja pendo langu au mungu amuonyeshe umuhimu wangu nafanya biashara ya daladala nne bado hanielewwi
Msamehe tu mama ni mama
 
Kumbe sio mimi tu,asante Mungu kunionyesha wengine wenye mama wa namna hii,usiombe kupata mama asiye na shukurani!!!
 
Nina story tofauti kidogo...nina kaka yangu.Niliwahi kulazwa na hakuwahi kunipigia hata simu ya pole.That was a last that broke a camels back..From that day,I dont give a damn about him.Life goes on..
Mi nadhani kuna mazingira ya kufanana linapokuja swala na ndugu ni rahisi sana kumchukia ndugu yako tena kwa kinyongo hata kwa jambo dogo lakini rafiki watu hadi wanadhulumiana mamilioni wanasamehana lakini kwa ndugu mmmmmh!
 
Mie sbb ya mama kufanya hivyo ni kudhani kwake kumtetea sana baba kuliko wanae wote kwani wao walitengana miaka ya 83 nikiwa mdogo mwanzo niliona mzee ni katili sana lakn baadae nikagundua mama ni mtu hatari sana hafai kuishi na binadamu yyt akishilikiana na ndugu zake wakataka kuuza nyumba ya mzee kwa kununua hakimu nyumba niliyojenga mie kwa hela niliyopigika machimbo Tunduru kila mtu anajua niliwaambia mama na nduguze wauze km mahakama ilivyoagiza ila mama utandanganywa na kk zako toka hapo nimewekwa kundi moja na Osama bahati mbaya mzee na kaka yangu wametangulia mbele ya haki ila maisha yanaemdela nimejemga dar na yy nimemjengea kijijini ndio mashambulizi ni bora ya Bush kwa Osama
 
Kisasi
Kulipisha kisasi ya paswa tumwashie Mungu. Imeandikwa Warumi 12:19 "Wapenzi sijilipizie kisasi bali ipiosheni ghadhabu ya Mungu maana imeandikwa kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa anena Bwana." Mithali 20:22 Yasema "Usiseme mimi nitalipa mabaya mgojee Bwana naye atakuokoa."
Tusilipishe kisasi kwa ajili ya upendo. Imeandikwa, Mathayo 5:38-39 "Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino lakini mimi nawaambia msishindane na mtu mwovu lakini mtu akupigaye shavu la kuume mgeuzie la pili."

Usifurahi adui wako anapo kuwa na taabu. Imeandikwa Mithali 24:17-18 "Usifurahi adui wako aangukapo wala moyo wako usishangilie ajikwaapo Bwana asije akaliona hilo likamkasirisha akageuza mbali naye hasira yake.
Ni maneno yaliyojaa hekima na busara nyingi i'm really touched.
 
Back
Top Bottom