Nakumbuka nikiwa mdogo ndugu/wazazi kwa namna moja walininyanyasa sana kwani kuna vitu kama mtoto/mdogo walikuwa na uwezo wa kunisaidia ila walinipuuza, hali hiyo iliweza kunijenga nikapambana kwa nguvu zangu zote kujijenga kiuchumi na ilinifanya pia kujitenga sana na watu na ndugu zangu pia.
Sasa kwa sasa naona maumivu ya kujitenga na ndugu ni makubwa sana naomba msaada wenu wakuu, kwani sijisikii raha ya kumsaidia ndugu yangu kwani walishindwa kunisaidia kipindi ninakomaa kwa hiyo chuki niliyonayo ni kubwa mno mpaka najitahidi kuwaacha na maisha yao ila ndo hivyo ndugu yako lazima kuna vtu vinakuunganisha naye kama misiba, harusi nk nikiwaona napatwa na maumivu zaidi.
Je nifanyeje ili niweze kuondokana na huu mzigo?
Mliwasemeheje walezi wenu pale waliposhindwa kujitoa kwa ajili yako na walikuwa na uwezo?
Kama mnavyojua leo unaweza kuwa na uwezo ila kesho mambo yamebadilika hapa naona ndugu ambao walinitolea nje kipindi hicho nao wameshuka kiuchumi watoto wao na wao wenyewe wanahitaji msaada wangu wa hali na mali je nifanyeje niweze kuwa na roho ya huruma kwao?