Kwa mliosoma mkitumia majina mawili na mkaongeza la tatu,nisaidieni hapa!!!

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
724
551
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
 
Nenda Mahakama ukajaze form ya kiapo kwajili ya kaongeza jina. Mimi pia niliwahi kuwa na tatizo km lako. Gharama ni 5000
Nashukuru sana.Sasa ni mahakama gani,ya mwanzo au hata ya wilaya au mkoa kote wanafanya hivyo?Pia baada ya kiapo sasa jina wataongeza kwenye vyeti au watanipa tu barua ya utambulisho?
 
nafikiri nenda kwa mwanasheria au mahakamani utajaza kitu inaitwa deed poll then utaenda kuisajili wizara ya ardhi kama sijakosea baada ya muda kisheria (nafikir itangazwe kwenye govt gazzete)utakua umebadili jina
 
Nenda Mahakama ukajaze form ya kiapo kwajili ya kaongeza jina. Mimi pia niliwahi kuwa na tatizo km lako. Gharama ni 5000

Yategemea na mahakama mimi niliambiwa 15,000 waliniwekea mlolongo wa malipo hadi nikajikuta naghaili tu.
 
Nashukuru sana.Sasa ni mahakama gani,ya mwanzo au hata ya wilaya au mkoa kote wanafanya hivyo?Pia baada ya kiapo sasa jina wataongeza kwenye vyeti au watanipa tu barua ya utambulisho?
Binafsi nilienda Mahakama ya wilaya.majina ya kwenye vyeti yatabaki km yalivyo ila hiyo form form itakuwa inakusaidia popote penye uhitaji wa majina yote matatu
 
Nashukuru sana.Sasa ni mahakama gani,ya mwanzo au hata ya wilaya au mkoa kote wanafanya hivyo?Pia baada ya kiapo sasa jina wataongeza kwenye vyeti au watanipa tu barua ya utambulisho?
Vyeti vitabaki na majina uliyoyasomea tu. Kama jina unaloliongeza lipo pia kwenye cheti cha kuzaliwa siyo shida sana, unaweza hata usilazimike kuapa.
 
Kama cheti chako cha kuzaliwa kina Jina ulilopewa, Jina la Baba la Ukoo, inatosha sana. We endelea kutumia majina mawili, watakaotaka la tatu unaongeza la tatu. Mimi sijawahi pata usumbufu wowote na ndivyo ilivyo kwangu.
 
Binafsi nilienda Mahakama ya wilaya.majina ya kwenye vyeti yatabaki km yalivyo ila hiyo form form itakuwa inakusaidia popote penye uhitaji wa majina yote matatu
Nashukuru sana.Inachukua muda gani kupatiwa hiyo fomu?Nina maana ukiijaza tu na kusainiwa na hakimu ndiyo imekamilika na unapewa?
 
Kama cheti chako cha kuzaliwa kina Jina ulilopewa, Jina la Baba la Ukoo, inatosha sana. We endelea kutumia majina mawili, watakaotaka la tatu unaongeza la tatu. Mimi sijawahi pata usumbufu wowote na ndivyo ilivyo kwangu.
Kuna bosi mpya ananizingua kunipitishia malipo anadai ni watu wawili tofauti
 
Ipo hivi Ndugu, Kama unaitwa majina mawili katika vyeti vya shule na chuo, na hilo jina la tatu lipo katika cheti chako cha kuzaliwa haina shida na inakubalika hadi utumishi. Mimi nilisoma kwa majina mawili had chuo, nilipoajiriwa nikaongeza jina la tatu katika ajira, ila jina hilo la tatu lipo katika cheti changu cha kuzaliwa. Hakuna aliyenisumbua had leo na utumishi natambulika kwa majina matatu. Hivyo haina shida. Ila kama umesoma na majina mawili na umeongeza la tatu na jina hilo la tatu, halipo katika cheti cha kuzaliwa, hapo inabidi uende kuapa mahakamani. Ili kuthibitisha uhalali wa jina la tatu.
 
Back
Top Bottom