Kwa mliosoma mkitumia majina mawili na mkaongeza la tatu,nisaidieni hapa!!!

It's possible mkuu hd leo mm natumia mawili tu

Mbona kawaida sana tu.....mie ninatumia mawili tangu primary, o level,A level,Universty...mpaka kazin
Kama ndivyo bhasi mlisoma enzi za ukoloni:! Majina ma3 tulikua tunalazimisha hata ukoo wangu nilikuja kuujua baada ya kuhimizwa shuleni darasa la 4 nilikua najuaga jina langu na la dingi na kabila ila ukoo baadae
 
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
Mkuu,,nenda mahakamani, ukaape baada ya hapo utapewa AVIDAFFITY FORM itakayo halalisha majina mawili ya mwanzo na majina matatu , ila kwenye.Vyeti yataendelea yaleyale matatu
 
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
Ukipata ajira ya serikalini hua wanaongeza wao wenyewe kwenye mikataba
Mfano vyeti vyote vimeandikwa
Juma Ramadhani
Na unaitwa Juma Ramadhani Hamis

Kwenye mikataba utajaza
Juma Hamis Ramadhani jina hilo la tatu litakuwa katikati

Kama si hivyo ukienda mahakama yoyote iliyo karibu nawe utapewa kiapo cha ubatizo wa jina hilo la tatu na utapewa kitu kitakacholihalarisha jina hilo
 
Nenda mahakamani upate affidavit ndio unaweza kuwa na ruhusa ya kutumia majina yako matatu, hata Mimi nilikuwa na tatizo kama lako lakini nilienda kupata kiapo cha kubadili jina
 
Jina la tatu unaloongeza kama itakuwa ni jina la babu au la ukoo,litakuwa linaonekana katika cheti cha kuzaliwa kwenye column ya baba wa mtoto na hiyo inatosha (mfano ni mimi mwenyewe),ila unaweza ukongezea na mbwembwe za kuapa mahakamani ili kuondoa doubts kabisa lakini hakuna ulazima, wahanga wa hili tupo wengi na bado tupo salama labda mambo yabadilike huko mbele na kwa kweli hatuombei manake itakuwa usumbufu mkubwa usio na umuhimu manake cheti cha kuzaliwa kitakuwa ni kama kimedhalilishwa.
Umesema kweli mkuu.
Mimi mwenyewe kwenye cheti cha kuzaliwa jina la tatu linaonekana katika hiyo column ya baba wa mtoto,na vyeti vyangu vyote kuanzia elimu msingi hadi elimu ya juu nimetumia majina mawili....sijawahi pata shida kwa maana ikihitajika majina matatu huwa naweka tu
 
Exactly mkuu!
 
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
Kachukue kiapo kwa mwanasheria au mahakamani,upeleke kwa msajiri au RITA kazi kwisha.
 
Nashukuru sana.Sasa ni mahakama gani,ya mwanzo au hata ya wilaya au mkoa kote wanafanya hivyo?Pia baada ya kiapo sasa jina wataongeza kwenye vyeti au watanipa tu barua ya utambulisho?
Hata advocate au mwanasheria yyte unapata.mahskama yyte pia
 
Back
Top Bottom