Kwa mliosoma mkitumia majina mawili na mkaongeza la tatu,nisaidieni hapa!!!

Mkuu,

Kama nimekuelewa vizuri, unachopaswa kufanya ni kuwasilisha kiapo ambacho kitabainisha nia yako ya kutumia majina hayo matatu "Affidavit". Kiapo hicho ni nyaraka inayoandikwa na kuthibitishwa "Attested" na Kamishna wa Viapo (Wakili, Hakimu/Jaji).

Ninaweza kukusaidia kufanikisha hilo kama bado una uhitaji.

Kaka ...
Asante kaka ngoja niende mahakamani
 
Haina haja ya kuahangaika.
Mie vyeti vyangu vyote vina majina mawili. Nilipoanza ajira nikalazimika kuweka la tatu so automatically sehemu nyingi zinazohusiana na taasisi utahitajika kuwa na majina matatu ambalo utalitumia na hakuna madhara ya kisheria as long as cheti chako cha kuzaliwa kina majina yako,ya baba yako na babu yako.
In case kama umesajiliwa kwa jina lako la kwanza na la ukoo na likarukwa jina la kati hapo ndipo sina ujuzi napo.
 
Petro E. Mselewa karibu tunaomba msaada huku ndugu yangu, wakili msomi, nguli wa sheria
Majina huongezwa, kupunguzwa, hubadilishwa au kurekebishwa kwa nyaraka maalum ya kisheria inayoitwa Deed Poll. Hii huandaliwa, kusajiliwa na kuchapishwa. Baada ya hapo, mbadili jina huanza kulitumia jina jipya. Kiapo/Affidavit hakitumiki kubadili jina. Kiapo hutumika kupambanua tu majina yaliyopo kwenye nyaraka tofauti kwa muda ule tu.
 
Mimi nimesoma hadi chuo nikitumia majina mawili ninataka kuongeza la tatu msaada please (tafadhali) kwa hatua za kuchukua.
Nisaidieni wana jf
Ulisomea nchi gani? Maana kwa nchi hii ni ngumu kufika chuo ukiwa na majina mawili tu... Mtoto wakati anaanza tu darasa la kwanza wakata majina matatu, kila siku alikuwa ananisumbua kuniuliza, eti babu yangu anaitwa nani?

hata hivyo kwa uzoefu wangu, niliongeza mwenyewe la tatu (la katikati) maana nilikuwa natumia ubini wa jina la ukoo na kuendelea kuyatumia yote matatu hadi yakazoeleka, na yapo kwenye nyaraka zangu zote ikiwemo passport, vyeti vya chuo n.k.
 
Usibishe mkuu, mbona inawezekana. Hata mm nimefika chuo kikuu kwa majina mawili tu
Kweli mkuu, haya mambo yameanza miaka ya 90. Kabla ya hapo hakukuwa na tatizo. Kuna siku bank walikataa kupokea cheque kwenye account ikabidi wanipe cash sababu jina liliongezwa herufi, Mfano Simiyu, cheque ikaandikwa Simmiyu.
 
Ipo hivi Ndugu, Kama unaitwa majina mawili katika vyeti vya shule na chuo, na hilo jina la tatu lipo katika cheti chako cha kuzaliwa haina shida na inakubalika hadi utumishi. Mimi nilisoma kwa majina mawili had chuo, nilipoajiriwa nikaongeza jina la tatu katika ajira, ila jina hilo la tatu lipo katika cheti changu cha kuzaliwa. Hakuna aliyenisumbua had leo na utumishi natambulika kwa majina matatu. Hivyo haina shida. Ila kama umesoma na majina mawili na umeongeza la tatu na jina hilo la tatu, halipo katika cheti cha kuzaliwa, hapo inabidi uende kuapa mahakamani. Ili kuthibitisha uhalali wa jina la tatu.
Upo sahihi dingi
 
Back
Top Bottom