Wanabodi,
Declaration of Interest
Naomba ku declare interest kuwa mimi sina chama, namfahamu Lissu na kumkubali sana tuu, pia na sympathize yeye kwa kilichompata, ila ninachofanya hapa ni being objective. Pia nafahamu fika kinachotokea kila ukifanya ukosoaji wa Chadema au viongozi wao wanaowaabudia, hivyo wale wa kutukana, be free to do so, the truth will always be the truth and will stand up to the end.
Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.
Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu. him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela, kwa sababu Mandela alirejea kuendeleza mapambano bila kujua nini kitampata, na alipofungwa jela na kusurvive hadi kuja kuja kuwa rais wa SA, hakujua, lakini Lissu, being a lawyer, anajua kabisa huwezi kutuhumu na kutaja majina ya watu bila ushahidi, hivyo ukirejea nchini, anajua fika akikanyaga tuu ardhi ya Bongo, atapokelewa na nani, na anajua atafikia wapi, and kwa situation hii tulionayo sasa, with vitu kama polonium 210, I doubt kama he will be so lucky kama Mandela.
Hivyo huu ni wito kwa watu wa karibu na Lissu, mshauri tuu aendelee na matibabu, hata mwili ukipona kabisa, aendelee tuu na matibabu ya kisaikolojia, ila aandike barua kwa Spika kuelezea kuwa bado anaendelea na matibabu, na kabla hajarejea, atumie international fora, kujihakikia akirejea, hata pokelewa na wale mimi ninaodhania ndio watampokea na hata fikia kule mimi ninakodhania atafikia.
Waliomshambulia Lissu ni watu wasiojulikana, hivyo nilishauri humu
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums
Pia nikawatambulisha aina mbili za wasiojulikana
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums
Nikauliza
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums
Mwisho nikasema waandishi wenye uwezo wa IJ, wanaweza kumsaidia Kamanda Siro kuwabaini wasiojulikana hawa, na mimi ni miongoni mwa waandishi wa IJ,
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums
My Take.
The Hard Talk kwa Lissu was a waste, Chadema inabidi ianzishe kitengo cha International Politics kuwafunda makada wa Chadema, wakipata international foras, waseme nini in terms of International politics. That was a great opportunity kwa Lissu kuongea as a president in waiting na sio kuongea kama mwana harakati mwanzo mwisho. Hakupaswa kutoa tuhuma zisizo na ushahidi, pia hakupaswa kuponda mwanzo mwisho as if Magufuli is all that evil, and is doing nothing good for this country.
Kwa upande wa lingua, kiukweli Lissu ana flow, kwenye top 5 wetu, mtu pekee mwenye uwezo wa kuflow kivile ni Mama Samia, na labda Majaliwa, tukishuka chini zaidi kwa mawaziri, MFA na January they are good. Kwa upinzani, ikitokea mtu kama Zitto akakaribishwa Hard Talk kiukweli mtaona the difference, nawashauri Wapinzani the man to bank on ni Zitto, kwa sababu Lissu kaharibu, unless awe kaharibu makusudi ili akirejea apokelewe kule so that they can make big noises!.
Paskali
Rejea za Ushauri wangu kwa Tundu Lissu na Chadema
Swali la Morality: Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa? - JamiiForums
Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!. - JamiiForums
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue, Serious Issue ya Katiba ni UKUTA!. - JamiiForums
Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele! - JamiiForums
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!. - JamiiForums
Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe! - JamiiForums
Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele! - JamiiForums
Kweli kabisa Pascal, kuna tatizo kubwa kwa wafuasi hadi wanachama wa hivi vyama kuelewa sera na itikadi ya vyama vyao ndio maana wanapinga kila kitu hata kama ndio sera yao kwavile tu anaitekeleza JPM. Sera ya ushoga umeona ilivyompa shida Lissu ingawa wafia vyama watamtetea. Kuhusu kurudi atarudi tu, mbona Zitto anaropoka kila siku na afanywi chochote?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mniwie radhi kwa kuwakwoti nyie wote wawili kwa pamoja ili nami nichangie...
Nimesoma mlichokiandika mara mbili ama tatu. Nikarudi kutazama na kusikiliza tena mahojiano kati ya Tundu Lissu na Steven Suckur...
Nikaona you all missed something. Sina hakika ni lugha ama uwezo wa kuelewa mantiki au evil intentions behind you...
Mimi hoja yangu si Tundu Lissu kurudi nchini kwake ama kuendelea kuwa mkimbizi wa kisiasa huko aliko. Siko huko.....
Lakini nilicho na uhakika nacho ni kuwa Tundu Lissu atarudi Tanzania tena si muda mrefu kwa sbb all he said are not new at all. Ameyasema mara nyingi tena kwa lugha kali kuliko hiyo akiwa London, hakuwahi kukamatwa...
With due respect, hoja yangu kubwa ni kujaribu kutafakari hiki unachojaribu kukiingiza kwenye akili ya vichwa vyetu, kwamba Tundu Lissu alitumia fursa vibaya aliyoipata kwa kutoeleza hata moja zuri la Magufuli....
Aeleze mazuri ya Magufuli kwani yeye ni mke wa Magufuli? Msemaji wa "serikali ya Magufuli?" Msemaji wa CCM?...
Ungesema mazuri ya NCHI mama Tanzania ningekuelewa. Lakini hakukuwa na swali lenye muelekeo huo moja kwa moja!!
Na kwa hoja hii haraka haraka nikajifunza mambo mawili kuwa:
1. Kumbe viongozi wetu kupitia ujumbe wako wanahitaji fursa kutumia international media platforms kama BBC, CNN, Sky News, Al Jazeera nk ktk kusema serikali wanazoziongoza zimefanya hili ama lile...
Kwa fursa aliyoipata Tundu Lissu, wengi imewauma sana hususani watu wa serikali (watawala) na wanaowaunga mkono....
Si kwa sababu ameongea uongo, ama uzushi .... la hasha....
Isipokuwa kaongea mambo ambayo kwa wengi wanaona kama amevunja "taboo" moja inayopaswa kulindwa sana.... kutosema mabaya ya serikali na hususani Rais Magufuli
😳😳!... And that's the problem we have right now....
2. Uwezo mdogo wa wengi wa waandishi habari wetu wa Kitanzania (ukiwemo wewe Paschal Mayallah ktk hili) wa kuelewa mantiki na kuchambua mambo/hoja kwa kuzingatia "context"...
Mfano kuna mmoja (si wewe, lakini naamini ni journalist) kamtukana kweli Tundu Lissu eti tu kwa sababu katika mazungumzo yale amemsikia muuliza maswali (Stephen Sucker) katika moja ya maswali yake akitumia maneno "baseless allegations"....
Hitimisho lake huyu mwandishi ni kuwa, hata mtangazaji alimwona Lissu akiwa na madai yasiyo na ushahidi (baseless allegations)...
Duuh, nilishangaa na kupigwa na butwaa kuliko maelezo!!
Tukirudi kwenye hoja, kwanza tukubaliane na wewe Paschal Mayallah kuwa kuna uwezekano mkubwa hujatazama wala kusikiliza mahojiano hayo mwanzo mwisho...
Ama kuna possibility number two, kuwa, hukujipa nafasi ya kutosha kupata logic ya kila kilicho zungumzwa na Tundu Lissu.
Nitaeleza......
1. Mahojiano yalikuwa ya kipindi cha takribani dakika 24 tu. Mimi naamini kwa style yako ya kuuliza maswali, kama ungekuwa Stephen Sucker ungeuliza swali moja na kuishiwa muda...
Ama kwa style yako ya kujieleza, ungeishia kujibu swali moja tu na muda kukuishia na kumwacha mtangazaji akitia kikapuni maswali na kurudi nayo kwa mhariri wake...
2. Lengo la kipindi ilikuwa ni Tundu Lissu na yaliyompata na kwa kuhusianisha jaribio la kuuwawa kwake na harakati zake za kisiasa, ukosoaji wake wa sera za utawala wa Rais Magufuli....
Ndiyo maana swali la kwanza la ufunguzi (opening question) lilikuwa, vipi Tundu Lissu na unajisikiaje hali yako kwa sasa?
Lililofuata na ni description ya tukio kwa ujumla na kwa ufupi...
Kisha swali muhimu na ambalo ndilo "backbone" ya mjadala mzima na kuzaa mengine yote yaliyofuata ni hoja ya kurudi ama kutorudi Tanzania ni:
Aliulizwa: Unadhani jaribio la kutaka kukua lina uhusiano na harakati za kuukosoa Utawala wa Rais Magufuli, sera zake na kumuita petty dictator??
Hili ndilo lililozaa maswali mengine yote kuhusu uwekezaji, sijui ghost workers, conrsevative controversial govt statements aginist human right as quaranteed by constitution such as "right to privacy" nk nk
Na hili la human rights na msingi wake ikiwa ni vita ya ushoga vs mkakati wa Paul Makonda (Daud Albert Bashite) RC wa Dsm kupambana nao, Tundu alijibu very clearly unless mtu awe na matatizo yake tu ya uelewa wa mambo kushindwa kumwelewa TL...
Alisema wazi kabisa, kuwa, jambo lolote lililo kinyume na katiba siku zote ni unconstitutional kwa mujibu wa katiba ya JMT ikiwemo "right to privacy"......
Na hili ni kweli kabisa, kama mtu ni shoga ama msagaji na anafanya mambo yake ndani ya chumba chake, how does it concern me and you? Tunapata wapi audacity ya kuingilia mambo ya sirini ya mtu huyo?.....
Kwani ni viongozi wangapi wakubwa ndani ya serikali ni mashoga na wasagaji so long as wanafanyia mambo yao sirini? Si hata Paul Makonda mwenyewe anatuhumiwa kuwa ni shoga? Alionekakana anafanya ushoga wake hadharani? Mimi na wewe hatujui na kiukweli haituhusu....
Itatuhusu tu pale vitendo hivyo vikifanyika hadharani maana hapo itakuwa kinyume cha sheria za Tanzania.... violation of right to privacy!!
Na swali moja kabla ya lile la mwisho kabisa lilikuwa ni aidha kurudi ama kutorudi Tanzania.....
Na kwamba umejiandaaje kurudi Tanzania wakati waliojaribu kukuua hata hawajakamatwa, hakuna kesi, hakuna uchunguzi....huogopi?
Hili sasa ndiyo likazaa swali la mwisho la kufungia HARD TALK la kujibiwa na Tundu Lissu kwa ufasaha ndani ya sekunde 50....
Ni kuhusu ku- fight against Magufuli through ballot paper box...
Tundu Lissu kwa ufasaha kabisa akajibu ".......If my fellow members of the party see me a correct person.....I am more than enough to face Magufuli...!!!"
3. Hakuna mahali katika mazungumzo mwanzo mwisho alipoulizwa direct aeleze mazuri ya serikali na ya Rais John Pombe Magufuli ama sera za CHADEMA...
Ulitaka awe anatoka nje ya hoja kwa mitego ya Muuliza maswali kama Rais Magufuli wakati ule wa press conference kule Uganda hata kusaidiwa kujibu maswali na mwenyeji wake Rais Museven? Anaulizwa hivi, yeye anajibu vile? Au anaulizwa swali la maana yeye anatoa majibu ya kitoto na kijeuri tu???
Na kwa taarifa yako, siyo jukumu lake kueleza mazuri ya "serikali" ama ya Rais Magufuli. Wenye kazi hiyo ni yeye mwenyewe Magufuli, ama Polepole ama waziri wake yeyote...
Kazi ya Tundu Lissu (kama angeulizwa lakini bahati mbaya hakukuwa na swali hilo) ni iwapo angeulizwa kueleza MAZURI YA NCHI YA TANZANIA na mpango wake wa kuyaendeleza mazuri ya nchi mama Tanzania....
Kwa hiyo ni vyema tukatofautisha NCHI YA TANZANIA na SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA BWANA JOHN POMBE MAGUFULI....
Tundu Lissu was absolutely full of composure and understable na nikuhakikishie hata huyo Mzungu amemkubali kama tunavyomkubali sisi wengine huku!!