Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Paskali tuko pamoja..
*Ameegeuza hard talk kuwa jukwaa la siasa na sio jukwaa la facts and points. No convincing but mere expressing
*Anatumia muda mwingi kugombana/kumsema Magufuli kama personal/personality war na sio vita ya kitaifa dhidi ya Serikali.
*Kukwepa maswali ya msingi na ku jump kwenye anayotaka kusisitiza kisiasa kunamfanya aonekane mwana harakati na sio mwanadiplomasia... hivyo kupunguza makali ya hoja.
*Taja japo moja zuri basi... unapopinga hata mazuri unaonekana una makengeza ya akili.
*Maswali magumu na ya mitego anayajibu kwa kutumia hadithi zilezile ndeefuuu na blah blah za kitaa na sio kujibu kama pro..
*Kelele za kuonewa na ukandamizaji kwa viongozi wa Afrika ni kitu cha kawaida sana hivyo namna alivyoelezea ni big waste kwakuwa he was too unrealistic na kuonekana unalenga kuchafua na sio kuwa na lengo la mabadiliko.
** Big waste
Ungekuwa we ndyo lissu umepigwa risasi 16 mwilini mwako usingeandika huu upupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ushahidi ataupata wapi zaidi ya ushahidi wa kimazingira uliopo?

Leo hii hata nyie waandishi mnaweza kuandika habari za kiuchunguzi juu ya nini kilitokea Lissu aliposhambuliwa?

Serikali iruhusu uchunguzi huru alafu muone kama alioongea yatakuwa ya uwongo.

Hivi umejiuliza IGP au waziri wa Mambo ya Ndani akienda kuhojiwa nini kitatokea kwa kuangali jinsi swala hili liivyokuwa handled mpaka sasa?

Unadhani kati ya Lissu,IGP au Waziri wa Mambo ya Ndani, nani angekuwa na wakati mgumu wa kujibu maswali yanayomuhusu?

Alafu si ni wewe Pascal uliewahi kuleta mada iliyoibua mjadal kuhusu Lissu kupigwa risasi?

Sometimes huwa una masilahi na mada unazoleta humu ila inawezekana tu watu humu hawajakujua na jambo ambalo una masilahi nalo unaweza kulianzishia mada zaidi ya moja hasa ikitokea kuna mtu wako ameguswa au jambo husika linakuhusu au kuna mtu unataka kumnanga au kumfagilia..

In short, sometimes hauko objective kama unavyotaka watu humu wakuamini.

Pascal usidhani unajua kila kitu!!
Hakika umenena
 
Hard talk ilikuwa ni bomba sana. Tundu kaonyesha uwezo mkubwa. Pia kumbuka kuwa Tundu alikuwa haongei kama Mgombea Urais, aliongea juu ya yale yaliyomsibu. TL alijeruhiwa vibaya but by God's grace he is alive and well. Kinachosikitisha ni kuwa hadi hivi sasa tukio lile baya na kioga halijawekwa hadharani uchunguzi wake. TL yuko ffit.
Waandishi wa habari walio wengi wa kitanzani mko so subjective. Andikeni ukweli, kitu ambacho hamuwezi asilani.
Mayala, Lissu akirejea bongo, basi fanya naye hard talk nyingine baada hiyo unayoiita the worst' kushindwa. Tundu Lissu ni mwanaharakati wa siku nyingi sana, na aliyejijengea heshima kubwa. Ni mwanasiasa mashuhuri. Ni mwanasheria muhimu na mashuhuri.
Watu kama Lissu wanahitajika Sana katika Awamu hii ya cherehani 4 ni Kiwanda
 
Hoja yenye maana kwa mtu asiye muelewa ni ile anayoipenda isemwe. Hali kadharika na hoja inayohusu Lisu. Waliokinyume na Lissu ndiyo hao wanaoponda kuwa amefail kwenye hoja zake na w anajitahidi kuwaaminisha watu kuwa ni mwongo. Na walioupande wa Lissu wanaona amefanikiwa sana. Turudi kwenye ukweli bila kujali upande. Mtu hata akikamtwa red handed kwenye uhalifu wowote anabaki kuwa mtuhumiwa mpaka pale uchunguzi ufanywe ushahidi upatikane na mahakama imtie hatiani. Kabla ya hapo huyo mtu anabaki kuwa mtuhumiwa. Lissu anatuhumu, kutokana na mazingira ya tukio la kushambuliwa kwake,lakini hata baada ya pale anaowatuhumu ndiyo wenye mamlaka za vyombo vya kiuchunguzi hawakutaka kuchunguza bila sababu za msingi. Je kutuhumu ni kosa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kosa.... ni majinga tu kwa kuwa yanahusika
 
PASKALI Mayalla mkuu nakuomba uhamie Chadema pamoja na kuwa ni mwandishi wa kujitegemea lakini ni muona mbali ilikulinusuru taifa hili unahitajika sana huku upinzani.
 
Pascal Mayalla, ni bora kuwa moto ama baridi ijulikane moja, kuwa vuguvugu ni unafiki, wewe ni muunga juhudi tunafaham hilo.

Umesema hivo kwa kuwa media na waandishi hamko huru kwa regime hii ya sasa. Kwa yale yalompata Lissu hata kama ungekua wewe sidhani kama ungesema tofauti au kuunga juhudi...!

Mahojiano ya Lissu Hardtalk kajibu maswali na kutuhumu kwa ushahidi wa mazingira, wewe ni mwanasheria hilo kwako halionekani?

Unaposema wafuasi wa Chadema wanatukana wanapo guswa viongozi wao wanao waabudu unakosea, ahabudiwi mtu ila ni kusimamia misingi ya haki na usawa kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika ni muunga Juhudi
 
Mkuu Charles Dotter nikiri ndio kwanza nasoma maandiko yako. Lakini hakika umesema ukweli mtupu. Natamani kuona Uzi huu unisomwa na viongozi kuanzia ikulu hadi Lumumba.
Hivi hawaoni kuwa Lissu ni muungwana sana katika hali ya kibinwdamu? Kama wao wanaweza kumchukia MTU kwa kuwasema tuu jee watajisikiaje kwa mtu unayeamini kakutumia upigwe risasi 16 ufe? Kasababisha operations zaidi ya 20 mwilini mwako?
Hebu tuvae u Tundu Lissu kisha tujipime

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata usipouvaa Ndugu ..Utu wa mtu sio vyama ni ujinga tu wa makada
 
Hivi wakimpeleka mahakamani watamshitaki kwa lipi?

1. Hawajafungua jalada la upelelezi, hawajahoji mtu hata mmoja, hawajakamata mtu hata mmoja wa kuzugia juu ya Jaribio la kuuawa kwake, Sasa watajenga hoja gani ya kijinasua na tuhuma mbele ya JAJI?

2. Kapigwa risasi kwenye compound ya makazi ya viongozi, hakukuwa na mlinzi hata mmoja, Watamueleza vipi Jaji mpaka amuone Lissu ana kesi ya kujibu?

3. Wameng'oa CCTV camera katika eneo la tukio, wakili wa Lissu akiutaka upande wa Jamhuri ulete hiyo footage wataiipeleka?

4. Kanyimwa pesa za matibabu ya bunge, Watamueleza nini Jaji kuwa walimnyima kwa nia njema mtu ambaye hakujipeleka mwenyewe nje bali alipelekwa nje huku akiwa hajitambui?

5.Ni mtu aliyetoa taarifa za kufuatiliwa na watu ambao wanaonekana hawakuwa na nia njema lakini hakupewa ulinzi wowote, watamueleza nini Jaji kuwa walizifanyia kazi tahadhari zake?

Tusing'ate maneno hapa:

Kama inatembea kama bata, inakula kama bata, inatweta kama bata na inakunya kama bata, basi hiyo ni bata huhitaji ushahi



Hapo ni Manemane
 
Kutetea Ushoga ni jambo lilinikera zaidi
Jingalao kweli names are reflections of ones character's. Wapi umesikia Lissu katetea ushoga? Au lugha aliyotumia ndiyo kikomo chako cha uelewa?
Lissu amemnukuu Mahiga( Foreign affairs Secretary) akitoa msimamo wa serikali kuhusu ushoga dhidi ya Bashite aliyekurupuka tu bila kuwashirikisha wakubwa zake.
Lissu amegusia issue ya privacy ambayo kila mtanzania kwa mujibu wa katiba anastahili kuwa nayo.
Lissu hajatetea ushoga hata kidogo.
Nitakupa mfano wa dhati kabisa kuhusu dhana ya Lissu.
1. Wachungaji, mapadre na mashekhe wanaofungisha ndoa kwenye nyumba za ibada wanapaswa kufungisha ndoa kwa sharti la wanaofunga ndoa wawe hawajawahi kukutana kimwili siyo tu kwa wao wanaofunga ndoa bali katika maisha yao yote hadi wanapofikia hatua ya kufunga ndoa.
Swali; Je wachungaji, mapadre na mashekhe wawe wanawachunguza kwanza wanandoa kabla ya kuzifungisha? Hii ndiyo dhana ya Lissu, mwenye masikio na asikie na mwenye macho vivyo hivyo!
Kama utaritibu huu ukitumika basi hakuna ndoa itakayo fungwa lakini si hivyo tu Wachungaji, mapadre na mashekhe watakuwa wanaingilia uhuru/privacy za wanandoa.

Nawakilisha!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna hata siku moja Mayalla kachemka kama hili bandiko!! Hebu wakuu mjikumbushe mabandiko ya Mtatiro siku za nyuma dhidi ya serikali, pia mjiulize serikali ilifanya nini mpaka jamaa akaipongeza. Tatizo la watu humu ni njaa kama majina yao.
Hata siku moja kauli alizokuwa akizitoa mtatiro sikujua kama atakuja kuzipinga mwenyewe. Kweli adui muombee njaa, watanzania njaa ndiyo inatumaliza, otherwise Mayalla usingeandika hivi umetia shaka kama lemtuzi ndivyo alianza.
 
"The Hard Talk kwa Lissu was a waste, Chadema inabidi ianzishe kitengo cha International Politivs kuwafunda makada wa Chadema, wakipata international forums, waseme nini in terms of International politics, That was a great opportunity kwa Lissu kuongea as a president in waiting na sio kuongea kama mwana harakati mwanzo mwisho. Hakupaswa kutoa tuhuma zisizo na ushahidi, pia hakupaswa kuponda mwanzo mwisho as if Magufuli is all that evil, and is doing nothing good for this country."
===========================
Acha mapenzi binafsi na woga wa kushambuliwa, tuchambulie ulichokiona kwenye yale mahojiano
lisu amejibu kulingana na maswali yalivyoulizwa
unasema hana ushahidi lakini kuna circumstantial evidence,mtu anaelezea walinzi wameondolewa siku anashambuliwa,cctv cameras zimeondolewa!!!!!
demokrasia na uhuru wa mawazo ndio msingi wa maendeleo,...
dreamliner zinasaidia nini iwapo ukisema ukweli kuwa imezuiwa sehemu unazawadia pyu pyu?
 
Back
Top Bottom