Shagiguku
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 407
- 133
Habari za leo wanaJF
Ndugu yangu mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela Mwanza, kama mimi ningekuwa ndiyo weye (Mkurugenzi wa Manispaa Ilemela) basi ningemuagiza mhandisi wa manispaa kushughulikia barabara ya National hadi wilayani kwa kujenga mitaro imara ya kusafirisha maji.
Na ningemwagiza aweke makaRavati katika eneo la shule ya msingi Gedeli, Buswelu center na Bondeni ili kuifanya barabara isiharibike kwa maji ya mvua yanayopita juu ya barabara.
Lakini kikubwa kuliko vyote ningeifanya barabara hiyo kupitia fedha za makusanyo ya halmashauri ijengwe kwa kiwango cha lami kuanzia hapo National hadi eneo maarufu la "Mbogamboga" hapo Buswelu center.
Bahati mbaya tu ni kwamba mimi siyo mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela.