Kwa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela - Mwanza

Kwa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela - Mwanza

Wana ilemela tumeshajifunza hatuchagui tena upinzani hawana maono kabisa. Mama Mabula na kijana wetu Mr.Wanga pigeni kazi.
Kazi gani amepiga huyu Mama Mabula? Acha kampeni za kijinga!
 
Kazi gani amepiga huyu Mama Mabula? Acha kampeni za kijinga!
hebu tumpe haki yake mama mabula, dili za viwanja hazipo tena, hakuna migogoro wa mashamba ilemela, barabara zimeboeka sana, maji ya uhakika, elimu imeimarika na uwajibikani uko juu sana, hebu nenda ofisi za umma huduma unapata chapchap, habari boss kaenda kunywa chai mara kaenda kwenye kikao hazipo tena.
 
Siku ile Magufuli ametua uwanja wa ndege hapa Mwanza akatoa amri hii barabara ya Airport - Igombe ifunguliwe haraka, naona kila kitu kilikufa, ila ile kauli ilikuwa ni ya kisiasa Zaidi siyo kitaalamu, na ni suala la muda tu hiyo barabara itafungwa, sasa ilikuwa ni jukumu la Manispaa na TANROADS kukutana haraka na kupanga mipango ya kuanza ujenzi wa Barabara hii ya NATIONAL-IGOMBE kwa kiwango cha LAMI ili nauli ishuke kutoka sh. 700 ile ya awali hadi 400 au 500, na hii ndio ilisababisha hadi Rais akatoa amri ya kufunguliwa hii barabara maana wakazi wa maeneo hayo kila siku walikuwa wanatumia sh. 1400 kama nauli kutoka IGOMBE kupitia National hadi mjini, sasa, sijui MKURUGENZI wa MANISPAA ndugu yetu WANGA ameridhika na hali hii au vipi?

Na kwa MANISPAA Ya Ilemela hiyo ndio barabara kero Zaidi inayotunyima usingizi wakazi wa Mwanza, maana watu tuna nyumba zetu huko lakini tumeshindwa kuhamia kutokana na kukosekana usafiri wa UMMA kuja kazini Mjini.

Tafadhari sana ndugu yetu Wanga, kama mipango ya lami bado sana, basi zungumza na SUMATRA ili Hiace zianzie maeneo ya NYAMWILOLELWA -SHIBULA-ILALILA-KAHAMA-BUSWERU-Hadi National-TO mjini, wakati mipango ya lami mkiikamilisha...


Hivi ina maana mapato ya ndani ya manispaa hayawezi kuijenga hii barabara kwa kushirikiana na TANROADS? mambo mengine ni kujiongeza tu si mpaka RAIS aseme, mkishaanza kuijenga ninyi basi serikali kuu itaweka mkono wake kuwasupport, na iwe kweli LAMI siyo kokoto tu Uchafu wa lami.
Naona maoni yako kwa kiasi yamefanyiwa kazi, tutafika tu. Barabara ya lami kupitia Buswelu kwenda Igombe itakamilika tu.
 
Back
Top Bottom