Kwa milioni tatu nifanyeje ili nikaishi kwangu?

Mchanga upo,Shimo la choo lipo tayali bado kujenga tu,lakini mambo hayaendi kabisa
Ada + Kodi ninayopa hapa na hali ya mitaani sioni kesho yenye matumaini
Hiyo nyumba ni kubwa, kama umeshajenga msingi inua chumba kimoja na choo (hata hiyo bedroom 2) kwa kuacha matoleo kwenye tofali za mwisho ili baadae ukipata pesa nyingine uendelee, ukisema uinue vyumba viwili utakwamia njiani tena
 
Na wewe milioni tatu hapo itafanya kitu gani? Labda ununue tofali uziache hapo zipigwe na mvua wakati unajitafuta. Mawazo ya kuweka chumba kimoja sikubaliani nayo kabisa. Nyumba za kuungaunga uwa zinakosa mvuto

Gangamala jitufute ukijipata endelea na ujenzi. Kila jambo lina wakati wake wakati wako bado ila kwa hiyo ramani una vision
 
Zinafanya kazi ndugu,nimenunua tofali 800,cement mifuko 15, nanyanyua master na chumba kimoja,pia mbao 30( 5500) na mabati 30. Najua vitakamilika hata sio kwa ubora ila nitahifadhi familia kwa kipindi hiki
 
Tamanio yako ninzuri na niyakisasa kwakua umeshajenga msingi, na shimo la choo lipo tayari pandisha vyumba viwili ili uanze maisha hapo alafu utamalizia kidogo kidogo
Nikushukuru kwa ushauri wako,nimeufanyia kazi na iko hivi ( Lengo sio kumtambishia mtu,ila somo na kutiana moyo) kama ulivyofanya kiongozi
Tofali 800* 1000=800000
Cement 15* 24000=360000
Bati 30* 19000= 570000
Nondo 6*25000= 150000
Mbao 25* 5500
Kokoto na mchanga vipo zilibaki kwenye msingi
Fundi 150000
Misumari kg 11* 4000= 44000
Mawe kwa ajili ya choo 5* 60000= 30000
Fundi 60000
N.b vilivyobaki nitabanana mwezi January nikamilishe,milango 2, grill 2, sink 2 za choo na PVC.
Ubarikiwe sana
 
Watu wengi hujenga kutokana na hofu ya maisha na sio hesabu za maisha.

Unapata Mil 5, unaanza kujenga. Nyumba yenyewe unajenga nje ya mji. Gharama za usafiri kwa mwezi zinakuwa zaidi ya kodi uliyokua unalipa. Nyumba yenyewe haikamiliki. Kwanini usiendelee kupanga. Zungusha hela hiyo. Huku ukijenga taratibu kutokana na faida unayoipata?

Ukianza jiuliza, 'je, hela hii itamaliza kupaua/itatosha?', jua unaingia kwenye mateso makubwa kimaisha.
 
Mtazamo mzuri,lakini kwa mjini mjini,kama una familia inatakiwa angalau upange vyumba 2 na sebule, kwa hapa mkoani si chini ya 2,500,000 kwa Mwaka,pia utakuwa na nauli ,umeme na maji.
Lakini hautakuwa na uhuru wa kulima vimboga mboga au kufuga hata kuku kwa ajili ya kitoweo. Ila vyumba viwili hivyo hivyo ukiwa huko mbali na mjini utakuwa huru kufanya vyote na una amani
N.B kuzungusha hela pia ni kipaji, kuikuza na kapata faida,pia kuna kupoteza kabisa,imenitokea mara nyingi ndio maana nimefikia hii hatua
 
Back
Top Bottom