Kwa mfumo wetu mbovu hautibiki kwa kuunda Baraza jipya la Mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mfumo wetu mbovu hautibiki kwa kuunda Baraza jipya la Mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshume Kiyate, May 9, 2012.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF.
  Ni wazi kwamba uozo uliopo kwenye mfumo wetu mzima ni mbovu, alichofanya rais si jambo geni kusukwa upya baraza la mawaziri ni kuongeza ulaji na ufisadi unakithiri, ndivyo itakavyokuwa mara hii.

  Rais amesema ataendelea kuwawajibisha maofisa wa Serikali pia, maana yake ni kuwastaafisha kwa manufaa ya umma, kitu ambacho kimekuwa kikifanyika miaka yote, hebu watuambie mpaka sasa ni Mawaziri na Wakurugenzi wangapi wako gerezani wakitumikia vifungo? Wangapi wamefilisiwa mali walizotupora.

  Mfumo mzima ni mbovu ndio maana Serikali inatoa misamaha ya kodi ya shilingi zaidi ya trilioni 1.02. Hii ni asilimia 18 ya kodi yote inayokusanywa.

  Sio kila kitu rais mpaka kuambiwa na CAG au Kamati ya kudumu kujua uozo uliopo, haiwezekani Serikali itumie Sh544 bilioni bila kuidhinishwa na Bunge, Sh bilioni moja zimelipwa mishahara kwa watumishi hewa na Sh3 bilioni zimetumika katika balozi zetu nje ya nchi. Fedha hizo ziko nje ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

  Huu ni ubovu wa mfumo mzima wa Serikali hautaondoka kwa kuunda baraza jipya la Mawaziri.
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Solution?
   
 3. O

  Ogutu New Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani kwamba si jambo la kulaumu sana.sawa inauma na kusikikitisha lakini ushawahi kufikiria cha kufanya ili hayo yote yasiweze kutokea mi nadhani kwa ni jambo la kuwaombea viongozi wetu hili waweze kubadilika maana mtu anapokua na hofu ya mungu ndani mwake hawezi kuiba wala kufanya yalio maovu mbele za bwana na jamii kwa ujumla
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ripoti ya CAG ni upande mmoja,lakini ari na morale ya kufanya kazi ni upande mwingine ukweli ni kuwa kwa sababu JK na IKULU yake sio watendaji wamejawa na ubabaishaji hakuna jipya kabisa litakalo tokea ni business as usual
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Lete ushauri tufanyeje sasa ili rais na watendaji wake waweze kugundua madudu kabla CAG hajapita.

  Nimesikia kuna kitengo kipya cha Internal Auditing na amechaguliwa Chief Internal Auditor. Na ninavyofahamu mimi huyu ndio anakuwa karibu sana na anafahamu mengi zaidi kuliko CAG, ngoja tusubiri tuone.

  Lakini bro hii nchi itajengwa na mimi na wewe. Kama mimi na wewe ndio watendaji huku chini tunaona madudu tunanyamaza tunasubiri CAG aone mwenyewe na JK wake basi ujue hatutafika. Kila mtu mahala pake pa kazi awe mpiga filimbi.
   
 6. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mfumo huu mbovu tulionao hauhalalishi wizi, ufisadi na unyang'au wa moja kwa moja! Hivyo watu kuwajibishwa ni jambo la lazima hadi hapo tutakapokuwa na mfumo bora ambao labda katiba mpya itauweka!
   
 7. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Internal auditors wako miaka nenda miaka rudi lakini walikuwa hawana meno kwa kuwa walikuwa chini ya management! Labda tusubiri utaratibu uliowekwa hivi sasa kuwa watakuwa kitengo kinachojitegemea!
   
Loading...