Kwa Matukio haya Wahalifu ni CHADEMA?

Kwa Matukio haya Wahalifu ni CHADEMA?

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,746
Wakuu hapa JF

Nimefikiria na kutafakari sana juu ya Matukio mengi yaliyotokea katika nchi hii juu ya Kudhuru Binadamu na hata Kuuawa na ni vema nikaorodhesha matukio haya ili tutafakari je ni kweli CHADEMA ndio ipo nyuma ya uhalifu huu dhidi ya binadamu?

1. Kuna lile tukio la Kuuawa kwa yule Mwenyekiti wa CCM kule Rungwe katika Tukio hili watuhumiwa walipatikana na wamehukumiwa KIFO kwa hii nalishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwajibika juu ya tukio hili

2. Kuuawa kwa Kuchinjwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA kule Usariver Arusha, katika tukio hili watuhumiwa walikamatwa na kupelekwa mahakamani lakini baadae walitoka mbele ya Polisi na hakuna aliyekamatwa hadi sasa na inawezekana hakuna anawatafuta wala kufuatilia issue hii.

3. Kushambuliwa na kuumizwa vibaya kwa Wabunge wa CDM pale Mwanza Tukio hili liliripotiwa na wahusika walitajwa ikiwa ni pamoja na No. za Gari waliyokuwa wakitumia na mmiliki wake. Katika Tukio hili hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa

4. Kutekwa na kuumizwa vibaya Dr. Ulimboka, Katika tukio hili kila kitu kiliwekwa wazi wahusika walitajwa ikiwemo na mawasiliano ya lakini hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kukakamtwa yule mkenya kama kisingizio.

5. Mlipuko wa Bomu pale Olasiti Kanisani uliosababisha vifo. katika tukio hili amekamatwa kijana mwendesha Bodaboda hadi sasa huku kukiwa hakuna mwendelezo wa nini kinachoendelea na tukio hili lilikuwa nyuma ya nani hasa yaani muhusika mkuu.

6. Mlipuko wa Bumo Soweto katika mkutano wa CDM. Chagonja alipewa kazi maalum ya kufuatilia issue hii lakini hadi sasa ni kimya na hakuna aliyekamatwa huku ilifahamika wazi aina ya Bomu lililotumika na lilikotoka je Vyombo vyetu vya usalama inamaanisha vimeshindwa kufuatilia Kiwanda lilikotoka na kujua ni nani aliuziwa?

7. Kushambuliwa vibaya Mh. Nassar kule Monduli na vijana ambao walifahamika kwa majina na gari waliyokuwa wakitumia. Katika Tukio hili hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa

8. Kuwekewa sumu Dr. Mwakyembe. Katika tukio hili hakuna aliyekamatwa huku ikijulikana wazi ile sumu iliyotumika(pollonium 210) inakotoka na umiliki wake.

9. Kumwagiwa Tindikali kijana Musa Tesha wa Kule Igunga. Katika tukio hili tumeshuhudia wakikamatwa wale vijana wa CDM na kuhusishwa na kesi hii na ikafunguliwa kama Ugaidi lakini ikashindikana na hadi sasa hatujui mwendelezo wake.

10. Kutekwa na Kuumizwa KIBANDA, hapa kwanza kabisa tulishuhudia Mwigulu na Zitto (Dec 2012) wakiwa Star TV na ndipo Mwigulu alipojinadi anamkanda unaoonyesha Viongozi wa juu wa CDM wakipanga mauaji, Baada ya hapo ndipo alipotekwa na kuumizwa Kibanda baada ya muda mfupi akakamatwa Lwakatare na Ludovick huku mawasiliano ya Ludovick, Denis Msack na Mwigulu yakiwa hadharani na kuonyesha uhalisia wa Tukio lile. Mwendelezo wa Kesi ya Lwakatare na Ludovick hadi sasa kimya.

11. Kushambuliwa na hadi kusababisha Kifo kwa Dr. Mvungi. Katika tukio hili KOVA alituonyesha Kofia na Skaf za CDM kwenye TV na kutamka kuwa ni moja ya vifaa walivyokutwa navyo wale wahusika wanaoshukiwa kumshambulia Dr. Mvungi. Baada ya Hapo hatujasikia tena zaidi ya Tamko la Mbatia na waumini wa kanisa wakisema wamewasamehe wote waliofanya uhalifu huo.

12. Kuuawa na Polisi kwa Daud Mwangosi katika harakati za shughuli za CDM. Katika tukio hili tulishuhudia yule kijana eti polisi akipelekwa mahakani lakini alikuwa kafunikwa na sura yake ikifichwa na hakuna aliyebahatika kupiga picha yeke tunajiuliza ni kwa nini ilikuwa hivi? na je mbona mwendelezo wa Kesi haupo?

13. Kuuawa kwa Padri Mushi kule Zanzibar. Katika tukio hili tulishuhudia akikamatwa yule kijana wa CUF kwa kushabihiana na ile picha ya kichina ya FBI lakini pia kesi ipo Kimya.

14. Kuuawa kwa yule kada wa CDM kule Igunga. Katika tukio hili hakuna aliyekamatwa na sidhani kama kuna ufuatiliaji wa tukio hili.

15.Tukio la Juzi la kutekwa na kuteswa pasipo mateso kwa yule Mwenyekiti wa CDM pale Temeke. Tukio hili ndio kwanza Movie inaanza chini ya director KOVA hatujui mwisho wake.

Nimeorodhesha hayo matukio kiuhalisia mengi yamejikita kwenye siasa na wengi wa wahanga ni Viongozi, wafuasi na wanachama wa CDM na ni vema tukaangalia inakuwaje katika matukio yote haya ni Moja tu lililotolewa hukumu na lenyewe ni kwa kuwa tu aliyeuawa ni MwanaCCM na hata haya ambayo yapo mahakamani unakuta wanaoshitakiwa ni WanaCHADEMA kwa kuwa tu wahanga ni wanaCCM lakini kwa yale ambayo wahanga ni CHADEMA hatusikii kesi wala mtu kukamatwa.

NAULIZA TENA KWA MATUKIO HAYA WAHARIFU NI CHADEMA?

Moderator naomba sisi kama wanachama wa hili jukwaa tunapoweka thread kama hizi ni vema mkazipa muda ili watu wasome na kutafakari na sio kuziondoa haraka.
 
ndugu yangu huu ni mtaji wa ccm na wanausalama uchwara,ambao wanafadhiliwa na wakina lowassa,nape,muaji mwigulu nchemba na wauza sembe wote wa ccm, hebu fikiria katika hizi zote hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyetiwa nguvuni na plisi, WENYE AKILI ZAO TUNAJUA NI MUENDELEZO WA HUJUMA YA MATUMANINI MEMA YA WANANCHI ILA KWA MSAADA WA MUNGU ALIYEHAI WOTE WATASHINDWA KATIKA MIPANGO YA UOVU NA HIKI KIZAZI KINAJUKUMU LA KUWAHUKUMU WAHUNI WOTE NA WAUAJI WA CCM IWE 2015 AU HATA 2015
Wakuu hapa JF

Nimefikiria na kutafakaJUri sana juu ya Matukio mengi yaliyotokea katika nchi hii juu ya Kudhuru Binadamu na hata Kuuawa na ni vema nikaorodhesha matukio haya ili tutafakari je ni kweli CHADEMA ndio ipo nyuma ya uhalifu huu dhidi ya binadamu?

Back
Top Bottom