Kwa mambo makubwa anayoyafanya mtoto wa Tandale, kama wananchi wakimuhitaji tuu, Kubenea mpishe!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,624
Wanabodi,
Ijumaa ndio hii imeanza, hivyo tuswich kwenye the weekend mood, tusijadili mambo mazito mazito siku za weekend, tujadili vitu light, with a light touch, tuenjoy week end yetu vizuri.

Naomba ku declare my interest kuwa mimi huwa siangalii TV za burudani, kama EATV, ETV na Wasafi, kwa sababu sio kuwa sihitaji kuburudika, bali huwa sina muda huo, lakini kutokana kitu kinachoitwa "Strength of a woman", nimejikuta nimelazimika kuangalia Wasafi TV, na hii sio mara yangu ya kwanza kulazimishwa kuiangalia TV hii, hata kwenye hili tukio, nililazimishwa.
Mwanajf, Naibu Waziri, Ahudhuria Birthday Wema Sepetu, Mlimani City, Avalia Gauni la Rangi ya Chanikiwiti, Apendeza!, Atokelezea!. - JamiiForums

Kupitia Wasafi TV, nimeshuhudia mambo makubwa mazuri yanayofanywa na Mtoto wa Tandale, Diamond Platinums kwa wakazi wa Tandale na shule za Tandale
Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale - JamiiForums

Ikitokea wananchi wakamuomba awe mwakilishi wao kule mjengoni, kama ilivyo kwa Sugu na Prof. J, itambidi Mhe.Kubenea ajikalie tuu pembeni ampishe njia huyu dogo, ameonyesha uwezo, hivyo atakuwa kama Mo Dewji.
Natoa pendekezo hili huku nikijua fika elimu ya Mtoto wa Tandale, Elimu yake ni darasa la saba tuu, kule bungeni tunao wabunge wengi tuu wa darasa la saba akiwemo Msukuma na Kibajaj, lakini bungeni humo, tunao ma Ph.D holders, hivyo angalieni michango yao bungeni na udarasa la saba wao, ulinganishe na michango ya ma Ph.D holders ndio mtanielewa, hivyo naomba hoja ya elimu ya Mtoto wa Tandale humu isiwe subject to discussion, na wote watakaobeza elimu ya huyu dogo, nawashauri watembelee tovuti ya Bunge, muangalie kwanza CV ya aliyepo ndipo mje mponde darasa la saba!.
Katika bandiko langu hili niliuliza Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?. - JamiiForums

Pia kuna walioishia darasa la saba kwa matatizo tuu ya maisha, lakini vichwani mwana wana IQ kubwa kama huyu
Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!. - JamiiForums

Kuna hoja kuwa mtoto wa Tandale ni entertainer na sio politician, hivyo hata changia lolote la maana katika mijadala ya maana, kama mule mjengoni, tunao entertainers kama Sugu na Prof J. Mtu ukiwa vizuri vizuri mfukoni, wanachotaka wananchi wako ni kuwaletea maendeleo, na sio lazima kusema sema saana mule Bungeni, tuna wabunge wenye nazo, kama kina Nimrod Mkono, kuna Lameck Airo, kula Turky, kuna Abood, vipi mnawasikia kusema sema?, kulikuwa na kina Rostam Aziz, Mo Dewji, hawa shida ndogo ndogo za wananchi wao, wanazimaliza wenyewe.

Pia nazijua kazi za Bunge ni kutunga sheria, kupitisha bajeti ya serikali na kuisimamia serikali, hivyo kuna watu watakuja na zile zile hoja za dharau kuwa mtu kama huyu atawezaje?, jibu ni simple tuu, kama mule mjengoni darasa la saba wapo na wameweza, vivyo hivyo huyu nae ataweza, ponti muhimu ni kama ni kutungwa kwa sheria mbovu, bunge letu limetunga sheria nyingi mbovu na hadi nyingine kwenda kinyume cha katiba yetu, na hao mabingwa wa sheria, wenye elimu nzuri na wasomi wapo, jee wamesaidia nini?.

Enzi za Mwalimu, sifa ya uongozi ilikuwa ni uwezo wa kuongoza na kipaji cha uongozi, yaani enzi hizo, uongozi ulikuwa more realistic than materialistic, utajiri ilikuwa ni sababu ya kukukosesha uongozi, lakini sasa uongozi ni more materialistic than realistic, mwenye nacho ndio anaonekana bora kuliko makapuku wasionacho, hivya kupata uongozi wa kuchaguliwa kwa siku za sasa, ni kwa mwenye kisu kikali, ndio anayekula nyama. Kwa kipimo kama hiki kwenye uongozi wa eneo husika, kupata kiongozi bora ni yule mwenye kipochi kinene kutatua shida zao, hivyo kwenye kuchagua ni kama kuchagua nguruwe, chagua aliyenona!.
Mimi na wish, wale wote wenye nia ya kuomba uwakilishi wa wananchi 2020, waonyeshe uwezo wa kudeliver kuanzia sasa, kwa kuonyesha uwezo kabla, ikiwemo uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, kama afanyavyo Diamond kwa kutoa mitaji sio wale wanaojipitisha pitisha majimboni kufanya matamasha, mara kuanzisha mashindano fulani fulani ili tuu to gain popularity, lakini maendeleo yao ni superficial, lakini huyu dogo, analeta maendeleo ya kweli yenye impact kwa wananchi haswa wa kipato cha chini!, ili uchaguzi wa mwaka 2020, hatutaki tena kuona chama kinanunua kura za ushindi kwa kugawa T-shirt na kofia!. Tunataka Bunge la 2020, lishehenezwe na wabunge wenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kwa kudeliver na sio mabingwa wa kupiga blah blah kwa maneno marefu, vitendo vifupi. 2020 we need people who can make changes and deliver those changes.

Faida nyingine, ya kuwa Mhe ni ile status ya uheshimiwa, unakuwa husumbuliwi kwenye mambo madogo madogo, ikiwepo kupatiwa diplomatic passport hivyo trips zake anapita VIP.
Mnalionaje hili?.
Nawatakia Furahi Dei Njema.
Paskali
Rejea za kuhusu Bunge letu, na Watanzania huwa wanachagua nini

Livingstone Lusinde, japo ni darasa la saba tuu, ni kichwa mbaya!, ana uwezo mkubwa na pia ana powers fulani!. - JamiiForums

Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?. - JamiiForums

Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?! - JamiiForums

Ikitokea CCM ishinde, Je ushindi huo ni kutokana kuwekeza kwenye Maendeleo au kwenye Ignorance? - JamiiForums

Watanzania ni ignorants au tumelogwa? October 25, tutafanya informed decision au tutachagua tuu? - JamiiForums

Umechoshwa na Ujinga, Umasikini, Maradhi, Rushwa na Ufisadi?!, 25/10 "Give It, "Just One More Try!" - JamiiForums

Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake? - JamiiForums
 
Wanabodi,
Kupitia Wasafi TV, nimeshuhudia mambo makubwa mazuri yanayofanywa na Mtoto wa Tandale, Diamond Platinums kwa wakazi wa Tandale na shule za Tandale
Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale - JamiiForums

Ikitokea wananchi wakamuomba awe mwakilishi wao kule mjengoni, kama ilivyo kwa Sugu na Prof. J, itambidi Mhe.Kubenea ajikalie tuu pembeni ampishe njia huyu dogo, ameonyesha uwezo, hivyo atakuwa kama Mo Dewji.

Mimi na wish, wale wote wenye nia ya kuomba uwakilishi wa wananchi 2020, waonyeshe uwezo wa kudeliver kuanzia sasa, ili Bunge la 2020, lishehenezwe na wabunge wenye uwezo wa kudeliver na sio mabingwa wa kupiga blah blah kwa maneno marefu, vitendo vifupi. 2020 we need people who can deliver.

Mnalionaje hili?.
P
Kubenea ni ovyo kabisa....
Kumbe kukopi kopi na kupaste habari za umbea ilikua njaa tu. Toka apate ubunge hana lolote.
 
Wanabodi,
Kupitia Wasafi TV, nimeshuhudia mambo makubwa mazuri yanayofanywa na Mtoto wa Tandale, Diamond Platinums kwa wakazi wa Tandale na shule za Tandale
Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale - JamiiForums

Ikitokea wananchi wakamuomba awe mwakilishi wao kule mjengoni, kama ilivyo kwa Sugu na Prof. J, itambidi Mhe.Kubenea ajikalie tuu pembeni ampishe njia huyu dogo, ameonyesha uwezo, hivyo atakuwa kama Mo Dewji.

Mimi na wish, wale wote wenye nia ya kuomba uwakilishi wa wananchi 2020, waonyeshe uwezo wa kudeliver kuanzia sasa, ili Bunge la 2020, lishehenezwe na wabunge wenye uwezo wa kudeliver na sio mabingwa wa kupiga blah blah kwa maneno marefu, vitendo vifupi. 2020 we need people who can deliver.

Mnalionaje hili?.
P

Kwa njia iliyo ' nyoofu ' kabisa hapa unamaanisha ya kwamba ' coming 2020 ' tunataka Wabunge ambao watafanya ' Walk the Talk ' na siyo wale wa ' Talk the Talk ' tuliowazoea na pengine sasa tunalekea Kuwachoka kama siyo kwamba tumeshaanza Kuwakinai na Kupata Kichefuchefu nao vile vile.
 
Wanabodi,
Kupitia Wasafi TV, nimeshuhudia mambo makubwa mazuri yanayofanywa na Mtoto wa Tandale, Diamond Platinums kwa wakazi wa Tandale na shule za Tandale
Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale - JamiiForums

Ikitokea wananchi wakamuomba awe mwakilishi wao kule mjengoni, kama ilivyo kwa Sugu na Prof. J, itambidi Mhe.Kubenea ajikalie tuu pembeni ampishe njia huyu dogo, ameonyesha uwezo, hivyo atakuwa kama Mo Dewji.

Mimi na wish, wale wote wenye nia ya kuomba uwakilishi wa wananchi 2020, waonyeshe uwezo wa kudeliver kuanzia sasa, ili Bunge la 2020, lishehenezwe na wabunge wenye uwezo wa kudeliver na sio mabingwa wa kupiga blah blah kwa maneno marefu, vitendo vifupi. 2020 we need people who can deliver.

Mnalionaje hili?.
P
dah Pasco njaa mbaya sana. Yani thread zako siku hiz za kusifu sana. You are a proffesional social climber and a nitorious gold digger aliyekubuhu. Una weledi wa haliya juu ya kuwini wadau kisaikolojia.Njaa imekubana umeamua utoke sasa hivi kwa taaluma yako.

FANYA KAZI ACHA POROJO
 
Wanabodi,
Kupitia Wasafi TV, nimeshuhudia mambo makubwa mazuri yanayofanywa na Mtoto wa Tandale, Diamond Platinums kwa wakazi wa Tandale na shule za Tandale
Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale - JamiiForums

Ikitokea wananchi wakamuomba awe mwakilishi wao kule mjengoni, kama ilivyo kwa Sugu na Prof. J, itambidi Mhe.Kubenea ajikalie tuu pembeni ampishe njia huyu dogo, ameonyesha uwezo, hivyo atakuwa kama Mo Dewji.

Mimi na wish, wale wote wenye nia ya kuomba uwakilishi wa wananchi 2020, waonyeshe uwezo wa kudeliver kuanzia sasa, ili Bunge la 2020, lishehenezwe na wabunge wenye uwezo wa kudeliver na sio mabingwa wa kupiga blah blah kwa maneno marefu, vitendo vifupi. 2020 we need people who can deliver.

Mnalionaje hili?.
P
Ni Kati ya mawazo ya kijinga zaid umewai kua nayo humu jamvini
Bunge linawajibu wa kuisimamia serikali,kutunga Sheria kupitia miswaada Na shughuli nyingine.
Kigezo cha mtu kusaidia jamii co sifa ya mtu kua mmbunge bunge linatakiwa liwe Na wasomi wenye weledi Na wanaoipenda nchi yao km tukiendelea kuchagua wawakilishi kwa pre-hongo,pre-takrima Na nduguzake uwakilishi wa wananchi utakua haunamaana Bora ilo bunge lifutwe kabisaa.
 
Back
Top Bottom