Uchaguzi 2020 Kwa mambo haya 10, mimi kama Mtumishi wa Umma (mwalimu), John Pombe Magufuli sikupi kura yangu asilani

You are crazy for accepting tsh 7800 from lumumba
 
Nikuwekee check number yangu ya nini kama huamini endelea kuamini falsafa za kinyumbu kwamba ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa ndege, ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati havina manufaa kwa watu.
Wewe endelea tu kutumikishwa na hao walio kuweka hapo Lumumba. Siku akili yako ikikukaa vizuri utanielewa tu nilichomaanisha. Yaani Uvccm tu eti unajiita mtumishi wa umma!
 
Mwalimu Mwenzangu wewe nimuongo sana tumeongezewa mshahara mwaka huu
Wewe umedanganyika kirahisi sana, haujaongezewa mshahara, isipokuwa umepunguziwa Kodi kidogo,(basic salary yako ipo vile vile) na madhara ya hiyo kitu ni kwamba, michango yako ya mifuko ya hifadhi ya jamii haijaongezeka hata mia moja, na kuongeza kodi ni swala la sekunde tu, lakini angeongeza basic salary kupunguza ni ngumu!

Mchagueni tena muone kundi la watumishi masikini litakavyoongezeka kwa kasi...
 

Ripoti ya CAG inasemaje kuhusu CCM na CDM. Tuanzie hapo ili kupata chama bora kupewa nchi.

Pia CCM iweke wazi inakopata hela za kujengea majengo ya kisasa na magari ya kifahari etc

Hakika naapa, CCM sheria ya utakatishaji fedha inaihusu. Mbele ya chombo huru cha uchunguzi, CCM haina uwezo wa kuelezea chanzo chake cha mapato kilicho halali mbele ya sheria.
 
Nyie ndio ccm wajinga jiwe anaowahitaji
 
Wapo walimu kibao watampigia wanaipenda CCM na JPM wewe kura yako moja haitabadili kitu!
Ulitakiwa kujibu hoja kwa vipengele ... sasa haya mambo ya kulazimisha kumpigia kura mtu huku mkilazimisha apendwe hayapo tena, mapenzi kwa mgombea yatoka moyoni sio kulazimishana hatumpi kachemka

Tunapiga na kumpa mgombea kura kulingana na sera na ahadi sio kwa mapenzi ya kulazimisha wapumbavu mmeng'ang'ania miundo mbinu, flyover, ndege ... matatizo kama hayo ya waalimu ndio vitu vya kipaumbele ili kuboresha maisha ya watu na sio vitu

#NI YEYE TU 2020 !!!
 
Kwa nyongeza tu kuonyesha ubabe na ukatili wa JPM, baada ya sheria mpya ya bodi ya mikopo iliyopitishwa makato ya asilimia 15 kutoka 8, kuna watumishi wanapokea mshahara hadi elfu tisini kwa kuwa walikuwa wamekopa kwenye benki kabla huku wakiacha 1 ya 3 kama sheria inavyohitaji, kwa lugha rahisi sheria mpya ya bodi ya mikopo imekiuka hata miongozo wa mtumishi kubaki na kiasi cha moja ya tatu baada ya makato!
 
Wewe sio mwalimu ni kanjanja tu!
 
Duuu umeandika kwa Uchungu,poleni walimu jmn.Hapo bado makundi mengine hapo hayajatoa kero zact.28 kampeni delete CCM#Twendeni tukapige kura.
 
Kila siku watu wanakilmbilia ualimu wanapenda .ualimu ni wito
Hii kazi yako ni ya "wito" pia?
Bila shaka anayekulipa kwa kufanya kazi unayofanya hapa jukwaani siku si nyingi ataona pesa yake imepotea bure. Utakuwa huna kazi tena.
 
Huoni hata aibu?
Hebu linganisha tu hata uandishi wako na wake..., hata hili hujui ninachoandika hapa?
 
Mkuu umeongea kwa hisia kali...pole sana.

Watanzania wamekusikia na watakuunga mkono wiki ijayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…