Kwa madudu anayoanika CAG, kumbe Magufuli uongozi wake ulikuwa sifuri tu

Huu utawala wa jiwe ulkua wa hovyo Sana.

Machale yaliaanza kunicheza kwa ile tabia yake ya kutembea na maburungutu ya pesa anagawa.

Nikajua, Kuna kitu hakiko sawa nchi hii.
 
Kwa mifumo iliyopo Tanzania hata rais awe Tundu Lissu, Makamu Lema, Waziri Mkuu Mbowe, Waziri wa mambo ya ndani Sugu, IGP Mnyika, CDF Yeriko Nyerere, Waziri wa Katiba Msigwa, Mkuu wa TAKURURU Heche, CAG Zitto, Uchumi Lipumba, Madini Mbatia.... madudu yataendelea tu. Ni falsafa ya Mtanzania kuwa akipata madaraka ni lazima aibe; na asipoiba akaja kuondoka madarakani hana kitu jamii hiyo hiyo inamgeuka na kuanza kumcheka na kumuita mshamba huku mafisadi yakitukuzwa kwa kuitwa matoto ya mjini, majoka makengeza....

Na kubadili falsafa ya jamii, kujenga mifumo imara na kuleta mwelekeo mpya wa jamii ni suala la muda mrefu na lenye kuhitaji vizazi kadhaa. Nyerere alijaribu sana katika hili lakini tatizo ni kwamba kumbe hata yeye alikuwa peke yake. Alipoondoka akaondoka na falsafa zake japo yeye mwenyewe alikuwa mwadilifu kabisa kabisa. Hata watu aliowaamini sana kama mwanafunzi wake Ben na komredi Kingunge nao wakaja kumgeuka na kuwa wapigaji tu. Kwa hivyo haitoshi tu kiongozi kuwa mchapakazi na mwadilifu, bila kubadili mifumo na fikra za jamii ni kazi bure.

Kwa hali ya sasa, Tanzania hii hata atawale nani (ukiwemo wewe mwenyewe), madudu na upigaji vitaendelea tu. Na ukijifanya wewe ni mkali, utakuwa na maadui wengi wa ndani na nje; na ukizubaa unaweza hata kuuliwa.

Mwendazake alijaribu sana. Tena kwa ukali mno lakini wapi. Upigaji uliendelea tu japo pengine ulipungua kidogo na ulikuwa unafanyika kwa kujificha ficha kidogo na siyo waziwazi kama kwa watangulizi wake.

Ni rahisi kuongea kishabiki kuhusu haya mambo lakini ukiyaangalia kwa undani wake ni mazito na yenye kusikitisha sana!
Sasa unashauri Nini kifanyike mkuu
 
Wakuu na wadogo wa JF.

Ukisikia hbr ya CAG juu ya jinsi pesa ya serikal inavyotafunwa kupitia watendaji wasio waaminifu kumbe JPM yalikuwa maneno tu na hakuwa na Sumu.

Sina kumbukumbu kamili kama miaka 6 ya jiwe CAG alikuwa anasoma Ukaguzi wake open kama inavyofanyika leo.

Kwa haraka 40% ya pesa ya serikal ilikuwa inaibiwa na wafanya kazi.

Na watu walimuogopa JIWE kipindi cha mwanzo lakini baada ya hapo wizi ulikuwa wa kutisha.

Ukisikia taarifa ya CAG utaona wazi kuwa katika kuthibiti mapato serikal ya JIWE haikumudu hata asilimia 50.


MAMA yetu kipenzi ana kila sababu ya kukaa na kamati wabuni mfumo wa kuthibiti wizi huu zaidi ya hapo TZ ni shamba la BIBI.

Pia nashauri MAMA AUNGANE NA KIDUKU KIM WA KOREA KUHUSU SHERIA ZAKE UKILA KUANZIA MILIONI 1, TUNYONGE TU HAKUNA NAMNA.

Mizizi ya Tz kuhusu,wizi kwa watendaji haiwezi kuisha kwa hali tu tuliyofikia kwa sheria zetu hizi lege lege.

Nasikia KAGAME amekomesha kabisa wizi cjw alifanyaje.

Nimeanza kuamini kumbe JIWE kuondoka inawezekana ni mpango wa SIR GOD mtenda haki.

Sifurahi kifo chake lakini tulifichwa mengi.

MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU MBARIKI SSH RAIS WETU MPYA.
Taarifa ya CAG ilianza kusomwa hadharani enzi za utawala wa JK (kama sikosei) na kabla ya hapo taarifa taarifa hiyo ilikuwa ni miongoni mwa siri za serikali.

Lakini tukiachana na hilo ukweli ni kuwa siyo kasoro zote zinazobainishwa na ukaguzi wa CAG ni ukweli halisi, kwani taarifa ya CAG inahusu hali ya ukaguzi ilikutwa wakati husika wa ukaguzi, wakati ambapo michakato ya nyaraka nyingine za miamala ya matumizi ya fedha huwa haijafikia tamati, hivyo kusababisha pamoja na mambo mengine, kukosekana kwa risiti za malipo ya miamala hiyo. Kwa jicho la kikaguzi huo unahesabiwa kuwa ni wizi au ukiukwaji wa kanuni za matumizi ya fedha za umma, hadi hapo risiti za kusupport miamala hiyo wazione, na kwa hakika nyaraka nyingi za kusupport miamala hiyo hupatikana, licha ya awali kuonekana kuwa ni wizi.

Sio nia yangu kujenga hisia kuwa hakuna wizi au matumizi mabaya ya fedha za serikali, la hasha. Wizi upo, tena ulikuwepo katika zama zote za utawala tangu awamu ya Baba wa Taifa, na utaendelea kuwapo, baada ya uongozi wa awamu ya sita, licha ya uongozi katika kila awamu kutunga sheria na miongozo mbalimbali na kuwa na utashi wa kudhibiti mianya ya upigaji.

Na kwa nchi zilizojitahidi na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti wizi na matumizi mabaya ya maduhuli ya serikali, kwa maoni yangu zilifanikiwa kwa sababu viongozi wao walikuwa na Uthubutu na kuwa na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi, kulingana na utashi wao, na hawakuwa tayari kuiga ama kufuata mkumbo wa sera na tamaduni kinzani za kigeni.

Viongozi wa Nchi kama Rwanda, China, Korea Kaskazini, au Libya ya Muamar Ghadaffi waliongoza kwa kutumia 'mkono wa chuma"; mkono usio sikia la mtu; mkono ambao haukushabikia kitu kinachoitwa 'demokrasia', katika kutekelza malengo pangwa; Udikteta wenye kuumiza baadhi ya watu kwa manufaa mapana ya umma; udikteta uliothamini na kuenzi uadilifu, uzalendo na haki ya nchi kujiamulia yenyewe na kunufaika ipasavyo kutokana na utajiri wake wa raslimali asili.

Hayati John Pombe Magufuli, licha ya mapungufu yake mengi kama ilivyo kwa binaadamu wengine, ni miongoni mwa viongozi wachache waliokuwa na maono kama hayo.

Kwa muda wa miaka takriban sita tu, ameacha alama kubwa, nchini, barani Afrika, na duniani kote, mambo ambayo watangulizi wake hawakuweza kuyafanya katika awamu zao.
Ni matumaini yangu kuwa Mama Samia Suluhu Hassan atafuata nyayo, huku akirekebisha mapungufu ya dhahiri au ya ghaibu yaliyofanywa na mtangulizi wake, katika jitihada zake za kuwatumikia watanzania, hususan wa maskini, ili naye atakapoondoka naye aache alama iliyotukuka, na aweze kuchaguliwa tena ifikapo 2025. Anaweza.
 
Mla nchi, ni mwananchi. Nikiwa darasa la saba kwenye mtihani wa kujipima pale shule ya msingi Mwere, Morogoro, niliikosa hii methali kwenye mtihani. Mwalimu alinilaumu sana!
Duhh aisee mwaka gani umemaliza mwere
 
Wakuu na wadogo wa JF.

Ukisikia hbr ya CAG juu ya jinsi pesa ya serikal inavyotafunwa kupitia watendaji wasio waaminifu kumbe JPM yalikuwa maneno tu na hakuwa na Sumu.

Sina kumbukumbu kamili kama miaka 6 ya jiwe CAG alikuwa anasoma Ukaguzi wake open kama inavyofanyika leo.

Kwa haraka 40% ya pesa ya serikal ilikuwa inaibiwa na wafanya kazi.

Na watu walimuogopa JIWE kipindi cha mwanzo lakini baada ya hapo wizi ulikuwa wa kutisha.

Ukisikia taarifa ya CAG utaona wazi kuwa katika kuthibiti mapato serikal ya JIWE haikumudu hata asilimia 50.


MAMA yetu kipenzi ana kila sababu ya kukaa na kamati wabuni mfumo wa kuthibiti wizi huu zaidi ya hapo TZ ni shamba la BIBI.

Pia nashauri MAMA AUNGANE NA KIDUKU KIM WA KOREA KUHUSU SHERIA ZAKE UKILA KUANZIA MILIONI 1, TUNYONGE TU HAKUNA NAMNA.

Mizizi ya Tz kuhusu,wizi kwa watendaji haiwezi kuisha kwa hali tu tuliyofikia kwa sheria zetu hizi lege lege.

Nasikia KAGAME amekomesha kabisa wizi cjw alifanyaje.

Nimeanza kuamini kumbe JIWE kuondoka inawezekana ni mpango wa SIR GOD mtenda haki.

Sifurahi kifo chake lakini tulifichwa mengi.

MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU MBARIKI SSH RAIS WETU MPYA.
Wewe hujawahi kusoma ripoti za CAG. Ungekuwa unazisoma hungeweza kuanzisha thread kama hii kwa kufuata snippets za headlines tu kwa CAG agundua "madudu". Hata hii ya sasa ni wazi hujaisoma ila unongelea hayo ya mitaani tu.

Ripoti zote za CAG ziko hapa https://www.nao.go.tz/index.php/reports/category/ripoti-kuu-za-ukaguzi

Zimekuwapo kwa miaka yote kuanzia mwaka 2011 hadi 2020, hazijawahi kuzuiwa kuwekwa; hii ya mwaka huu haijawekwa kwa hiyo subiri uje uisome ndipo utoe maoni. Ya mwaka jana ni hii hapa pamoja na ambatatisho lake. Mkaguzi hutoa hati za aina nne: hati zinazorithisha, hati zenye mashaka, hati zisizoridhisha na hati chafu. Hati zisizoridhisha na hati zenye mashaka hasima maana ya wizi au upotevy, huwa zina maana ya taratibu za kutunza mahesabu kuwa zimekosewa, hati chafu ndizo zile zenye upotevu wa pesa. Miaka yote hati chafu huwa ni kkati ya 2% mpaka 5% tu.; hataa mwaka huu utakuta ziko kwenye range hiyo hiyo. Ukipitia majendwali unakuta hati chafu nyingi huwa zinatokana na ama kuchelewa kulipa madeni na hivyo kulazimika kulipa zaidi ya kiwango kilichotegemewa, kujenga miradi kwa kwa kutumia tathmini isiyo sahihi inayoonyesha gharama ndogo za ujenzi, na kumbe wakati wa ujenzi gharama zake halisi zikwa juu zaidi ya bajeti iliyokuwa ikitegemea. Ni sehemu ndogo sana inayoonyesha matumizi mabaya au hata kushukiwa wizi.

halafu CAG kazi yake kubwa na kutafuta makosa kususdi yashughulikiwe kwa hiyo anapopata hata makosa machache tu, hayo ndiyo atakayoripoti na kuyatolea mapendekezo. mwaka juzi tulitangazazi hapa na wapiga porojo kuwa kuna pesa trilini 1.5 zimeibiwa kumbe sa kweli, na ripoti ikiwa wazi kabisa hata unashangaa huyo alikuja na taarifa hiyo ya trilioni 1.5 aliitoa wapi. Wewe neda kwenye hiyo website pakua ripoti zote uzisome kwa makini, halafu subiri hii nayo ikishawekwa isome ndipo utoe maoni
 

Attachments

  • SERIKALI_KUU_KWA_MWAKA_WA_FEDHA_2018-2019.pdf
    5.2 MB · Views: 3
  • MASHIRIKA_YA_UMMA_KWA_MWAKA_WA_FEDHA_2018-2019.pdf
    2.9 MB · Views: 3
  • MIRADI_YA_MAENDELEO_KWA_MWAKA_WA_FEDHA_2018-2019.pdf
    1.4 MB · Views: 2
  • MAMLAKA_ZA_SERIKALI_ZA_MITAA_KWA_MWAKA_WA_FEDHA_2018-2019.pdf
    5.8 MB · Views: 2
Ndiomaana alikua anahangaika na kufungia wanaharakati na vyombo vya habari ili uozo wake usijulikane yaani kaaibika hata hajaoza vizuri shwenzyyy
Kwahiyo Watumishi Wa Umma miaka 5 bilabila no nyomgeza ya Mshahara,madaraja,increment kumbe ndiyo hela tulikuwa tunawalisha wahuni hawa siyo? Mama tuangalie waja wako
 
Najua unapenda kutukana na kukashifu wengine. Hiyo ni haki yako japo ingependeza mno kama pia ungeheshimu maoni ya wengine kwa sababu nao wana haki ya kutoa maoni yao sawa tu na wewe. Hapo hata sijui Usukuma unaingiaje kamanda.

Mimi sipo katika ushabiki wenu huu wa kisiasa uliopitiliza kwa sababu hautufikishi po pote wala kutusaidia cho chote. Kama mifumo ni hii hii, na taasisi zetu ni hizi hizi legevu hata uje wewe mwenyewe uwe rais tutaendelea kupigwa tu. Hiyo ndiyo hoja yangu ya msingi. Hata kwa huyu mama tutaendelea kupigwa tu...na atakayekuja....na ajaye...na mwingine...

Mpaka lini?
Sawa,ila la kushukuru ni kuwa dhalimu is no more
 
Jiwe alikuwa ni muhuni tu pia mwizi na jambazi aliyeliibia Taifa letu kuliko mtu mwingine yeyote yule. Na yule mwizi mwenzie Dotto James anajua wizi wao wote tangu 2015 hadi anafariki.
Dotto siku zake zinahesabika...

Mama asipomzingua, sisi tutamlilia Mungu kama kawaida yetu
 
Sawa,ila la kushukuru ni kuwa dhalimu is no more
Good. Let's celebrate with a nice dinner, if that is cathartic to our tortured and tired psyche



IMG-20210405-WA0022.jpg
 
Ndiomaana alikua anahangaika na kufungia wanaharakati na vyombo vya habari ili uozo wake usijulikane yaani kaaibika hata hajaoza vizuri shwenzyyy
Usimtukane Marehemu,yeye alishafanya kwa sehemu yake,waliobaki nao wafanye sehemu yao.
 
Back
Top Bottom