kwa kutumia taaluma ya kawaida ya masuala ya afya hiyo haiwezekani kama tarehe aliyo taja ni sahihi, japo naami huenda amekosea tarehe kwa mshutuko alioupata. Usiwe na hasira au haraka ya kugombana nae, nenda kawaone wataalamu wa afya ya uzazi katika hospitali zinazotambulika utapewa majibu ya mtoto ni wako au la na utaimaliza hiyo kesi kirahisi sana. Kwanza punguza hofu za kuogopa kuwa baba ni jambo la kawaida katika maisha na pili kama nilivyo kushauri hapo juu ndenda hosipitali kupata ukweli achana na mahesabu ya ni lini alipata hedhi mabadiliko madogo ya mwili yanaweza kuharibu kabisa huo mzunguko unao uhesabu.