Mkuu Kaumza,
Me nimekubali sana hayo maandishi yako umeelezea vizuri sana kuhusu Lowassa, na kama hao Wapinzani wake wanasifa kama zake mbona hatuzioni, Jamaa Jembe, Nlikuwa namuuliza jamaa yangu Membe amefanya kipi katika nchi hii kinachomfanya aone anasifa ya kuwa rais ila jamaa alichoniambia ni kuwa eti ni kwa sababu ni waziri wa mambo ya nje na hivyo anasifa ya kuwa rais, tukumbuke kuwa alikuwa naibu waziri wa Migiro so ambaye tungetarajia kutajwa ni Migiro na si yeye kwani yeye hata unaibu aliupata kwa uswaiba na pengine undugu na mukulu ila leo kifua mbele naye urais anautaka.
My take, kama CCM wanaitaji kweli chama kiwe imara ni kwanza kuondoa ukasuku, wivu, fitina na unafiki baina ya viongozi wake. Nasema hivi kwa sababu kwa mtu makini anaweza kung'amua ya kwamba anayeharibu CCM ni wanaccm wenyewe tena viongozi waandamizi ambao wametanguliza maslahi yao mbele kuliko ya chama.
Kumza, ni kitu cha ajabu sana leo kuona kiongozi wa ccm akimwita mwenzake fisadi tena bila uthibitisho ila kumbe nyuma ya pazia ana agenda binafsi.. Yaliyompata Edward yalipangwa na wahusika wanafahamika na hii imekuwa laana hata kwa serikali ya Jakaya, wote tunakumbuka wakati Edu akiwa waziri mkuu spidi ya maisha bora ilionekana ila baada ya kuondoka mambo yakapwaya.
Kingine ni urafiki wa mashaka kati ya Mukulu na Edu kuna kila dalali hawa jamaa hawaelewani, na hii inaonyesha wazi kuwa yale maneno ya Edu aliyoyatoa NEC yanaukweli kuwa hausiki na Richmond na kwanda alishamwambia rais wavunje mkataba ila akasema wavute subira...inawezekana kabsa kwamba muhusika bado yu ndani ya serikali.
Lowassa ni Jembe, anayesema mla Rushwa toa ushahidi kila aliyewahi kufanya naye kazi anamsifia na kila ambaye ameuona utendaji wake unavuta, ni mvumilivu si mropokaji kama wapinzani wake...AKIGOMBEA NITAJITOA MIA KWA MIA KUMPIGIA KAMPANI BUREEEEE.....KWA MANA I AM SURE HE GONNA PROVE PEOPLE WRONG, VIVA EDWARD LOWASSA