Kwa Lipi Wazanzibari Mumuenzi Mkapa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Lipi Wazanzibari Mumuenzi Mkapa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jun 4, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkapa roads zanzibar,
  Moja inatokea njia ya Amani kupitia Darajabovu mpka Bububu, hii aliifungua Mkapa na inaitwa Mkapa road.
  Nyengine inaotokea Kisiwandui kuelekea Michenzani pia inaitwa Mkapa road.
  Haikutosha kuna Shule ya walimu kisiwani Pemba inaitwa Benjamin W. Mkapa.
  Mbali na utitiri wa vibanda vya kupiga soga vinavyoitwa "maskani za chama, vilivyotapakaa katika vichochoro mbalimbali vya Manispaa ya zanzibar ambavyo vingi tu vinaitwa kwa jina lake.
  "Maskani ya Mkapa" linasomeka bango moja lililotundikwa katika moja ya vibanda hivyo katika eneo la Darajani.
  ukiuliza. Jibu ni kuwa ni kumuenzi Mh. Mkapa kwa blah blah blah...
  Hapana tatizo kumuenzi kiongozi, tatizo ni kwa lipi kiongozi huyo aenziwe?
  Kwa mtu kama Mkapa anaenziwa kwa lipi zanzibar?
  kwa kuwachagulia wazanzibar mtu wa kuwaongoza asiechaguo lao?
  Kama amiri jeshi mkuu, kusabisha mauwaji ya kutisha Jan 27/01, kwa raia wasiokuwa na hatia?
  Hivi?! Hakuna watu walioifanyia makubwa zanzibar wakastahili kupewa majina ya barabara na shule hizo?
  Basi hata Aboud Jumbe Mwinyi hana hata kichochoro au kibanda cha kuuzia urojo kilichopewa jina lake?
  Au J.Okello, kahatarisha uhai wake 1964 kwa kuifurusha madarakani serikali halali ya wazanzibar, hata ile kambi ya "janjaweed" ya kule Hanyegwamchana, haijapewa jina lake? is it fair kweli?
  Nani katika vitoto vya siku hizi zanzibar vinamjua Abdulrahman Mohammed Babu? dunia inamjua wazanzibar wenyewe hawamjui! shame.
  Wapi pana kumbukumbu ya maulamaa na wasomi wa zanzibar kama akina Omar bin Sumeit ambao nchi za n'gambo hukoo zimeweka kumbukumbu zao lakini kwa zanzibar walipotokea na kutoa utumishi wao uliotukuka hawana alama yoyote.
  Nani katika vizazi vya leo anamfahamu kanali Ali Mahfoudh(jamadari), hukoo Msumbuji wanamuimba na kumuenzi kwa mchango aliotoa kwa FRELIMO katika mapambano na wakoloni, kwao zanzibar kitovu chake kilikozikwa, hakuna hata uwanja wa kuchezea judo uliopewa jina lake.
  Ipo wapi alama ya mwanasiasa SK. Ali Muhsin Barwan(zaim)aliemfunza Nyerere "the saint", siasa ya usawa na umoja wa kweli wa Kiafrika kule Ghana 1950s,japo ile skuli ya kidongo chekundu ingetosha kumuenzi.
  Si sawa hata kidogo kuona kuwa mashujaa wote hawa na wengine ambao sikuwataja hapa waliofanya mengi ya kustahali kuenziwa katika uhai wao wote visiwani alama zao zinapotea na vizazi vya leo haviwajui, na badala yake wanakuja watu wa siku mbili tatu na udhalimu juu, wanaekewa alama za kuwakumbuka milele.
  Hata Mungu hayupo radhi na ndo maana wanasibika sasa.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa kumbukumbuku zangu karibu viongozi wote walioshika madaraka ya juu huko Zenji wanakumbukwa katika barabara chache za visiwani humo.

  Kazi ya kutoa majina kwa barabara hizo hufanywa na Kamati ya Mipango Mji ya Baraza la Manispaa(Jiji) Zanzibar, baadhi ya barabara nazukumbuka kupatiwa majina mapya katika miaka ya tisini ni kama hizi
  • Barabara ya Creek(inatoka Malindi kupita Darajani na kuishia Mnazi mmoja)- Benjamin Mkapa
  • Kutoka Kinazin kwenda Bububu- Aboud Jumbe
  • Kiembe Samaki hadi Amani- Idrisa A. Wakili
  • Mnazi mmoja- Airport- Nyerere
  • Mkunazini hadi Kariakoo - Karume
  • Maisara - Michenzani kwenda Mlandege- Dr. Salmin
  • Ule Uchochoro wa Darajani hadi Mlandege- Ali H.Mwinyi
   
  Last edited: Jun 4, 2009
 3. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kibandamaiti kwenda mchambawima - Mwanakijiji
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyo mwisho wake ni Chumbe
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mbona Karume bara kuna Viwanja vya Mpira na shule kibao za kumbukumbu??

  Kuna ubaya gani Mkapa akakumbukwa kwa kabarabara kamoja huko visiwani?

  Mimi sipendi mtu aliye hai sehemu kupewa majina..haitoi picha nzuri! Nivema kwa nyerere au Karume marehemu..ila sasa kuna haja gani raisi anajenga daraja la Mkapa(wajibu wake)..halafu hilo daraja linaitwa jina lake?
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mzalendohalisi,
  kuna maeneo matatu yamepewa alama ya jina la Mkapa zanzibar, sujui kwa lipi kubwa mpaka akawa shujaa wa kukumbukwa kiasai hicho wakati zanzibar ina mashujaa wamefanya na kuifanyia makubwa zanzibar alama zao hazijuulikani au zimewekwa katika maeneo si maarufu, watu hawazijuwi hasaa.
   
Loading...