Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

huyu mtu ni mtu wa kawaida tu kwanza mm namuona hana historia yoyote zaidi ya wizi na ukimuona mtu anamshabikia huyu mtu ujue na yeye ni mwizi au ni tapeli sana cha maajabu huyu mtu ndio anataka kuja kuwa rais kwa misingi ipi na atatusaidia nini wakati hajawahi hata kupata shida hajawahi hata kulala na njaa yule ni mtu ambaye amekulia kimayai alafu leo anataka awe rais kiraisi raisi tu kwanza mtu mwenyewe yule mgonjwa isije ikwa kama zambia raisi anakaa mwaka 1 harafu anakufa watanzania makosa ambayo walifanya wazee wetu sisi haitakiwi tuyarudie
 
yule mtu na ninapenda nimuite ni mtu kwasababu hana ubinadamu yani mtu aliiba hela zote zile anafikiri tumesahau alafu leo anataka tumpe kula awe raisi au anafikiri hii nchi ni ya baba yake
 

Uko sahihi
Na hayo maagano ndo yanatu cost Sana,ndo maana inakuwa ngumu ht kupata maendeleo.....
Ni ushetani tu....Mungu atusaidie
 
Watanzania watu wa ajabu sana.huyu lowasa anajulikana wazi anavyotoa rushwa ili achaguliwe chaa ajabu bado kuna watu wanamshabikia kama mataahira.
 
Nikukumbushe: Labda nikuulize tu mkuu kuwa, hv kama EL hafai kwa ajili ya ufisadi ni nani anayefaa kwenye Manyinyiem? Manake wote hakika wameoza tena ile ya kabisa. Ni nani msafi huko????? EL afadhali zaidi manake alibeba mizigo ya watu na inafahamika hivo.
 

sasa kama alibeba mizigo mnamtaka mumgeuze mwenzenu Kuli? Acheni dharau muacheni apumzike ale mafao yake. Si waziri mkuu mstaafu yule? (Watanzania mlivyo matapeli et mnamuita hivyo)
 
Bwana Lowasa aliyejiuzulu uwaziri Mkuu -kwa tuhuma za ufisadi wa Richmond na sasa hivi ana utajiri wa mali na pesa kupindukia-mali na pesa ambazo hazielezeki chanzo chake-hastahili kuwa Rais wa nchi hii.

Hata Mwalimu Nyerere aliyekuwa bosi wake enzi hizo naye aliwahi kuhoji utajiri wake

Akiwa Rais hizi Pesa nyingi anazozitumia kujenga mtandao wake na kujiaminisha kwa taasisi mbali mbali zikiwemo za dini lazima azirudishe.

Watu wengi mnaomshabikia Lowasa ni kwa sababu ya ubinafsi Wa kupewa pesa mkiwa kwenye mtandao wake. -Lakini mfahamu kwamba akiwa rais ufisadi utaendelea kung'ata watanzania wenzenu wakiwemo ndugu zenu.

Kwa ufupi Lowasa akipewa nafasi ya kushika madaraka ya urais kazi yake kubwa -itakuwa ni kujenga himaya yake ya kifisadi badala ya kujenga nchi.

Hapa nachojiuliza ina maana CCM haina mtu mwigine anayeweza kuwa rais zaidi ya Lowasa?
 
CCM kwisha habari yake, Inaonekana Hakuna watu wenye uwezo Wa kuwa rais
 
Ni tanzania pekee wasomi wanaweza kumshabikia fisadi wa kutupa, ashukuru nyerere katangulia mbele ya haki wamebaki wazee mafisadi kama kingunge hawawezi kukemea maovu kwa sababu wamechafuliwa na ufisadi ndio maana watu kama lowasa wanapata nguvu ya kununua uraisi kwa pesa za aibu. Eti wanafunzi wanaandamana kumtaka lowasa agombee uraisi hakuna kitu ni njaa zao tu mbona wasishabikie watu waadilifu kama jaji warioba na wengine aibu sana kwa taifa hili changa
 

Hivi wewe tukikuuliza JK alipewa nchi kwa lipi alilofanya utajibu nini???
 
Angalia hatari tuliyonayo,JK alikataliwa na Mwl Nyerere angalia alivyoligawa taifa. Lakini watz kwa upumb,avu wetu tukampa urais, umeona matkeo yake? Hatuwezi kumpa urais mtu aliyekataliwa hapa tunaongeza laana maradufu.
Hivi wewe tukikuuliza JK alipewa nchi kwa lipi alilofanya utajibu nini???
 
NAPENDA KUNUKUU MANENO YA MAREHEMU PROF.SAITOTI WA KENYA." IT WILL BECOME A TIME WHEN THE NATIONAL WILL BE IMPOTANT THAN INDIVIDUAL.PROVE ME IN THE NEAR FUTURE" nataka kujibu hoja inayomhusu Riz.Pili swala la kusema LOWASSA fisadi nachelea kushangaa wanamgopa nn wasimpeleke mahakamani kama akina Mramba? Tatu nani aliye kuwa Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri wakati LOWASSA ni PM kwani huwezi kuagiza mitambo kama ya Richmond bila baraza la Mawaziri kujuwa! Lingine swala la utajiri kwa yule anayehoji labda ana upofu mbona wengi wameingia madarakani hawana kitu Leo wanatoka Matrillionea? Falsa ya baba wa Taifa ya Ujamaa na kujitegemea hakuna tena.Tusidanganyane kabisaaaaaa! Tumechoka na umasikini gape ya waliyonacho ni kubwa sanaaaa kuliko wasiokuwa nacho.
 
wallahi mtoa mada umelogwa wewe sio bure. Kamwambie awe rais wa kale kafamilia kenu pale lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…