Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Mnarudia rudia sana yale yale!Kimsingi jamaa yenu amekwisha kwama!
 

acha kero, acha kurefusha uzi bila sababu za msingi.
 
 
hakuna kazi aliyotenda zaidi ya kuchakachua..... apumzike tuu.
 
Maamuzi ya kuanzisha shule za kata zisizokuwa na uwezo wa kutoa elimu?

Wazo la hizi shule lilitoka kwa mzee Cheyo,,,,

Huyo jamaa wala hayuko huko
..


yeye na richmond tu
 
 
 
nimeshtushwa na wazee wa sebule kuu.
Ni mchana huu baada ya kuhudhuria lunch ''majris''.
Namnukuu mmoja wao.
''safari hii ni zamu ya wakristu.akafinyanga tonge....
Na katika wakristu lowasa tunamkubali.......akameza.......
Maana ameshatuweka sawa.''kimya.......
Nilisikia kizunguzungu na biriani yoote ikayeyuka.
Nikajikausha, kama sijasikia..........
Huyoo nikaosha mikono nikasepa.
 
[h=2]Lowassa ageuzwa mtaji[/h]

Na Mwandishi Wetu

KUONGEZEKA kwa idadi ya watu wanaokwenda kumtembelea mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwa madai ya kwenda kumshawishi agombee urais, inaelezwa wanafuata kiasi kikubwa cha posho wanachopata kutoka kwa mbunge huyo ambaye anawania urais.

Jana mbunge huyo alipokea watu zaidi ya 715 kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao inadaiwa walikwenda kumshawishi agombee urais, ingawa inaelezwa watu hao walilipwa posho na kuponda raha ndani ya jimbo hilo kwa gharama za Lowassa.

Kwamujibu wa kada mmoja wa CCM ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara huo alisema, kabla ya kufikia makubaliano ya kuanza safari ya kwenda Monduli, kila aliyekubali kufanya kazi hiyo, aliahidiwa posho ya shilingi 150,000 ambayo walilipwa baada ya kufika jimboni humo.

Kada huyo ambaye alikuwa mmoja wa walioandaa msafara huo, alisema pia waliandaliwa malazi na kila mmoja alitakiwa kuhakikisha analala kwenye hoteli inayogharimu shilingi 25,000, huku akitakiwa kutumia vinywaji visivyozidi shilingi 40,000 kwa siku tatu watakazokaa Monduli.

Aidha, ndani ya kundi hilo kulikuwa na wazee 15 ambao kila mmoja alilipwa shilingi 300,000, huku bajeti ya mafuta kwa magari binafsi na mabasi yaliyokuwa kwenye msafara huo yakitengewa shilingi 26,500,000 ambapo jumla inayoelezwa kutumika kwa safari hiyo inakadiriwa kufikia shilingi 382,675,000 na inaelezwa kila kundi linalofika hapo linapokea kitita chake kulingana na umbali waliotoka, wingi na umuhimu wao kwa jamii.

"Nikueleze ukweli ndugu yangu hili ni dili, kuna watu walitufuata wakasema tujikusanye twende kwa mheshimiwa Lowassa na yupo tayari kugharamia safari yetu na kila kitu kwa siku tutakazokuwa kule ili ionekane kuna watu wanamuunga mkono kwenye harakati zake za urais, hakuna lolote hapa ni mipango tu ya mjini hii" alisema kada huyo wa CCM kutoka Manyara.

Kada huyo aliendelea kusema: "Unajua huu ndio wakati wa mavuno, ukipita hawa waheshimiwa hawapatikani, sasa watu wanapeana taarifa kwamba mambo yapo Monduli, ndio maana watu wanapishana kila kukicha, wengi wanatamka wazi kwamba nao wanaambulia hela zilizoibwa serikalini na huyu bwana (Lowassa)"

Kundi hilo la watu 715 kutoka mikoa mbalimbali, lilipishana na kundi jingine la wafanyabiashara ndogondogo ambalo nalo kama wengine waliopo kwenye mpango huo, walimpatia Lowassa fedha wanazodai kuchanga kwa ajili ya kuchukulia fomu ya urais, sambamba na kadi ya uanachama na baadaye inaelezwa kiongozi wao alikabidhiwa kitita cha fedha ili kumalizia sehemu ya fedha walizopewa awali kama walivyokubaliana.

"Huu ni mgodi mzee, wacha tupige hela huyu ni fisadi hatuwezi kumpa nchi, kwanza amechoka na tumejionea wenyewe kwa macho, halafu tulikuwa tunasikia watu wanakula hela walau nasisi tumepata chochote" alisema kijana mmoja kutoka kanda ya ziwa.

Hata hivyo, inaelezwa makundi mengine baada ya kusikia watu wanaokwenda Monduli wanalipwa, nao wanajikusanya na kuanza safari ya kulekea jimboni hapo kabla Lowassa hajarudi bungeni kwaajili ya bunge la bajeti.

Taarifa kutoka Mkoani Simiyu zinasema, kundi kubwa la watu linatarajia kuwasili Monduli na tayari wapo watu wanaotembeza daftari kuchangisha fedha za kukodi basi za kuwafikisha huko, huku wachangishaji wakisisitiza wakifanikiwa kufika Monduli fedha hizo zitarudi na watapata na faida.

Watu mbalimbali wanasema, hii ni aina nyingine ya mtindo wa Lowassa kugawa fedha, ambapo kila mwaka amekuwa akiandaa sherehe nyumbani kwake Monduli na kuwakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo wahudhuriaji wamekuwa wakilipwa posho na kurudishiwa gharama za nauli zao walizotumia ikiwemo mabasi, ndege na usafiri binafsi na kuandaliwa chakula, vinywaji na malazi kwa siku wanazokaa jimboni humo.

Hata hivyo, mwaka jana sherehe hizo hazikufanyika huku sababu za kiafya za mbunge huyo zikitajwa, ambapo licha ya watu kupewa taarifa kusitishwa kwa sherehe hizo, bado waliendelea kumiminika nyumbani kwa Lowassa ambaye hakuwepo jimboni humo.

"Tutarajie wageni wengi zaidi, maana watu wanajua wakifika wanapata chochote ila sidhani kama wote wanamuunga mkono kwa dhati huyu mzee, watu wanapiga hela tu si unawajua wabongo wakijua wapi kuna mteremko wanajaa, kuna sura nimeziona humu nimeziona kwa wagombea wengine, huenda hii ni ajira yao" alisema mmoja wa vijana waliokuwa kwenye msafara huo.
 
Ukiona mtu anamsifia mtu mchafu kama Lowasa basi ujue yeye ni mchafu zaidi mpaka ananuka.
 
anaandaa timu ya kuingia msituni au ikulu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…