Kwa Laki 5 naweza nikafungua Maabara?

Kwa Laki 5 naweza nikafungua Maabara?

Budget ya laki tano
Nunua Mrdt 2 zakuanzia
Upt box 1
Hiv kit 1
gloves box 1
hivo hata laki haiishi

Tafuta microscope used kwa la3
chumba lipa miez2 (50*2)

Dawa si lazima uwe nazo utakua unawaandikia wakanunue

anza na hapo utaja nishukuru
Mkuu microscope used ya laki 3 inapatikanika wapi mimi nikupe laki 3.5
 
Budget ya laki tano
Nunua Mrdt 2 zakuanzia
Upt box 1
Hiv kit 1
gloves box 1
hivo hata laki haiishi

Tafuta microscope used kwa la3
chumba lipa miez2 (50*2)

Dawa si lazima uwe nazo utakua unawaandikia wakanunue

anza na hapo utaja nishukuru
perfect
 
Laki tano hiyo inaishia kwenye kodi na kutengeneza mazingira ya hilo eneo yakae ki maabara ( utakuwa umeelewa). Pia kumbuka kuna kununua meza na viti na vitu vidogo vidogo kama dustbin nk..

Hiyo ni nje ya kodi ya jengo bana
 
Wakuu nataka nifungue maabara ndogo.

Elewa hapo ndogo! Ila nina mtaji wa laki tano je unatosha kufungua Maabara ndogo ya kuanzia nikipata hela nitakuwa naongezea vitu!

Wataalam wa Afya nawaomba hapa!
Hata Mabara unayafungua ni pesa nyingi tu hiyo.
 
Maabara unayotaka kufungua ni ya udongo ila kama upo serious fanya research ujue vinavyohitajika nini halafu bei zake zipoje uchukue mkopo na kabla hujachukua angalia benki ipi inariba kidogo ila nzuri ni equaty benki na pia angalia mkopo unaoukopa unaweka akiba maana lazima uajiri na mtu mmoja wakuanzia.
Even salary je unaweza kumlipa na nihow much.?
Angalia advantage ya biashara hiyo na hasara zake na back up uwe nayo umeerewa?? Kijana kafanye hayo

wewe ndio mtu

wewe ndio mshauri

kwa huu ushauri nimewasamehe wote waliokua wanatukana!
Ubarikiwe
 
labda ya kupiga ramli...

sorry kama ntakukwaza maana laki 5 unalipa kodi ya jengo miezi mitatu tu na hela ya usafi kwenye jengo kwishaa
 
Maabara huwezi ukafungua kwenye kachumba,😂 kama duka la mangi.. ili upate kibali cha msajili wa maabara Tz lazima uwe na room zisizopungua 3, waiting area ya wagonjwa pamoja na reception, phlebotomy (eneo la kukusanya sampuli), analytical room (eneo la kuchakata sampuli). Unaweza kufanya partition kwa aluminium au boards kupata izi room.

Lazima uwe na male na female Toilets kwa ajili ya ukusanyaji wa sampuli.

Lazima uwe na sink za kunawia mikono zisizopungua mbili.
Surface ya Working benches za maabara zinatakiwa kutengenezwa kwa material isiyofyonza maji (water proof) kama mable. Vitu vingine muhimu ni umeme na AC, room temperature ya maabara inatakiwa kua monitored.

Lakini pia ni lazima waone eneo utakalokua unateketeza taka kwasababu unazalisha taka hatarishi au uwe na kibali cha mahali ambapo utakua unapeleka taka kama nearby hospital inaruhusiwa. Haya ni baadhi tu ya mahitaji ya mazingira ya maabara yanavyotakiwa kuwa ili wakupe kibali cha kufungua iyo maabara.

Kuna vitu vingine vya muhimu sana kwenye usajili, moja ni leseni active ya msimamizi wa maabara awe full registered na baraza la wataalam wa maabara HLPC (baraza linaelekeza kumlipa huyu mtaalam kiasi kisichopungua 400,000/=) ambaye atakua responsible kwa lolote katika hiyo maabara na ikitokea kuna unprofessional issue basi jukumu hili atalibeba yeye ikiwemo kufungiwa leseni

Pili ni leseni ya mtaalam ambaye atakuwepo apo kama mfanyakazi.

Mwisho lazima uende TRA wakakukadirie kodi upewe tax clearence na uende jiji ili upate leseni ya biashara

Hapa hujanunua vitendanishi wala hadubini wala refrigerator wala centrifuge vitu muhimu kipindi cha ukaguzi apo ni vibali tu ndugu!

Kwahiyo nafikiri jibu utajipa mwenyewe kwa laki 5 inawezekana au la!
 
Mkuu hii kitu nauhitaji nayo
Ukikua kibiashara(not now) tuwasiliane, kuna portable device ukiwa nayo you'll make money. Inapima more than 100 diseases from gastrointestinal, hormonal to thyroid.. etc
 
Back
Top Bottom