Kwa kweli wakati mwingine maisha ni ufala sana

Kuna vitu Mungu aliweka siri kubwa..
Mf kifo,maradhi na madaraja ya kimaisha

Huwa napenda kusoma Hekima za Mfalme Suleiman hazichoshi
Ni uhalisia mtupu wa maisha tangu zamani hakuna jipya
Na yote ni ubatili na kujilisha upepo
 
Sisi kajamba nani ndio tukiwaona wanatumia pesa zao tunaumia na kusema "ushamba tu na ulimbukeni unawasumbua".
Na tunavyowalaani wenye pesa zao, kulalamikia ndugu kwamba wameshindwa kutusaidia ili hali na wao hawana, tunavyozaa watoto kila mwaka halafu ada tunalia kwa ndugu watulipie watoto wetu ni shida
 
Tena kunakuwa na chuki kubwa kwa wenye nazo na kuwaandama kwa maneno mabaya ili nao waishi kama mashetani.

Sisi kajamba nani ndio tukiwaona wanatumia pesa zao tunaumia na kusema "ushamba tu na ulimbukeni unawasumbua".
 
Hbr bob! Hamjambo huko TZ? nimekuja UK mara moja mpaka next week. Ntakuja ntaanzisha uzi nikielezea maisha magumu au gari yangu ya japani inasumbua ntapata wapi fundi ili wadau wengi wachangie kwa furaha. But nikiwaelezea trip zangu za Paris na Leo Uk Watakasirika sana. Ndo ufala wa maisha wenyewe huo.

Kiduku Lilo The Don ...mchango wako ni wa muhimu sana eneo hili.Tunakungoja 😂
 
Mkuu tafuta pesa acha kuchonga sana
 
Money also will never betray you.
 
ujieleze tu utapata kazi? Na hizo kazi zozote unazozungumzia watu wanatafuta na hawapati.tukubali maisha ni kama kiganja cha mkono hatuwezi kuwa sawa hata iweje.
Tatizo lenu kazi mnazani ni ile muajiriwe tu, tena mnachagua siwezi kufanyakazi ya aina Fulani. Kazi ni shughuli yoyote halali itakayokuingizia kipato. Nafasi za kufagia barabara zipo muda wote, saiti zote za kujenga zinanafasi za kazi ya kubeba zege muda wote. Masoko yote yana kazi za kubeba mizigo muda wote n,k, n.k. Nikweli binadamu hatutalingana na haitakiwi tulingane, lakini unashindwa hata kulihudumia tumbo lako.
Kaa na vyeti vyako subiri eti mpaka upate kazi yenye hadhi yako utasubiri sana. Anza chini ukipata mtaji unabadilisha kazi hatua kwa hatua
 
Na tunavyowalaani wenye pesa zao, kulalamikia ndugu kwamba wameshindwa kutusaidia ili hali na wao hawana, tunavyozaa watoto kila mwaka halafu ada tunalia kwa ndugu watulipie watoto wetu ni shida
Yaani ni taabu juu ya shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…