Shaka-Zulu
JF-Expert Member
- Nov 20, 2018
- 432
- 822
Hawa unaowaita waathirika pia walitumia pesa zao kununua sleeping pills, pain killers nk, kujipatia usingizi na kujisikia vizuri, na ghafla walijikuta kuwa hawawezi kushinda bila ya madawa!!!Mzee mbona umetolea mfano wa stress za watu kundi la wavuta bhangi na watumiaji wa dawa za kulevya?
Yote uliyoyaandika yana mantiki ya msingi lakini hayana conclusion.
Umetamani kusafiri kukutana na marafiki zako, utasafirije bila pesa?
Mifano hiyo michache lakini ipo mingi sana katika maisha ambayo kuipata furaha yako mpaka uigharamie.
Hujawahi kusikia kwamba mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake!!! Watu wasiokuwa na pesa huwa wanatafuta furaha zao kwenye simple things zinazoendana na hadhi yao. Wahenga wameshasema "tamaa nyingi, mbele giza!" Nani hapa kwetu amesikia kuhusu caviar, chakula cha matajiri??! Hatujasikia kwa sababu haina uhalisia na maisha zetu. Maskini amejifundisha kufarahia ugali na mchicha, bora ushibe kuliko kushinda na njaa, huku ukiwaza biryani! Ukiishi kwa tamaa inayozidi kipato chako, unajiweka wazi kwa mambo kama rushwa, uwizi, uporaji nk!!
Halafu, angalia takwimu ya suicide rates duniani - nchi tajiri kama Sweden, South Korea, Japan ndio wanaongoza na hali imekuwa mbaya mpaka imetangazwa janga nchini mwao. Sasa jiulize, kwa nini kwenye nchi tajiri inazowapatia kila aina ya huduma kuanzia cradle to the grave, bado raia hawaoni furaha ya kuishi na wanaamua kujiua??!!
Pesa si kitu ya kudharau, lakini kuna vitu vingi - upendo, urafiki, afya, hekima, nk ukizinunua utagundua ni feki!!!! Ni vitu ambazo ni majaliwa ya Mungu na ndizo zinaongeza furaha kwenye maisha. Kama pesa ingekuwa kila kitu, basi kwa nini tunasema "Mungu akuongezee baraka" badala ya "Mungu akuongezee pesa" na "Ubarikiwe Sana!!" badala ya "Utajirike Sana!!"???