Kwa kuwaita "Mafisadi" tumeficha uovu wao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa kuwaita "Mafisadi" tumeficha uovu wao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 27, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Public Discourse 1 - Tuwaite Wahujumu Uchumi:

  Na. M. M. Mwanakijiji

  Ndio tumeamua kuwapachika majina ya uongo na hivyo kuficha uzito wa makosa yao na kwa kuwaita kitu ambacho sicho tumeshiriki kuficha ukali wa uovu wao. Tumeamua kuwabatiza jina la "mafisadi" tukiamini ya kwamba hilo ndilo jina sahihi linaloelezea kile wanachokifanya.

  Tumewaita "mafisadi" tukiamini ya kuwa tunataja kosa lao na hivyo kuashiria katika jamii kuwa tumewagundua. Hata hivyo ukweli hauko mbali; kwa kuwaita "mafisadi" tumeshiriki katika kuighiribu jamii kuamini kwanza kabisa kuwa kuna kosa la "ufisadi" na pili tunawaaibisha watu hao kwa kuwaonesha kile wanachofanya.

  Hakuna kosa la "ufisadi" nchini, halijawahi kuwepo. Ufisadi kimsingi unahusiana na mambo ya ngono zaidi kuliko kutafsiri neno "corruption" kama wengi tulivyolichukulia. Yawezekana kutokana na kukua kwa lugha neno hilo sasa linakubalika kuelezea mkusanyiko wa tabia zote ambapo mtu katika sekta ya umma na binafsi anatumia nafasi yake kujinufaisha, kuiibia serikali, au kutumia madaraka yake vibaya. Lakini hata ikiwa hivyo "ufisadi" hauelezei kile hasa ambacho kimefanywa na watu mbalimbali ambacho kinaathiri au kimeathiri uchumi wetu na nafasi ya Taifa zima kufanikiwa.

  Huko nyuma kuna wimbo (nadhani ni Vijana Jazz wale) unaoitwa "Wanaitwa Matapeli". Wimbo huo ninapoufikiria unaelezea kile ambacho kilidaiwa kufanywa na watu kadhaa ambacho ni kuwauzia watu kanyaboya kwa minajili ya kujipatia fedha bila kutoa huduma au bidhaa halisi. Hivyo watu hawa walipoibuka waliitwa "Matapeli".

  Naamini wakati umefika wa kuwaita watu hawa jina wanalostahili, linaloelezea kosa lao la kisheriia na pia kile wanachokifanya dhidi ya nchi yetu. Ndugu zangu watu hawa ni WAHUJUMU UCHUMI kwa mujibu wa sheria ya Kuhujumu Uchumi ya 1984 na mabadiliko yake ya 1987.

  Kwa wengine jina hilo linawafanya vinyweleo visimame kwani vinawakumbusha kampeni dhidi ya wahujumu uchumi ya miaka ya themanini. Watu wanaoogopa kuwaita wauza magendo, mchoromchoro, na wanaopenda mwendo wa kuruka kuwa ni wahujumu uchumi. Tumekwepa kuwaita walioiibia Benki Kuu mabilioni ya shilingi kuwa ni Wahujumu Uchumi na badala yake tumewavika mafuta ya "Ufisadi". Tumeshindwa kumuita Chenge Mhujumu uchumi anapohamisha Shilingi Bilioni moja na kuzificha nje ya nchi, tumemuita fisadi tu. Tumeshindwa kuwaita kina Karamagi, Lowassa, Msabaha na kina Gire kuwa ni Wahujumu Uchumi licha ya maamuzi na matendo yao kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu.

  Tumeogopa (sijui sababu nini) kuwaita waliogawiana mali za Taifa letu kama njugu na kumegeana kama viazi nyumba zetu kuwa ni wahujumu uchumi. Kwa kuwaita "mafisadi" tumeficha uovu wao na kuficha kiini cha matendo yao. Ndugu zangu hawa ni wahujumu uchumi na hilo ndilo lililivyo.

  Kuwaita "mafisadi" ni kuwavisha cheo cha chini cha uovu na matendo yao. Ni sawa na kumuitwa mwizi "aliyesogeza kitu si chake" au mbakaji "aliyejiridhisha zinaa bilaa ridhaa ya mwingine". Tunapotumia neno "fisadi" kimsingi hatutaki kuita kile ambacho wote naamini tunakifahamu kuwa watu hawa waliokwapua fedha za umma, kufanya maamuzi mabaya kabisa kwenye Taifa letu si kingine isipokuwa ni WAHUJUMU UCHUMI.

  Tukiweza kuwapa jina sahihi ndipo hapo tutajua tupambane nao vipi kwani tutakuwa tumedefine adui yetu sawasawa na hivyo kutafuta mbinu sahihi za kupambana naye. Kwa vile hakuna sheria dhidi ya ufisadi ni vigumu kupambana na mafisadi.

  Ashukuriwe aliyejuu kuna sheria inayohusiana na "uhujumu uchumi" na ambayo inastahili kutumiwa kwa nguvu zote sasa kupambana na wahujumu uchumi hawa ambao wamejificha kwenye pazia lilioandikwa "Ufisadi". Tuwape jina sahihi, ili tuwashughulikie kwa usahihi. Vinginevyo, tukiendelea kuwaita "Mafisadi" tunaficha uzito wa matendo yao. Nimeamua kuwaita "wahujumu uchumi' kwani hivyo NDIVYO WALIVYO.

  Ni mimi,

  Mwenzenu,
  Ndugu yenu,
  Rafiki yenu na kwa wengine
  ADUI YENU

  M to the THIRD POWER!
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono 100%.Enzi zile za Nyerere as history tell us a special Tribunal was formed to try and presecute hawa wahujumu uchumi and it was presided by one Judge who did his work impeccably.
  I suggest that hapa Tanzania for God's sake tuwe na malawyers na judges kama wa Pakistan who real know what it means to administer justice.We proclaim that our legal system is one of the most respected in Africa why dont we push for such a tribunal so that we can prosecute all of them hawa aka MAFISADI?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua kwa kadiri tumeendelea kuwaita "mafisadi" ndivyo hivyo hivyo hawakutuchukulia maaanani kwani hatuwaiti kwa kosa wanalotuhumiwa kufanya na badala yake tunatumia euphemism ya "fisadi" tukitaka kweli kumaanisha "mhujumu uchumi". Kwa kufanya hivyo, fisadi haogopi lolote kwani hakuna sheria inayokataza au kuadhibu kosa la "ufisadi" kwani kosa hilo halipo.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ufisadi is a more general term that include uhujumu uchumi.It is possible to be fisadi without being "mhujumu uchumi"

  In the interest of preciseness an argument can be built for the need to adoptb a more descriptive name, let this name apply correctly, as for example, the term "wahujumu uchumi" may not apply to socially corupt / morally banjkrupt people.

  Some people may have chosen "fisadi" over "mhujumu uchumi" to differentiate this war on corruption from the Sokoine misguided effort.From this perspective, they should be free to use any term suitable as long as it applies, even if it is generic.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Fisadi ni neno ambalo kwanza linatumiwa vibaya katika Kiswahili na pili halielezei hasa nature ya vitendo vinavyotajwa. Ni neno ambalo kwa bahati mbaya sana linaficha kwa kiasi kikubwa vile hasa vinavyozungumzwa.

  Mhujumu Uchumi ni kosa la kisheria na ni pana mno kiasi kwamba watu wengi ambao tunawataja katika migogoro yetu ya siku hizi wanaangukia humo. Tatizo la fisadi ni kuwa linapotosha; mtu ambaye ni mzinzi anaweza kuitwa fisadi, mla rushwa anaweza kuitwa fisadi, mwizi anaweza kuitwa fisadi n.k Tatizo ni kuwa tunachozungumzia kwa kiasi kikubwa ni kile kinachohusu uchumi wetu zaidi na hivyo yale yanayofanywa yanaathiri uchumi kuliko kitu kingine chochote. HIvyo kuwaita wanaohujumu uchumi kuwa ni "wahujumu uchumi" siyo tu tunakuwa precise bali zaidi tunaelezea essence ya vita tunayopambana nayo.

  Wakati wa Sokoine walikuwepo wahujumu uchumi na kuna wengine ambao waliingizwa katika kundi hilo pasipo haki na hii ndiyo iliyosababisha mabadiliko ya sheria ile mwaka 1987 ili kuitengeneza vizuri ifae. Wapo mafisadi lakini wapo pia wahujumu uchumi. Ingawa wahujumu uchumi wanaweza kuwemo kwenye kundi la mafisadi, mafisadi wote siyo wahujumu uchumi.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Heshima ya MMKJ.
  Every one is presumed to be inocent until proven guilt.
  Naomba tusianze kuwahukumu kwa majina ya makosa ya kisheria wakati hata hawashitakiwa.

  Naomba tusubiri washitakiwe mthibitishe wanashitakiwa kwa makosa gani ndipo angalau tuwaite watuhumiwa wa uhujumu na wataitwa wahujumu baada ya mahakama kuthibitisha kosa.

  Naomba Tusihukumu Tusije Tukahukumiwa.
   
 7. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama ni lazima tusubiri washitakiwe. MM amewaita jina sahihi kabisa. Kwamba hawa wanadamu, aka mafisadi, wanatuhumiwa kwa kuhujumu uchumi. Wamevunja sheria. Kwahiyo bado ni tuhuma, na zitadhibitiswa mahakamani.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  The first principle of natural justice is 'No one is condemed aheard'

  Hawa jamaa wametajwa tuu kuhusika. Hakuna aliyeshitakiwa mpaka sasa. Kwanini tuanze kuwaita majina?. Zimebaki siku mbili tuu kesi itinge mahakamani. Kama tumevumilia siku zote hizo kwa jina la mafisadi, tuvumilie siku mbili nyingine tuone kama watashtakiwa kama wahujumu.

  'Tusihukumu Tasije Kuhukumiwa' I hope you know the law of the Karma.
   
 9. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Forget about natural justice, the laws of semantics favors "mafisadi" over the more descriptive and accurate but mouthful "wahujumu wa uchumi".

  Picture a newspaper editor with economy of space in mind and a choice between "mafidadi wakamatwa" and "Wahujumu wa uchumi wakamatwa"

  Fisadi has the mysterious air of sounding even more heinous.
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Neno Mafisadi lililenga ku-"provoke then assess" na majibu tuliyapata kwani wengi waliitikia bila kujua mtego wa Lissu kuwa wataenda mahakamani, baadaye wakang'amua na kukaa kimyaaa, sasa nafikiri ni muda muafaka kuwaita Wahujumu uchumi kwani makabrasha yenye ushahidi mengi kina slaa na jamii wanayo
   
 11. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji nililisema hili ktk moja ya hoja za jf wiki iliyopita, too much kuiga kusikoleta fasiri ya maana kwa kizazi kijacho
   
 12. M

  Mavanza Member

  #12
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hilo jina la fisadi ndilo lenyewe. Wadanganyika leo wameshaaminishwa kuwa fisadi ni mwizi na mhujumu wa uchumi, tusiwachanganye watu. Kama hiyo sio maana yake basi kwa jamii yetu sasa limebatizwa na kupewa maana tunayoijua sisi. Fisadi ni mtu mbaya sana, mwizi wa mali ya umma, mhujumu wa uchumi, mtu asiyejali maslahi ya taifa hili na kuamua kuiba hazina, mla rushwa nk. Hiyo maana nyingine imeshakwenda na maji.

  Tusichanganye wananchi, ufisadi unaeleweka tuendelee kuwaita hivyo tu na kwa maoni yangu hilo wala hali hafifishi wizi wa EPA wala Richmond hao ni mafisadi tu.
   
 13. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Watu wamegushi nyaraka ili kujipatia mabilioni kutoka Benki kuu...hakuna lugha yoyote ya kuwaita hawa zaidi ya WEZI. Kilichotokea EPA is simply FRAUD na sheria iko wazi kuhusu suala hili.
  Hivi kuna sheria yoyote inayozungumzia kosa la ufisadi??
   
Loading...