Kwa kupunguza mishahara ya madaktari wa Bugando, wakazi wa kanda ya ziwa tumekwisha

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
476
Ni taarifa ya serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikifafanua kuhusu ajira, posho na mishahara katika sekta ya afya.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na Watumishi wa Hospitali ya Bugando ililenga kutoa ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.

Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya Serikali na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.

Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika. Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda.
Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali nyingine za Kanda.

Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Serikalini litakapokamilika. Hivyo, vibali vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo itakapotamkwa vinginevyo.

Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta posho ya ‘Interns’ kuanzia mwaka huu wa fedha. Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.

Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na Mamlaka husika kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala ya Mitandao ya kijamii.
 
Kwa hii miaka 5 watumishi wa umaa watakuwa roho juu sana. Wazee walioapa kwa kudanganya na kuongeza umri wa kustaafu wanajuuuta sana.
 
Hili Nalo Neno
Acha Wote Waisome Namba Hii T 2020 CCM
Hutaki Unaacha !!!!
 
kumshushia mtu mshahara ni kumuadhili kisaikolojia kiutendaji mzuri na kudidimiza utoaji wa huduma ya afya kwa hospitali hiyo tegemeo la wakazi wa kanda ya ziwa , bora wangepandishia hao wengine walingane harafu....kwanini iwe bugando tu aise sijui hii nchi tunakoelekea
 
Serikali inaongeza mapato kwa kukusanya kodi,sio Kupunguza mishahara,hata wakati wa vita ya Uganda na baada ya vita Mwalimu nyerere hakupunguza mishahara,bali alijitahidi kuongeza uzalishaji Mali,

Tunataka kumsikia Mkuu akiongelea Mbuga za wanyama, migodi ya madini na gesi,kila siku watumishi,kila siku watumishi,kwenye mapesa mengi hagusi
 
Kwa hii miaka 5 watumishi wa umaa watakuwa roho juu sana. Wazee walioapa kwa kudanganya na kuongeza umri wa kustaafu wanajuuuta sana.
Hivi kweli mmeelewa hiyo taarifa au mnachangia tuu? Hivi kwanini mnakataa kusoma kwa makini na kutafakari bali mnakimbilia kuchangia tuu?

Hivi Madaktari wa bugando kwanini walipwe zaidi ya wengine? Hatua hii imechukuliwa kuleta Usawa kwa watumishi wote wa kada za udaktari kwenye swala la mshahara.

Mbona mmeshindwa kujadili waliopotosha kuwa posho zimefyekwa?
Nyie huwa hamuoni?
Hili Nalo Neno
Acha Wote Waisome Namba Hii T 2020 CCM
Hutaki Unaacha !!!!

kumshushia mtu mshahara ni kumuadhili kisaikolojia kiutendaji mzuri na kudidimiza utoaji wa huduma ya afya kwa hospitali hiyo tegemeo la wakazi wa kanda ya ziwa , bora wangepandishia hao wengine walingane harafu....kwanini iwe bugando tu aise sijui hii nchi tunakoelekea

Serikali inaongeza mapato kwa kukusanya kodi,sio Kupunguza mishahara,hata wakati wa vita ya Uganda na baada ya vita Mwalimu nyerere hakupunguza mishahara,bali alijitahidi kuongeza uzalishaji Mali,

Tunataka kumsikia Mkuu akiongelea Mbuga za wanyama, migodi ya madini na gesi,kila siku watumishi,kila siku watumishi,kwenye mapesa mengi hagusi
 
Hivi kweli mmeelewa hiyo taarifa au mnachangia tuu? Hivi kwanini mnakataa kusoma kwa makini na kutafakari bali mnakimbilia kuchangia tuu?

Hivi Madaktari w
a bugando kwanini walipwe zaidi ya wengine? Hatua hii imechukuliwa kuleta Usawa kwa watumishi wote wa kada za udaktari kwenye swala la mshahara.

Mbona mmeshindwa kujadili waliopotosha kuwa posho zimefyekwa?
Nyie huwa hamuoni?

Taarifa tumeielewa kwa akili yako hili swala unaona kawaida....hebu jiulize kwa nini waliwapandishia Mshahara?, pili hili kiutendaji limekaaje? tatu uzito wa kazi kwa bugando ni sawa hospitali za wilaya?kama ziko sawa kwa nini mgomjwa anapelekwa hospitali ya bugando akishindwa hizo hospitali za wilaya? kwani nin MNH,Ocean road,na Moi wawe wasipunguziwe pia walingane na hospitali zingine....kwa akili hii maendeleo sdhani kama tutayapata kama tunavyotegemea
 
Mbona wa muhimbili hawakuwa na hilo ongezeko?
 
Mbona wa muhimbili hawakuwa na hilo ongezeko?
unauhakika na unachokiongea kwa kukufamisha muhimbili wanahilo ongezeeka na wako malipo ya mashirika ya umma ikiwemo moi na ocean road kwa taarifa ya katibu wa wizara ya afya . hizo zote hawashushi mishahara isipokuwa bugando tu....
 
Soma taarifa tena bugando wana ongezeko zaidi ndio maana limeondolewa.
 
Soma taarifa tena bugando wana ongezeko zaidi ndio maana limeondolewa.
Taarifa inaonesha Bugando ilipanda ikawa shirika kutoka na hadhi ya kazi inazofanya ikastahili kuwa na status hiyo ndio maana wakaibadilishia mshahara ukawa kama wa muhimbili ocean road na moi lakini kipindi hiki wamegundua haina level hizo ndio maana wameamua kuishushia mishahara kwa maana hiyo bado wanaruhusu ubaguzi ndani ya hiz taasis .kama lengo ni ulinganisho wangefyeka kote kukalingana
 
Nashindwa kuelewa kwanini madaktari wa Bugando wanaolipwa na serikali walipwe mishahara tofauti na madaktari wa KCMC, Muhimbili na Mbeya zonal refferal hospital?

Kwa hizi ngazi za chini kuanzia hospitali za mikoa wilaya mpaka zahanati najua watumishi wa Afya wanalipwa kulingana na elimu pamoja na uzoefu kazini bila kujali yupo katika hospitali ya mkoa, wilaya, kituo cha afya au zahanati. Mfano Clinical Officer (CO) aliyepo hospitali ya mkoa mshahara wake ni sawa na Clinical officer aliyepo katika zahanati ya kijijini kwetu. watakachotofautiana ni malupulupu tu
 
Taarifa tumeielewa kwa akili yako hili swala unaona kawaida....hebu jiulize kwa nini waliwapandishia Mshahara?, pili hili kiutendaji limekaaje? tatu uzito wa kazi kwa bugando ni sawa hospitali za wilaya?kama ziko sawa kwa nini mgomjwa anapelekwa hospitali ya bugando akishindwa hizo hospitali za wilaya? kwani nin MNH,Ocean road,na Moi wawe wasipunguziwe pia walingane na hospitali zingine....kwa akili hii maendeleo sdhani kama tutayapata kama tunavyotegemea
Kwahiyo we unafikiri huyo wa Moi, muhimbili na zingine wanalipwa zaidi kuliko dactari wa mikoani au zahanati?
Kikubwa wawe na elimu sawa, wote ni sawa na watalipwa sawa.
Huyo wa Moi, muhimbili na Bugando atafaidika na posho na overtime na semina na mambo mengine, ila mshahara unatakiwa kuwa sawa...
Mshahara unatokana na elimu yako na secta uliyoko...
Sasa kwanini Hao wa Bugando walipwe zaidi? Ndio maana wakapunguziwa wawe wanalipwa kama wengine....
Nyam......ba.....fu......
 
kwa jinsi akili yako ilivyo fu...pi unafikiri Dactari wa Muhimbili analipwa sawa na wa mikoani au zahanati? ndio maana lowasa alisema kipaumbelee elimu elimu elimu ili kuondoa mazo...mbie kama nyinyi
 
kwa jinsi akili yako ilivyo fu...pi unafikiri Dactari wa Muhimbili analipwa sawa na wa mikoani au zahanati? ndio maana lowasa alisema kipaumbelee elimu elimu elimu ili kuondoa mazo...mbie kama nyinyi
Haya kaka... Nashukuru kwa elimu uliyoipata....
Kwa kuwa sina uwakika na hilo, basi siwezi kulishupalia sana......
 
Back
Top Bottom