Kwa kupunguza mishahara ya madaktari wa Bugando, wakazi wa kanda ya ziwa tumekwisha

Serikali inaongeza mapato kwa kukusanya kodi,sio Kupunguza mishahara,hata wakati wa vita ya Uganda na baada ya vita Mwalimu nyerere hakupunguza mishahara,bali alijitahidi kuongeza uzalishaji Mali,

Tunataka kumsikia Mkuu akiongelea Mbuga za wanyama, migodi ya madini na gesi,kila siku watumishi,kila siku watumishi,kwenye mapesa mengi hagusi
mkuu ulichoadika ni ukweli mtupu kupunguza mishahara na haya maisha ni kuharibu utendaji kazi
 
mkuu ulichoadika ni ukweli mtupu kupunguza mishahara na haya maisha ni kuharibu utendaji kazi
Kweli kabisa,marais wote walisifika kwa kuongeza mishahara,kama sehemu nyingine mishahara yao iko chini ni bora uiongeze ifanane na wa bugando,yaani wa chini apande juu,sio wa juu umshushe ili awe masikini halafu ujisifu umeboresha kitu
 
Naomba Sana Watanzania Mniombee
Ili Ninapofanya Maamuzi Asiwepo Wa Kunikwamisha
By Jpm
 
Kuna watumishi mwezi wa tatu na wanne walipandishiwa mishahara mwezi wa 5 wakashushwa tena et tunahakiki wafanyakazi hewa hii sio haki kabisaa
 
Kweli kabisa,marais wote walisifika kwa kuongeza mishahara,kama sehemu nyingine mishahara yao iko chini ni bora uiongeze ifanane na wa bugando,yaani wa chini apande juu,sio wa juu umshushe ili awe masikini halafu ujisifu umeboresha kitu
Mnachangia bila kusoma madaktari wa Bugando wamekuwa wakilipwa zaidi ya wengine na hilo ndio kosa lililo fanyika...Hivi siku wengine wakigoma kuhitaji ongezeko kama bugando itakuwaje? Hapa tunaongelea mshahara si posho...maana posho ni kweli lazima watofautiane.

Na ninaomba Moderator Invisible Mhariri Mod 6 Paw mbadilishe kichwa cha habari kiwe serikali yatoa ufafanuzi kuhusu taarifa za madaktari kukatwa mishahara na kukatwa posho..
mkuu ulichoadika ni ukweli mtupu kupunguza mishahara na haya maisha ni kuharibu utendaji kazi
 
Ni taarifa ya serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikifafanua kuhusu ajira, posho na mishahara katika sekta ya afya.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na Watumishi wa Hospitali ya Bugando ililenga kutoa ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.

Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya Serikali na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.

Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika. Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda.
Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali nyingine za Kanda.

Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Serikalini litakapokamilika. Hivyo, vibali vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo itakapotamkwa vinginevyo.

Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta posho ya ‘Interns’ kuanzia mwaka huu wa fedha. Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.

Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na Mamlaka husika kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala ya Mitandao ya kijamii.
Kumbe unatuletea habari ya uvumi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom