Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Wanabodi
Naomba kuanza na Angalizo:
Mada kama hizi ni mada za kiutu uzima, hakuna kutaja taja majina ya watu wowote humu!, na ukijiona una washwa washwa kutaka kutaja majina hapa, au kuuliza ni nani, ujijue huu uzi sii saizi yako!, nakuomba jipitie tuu kwenda kwenye nyuzi za kimo chako!, sio lazima kuchangia kila uzi!.
Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo, Kwa Makubwa Aliyoyatenda, haja ya kupiga tarumbeta kumnenea, tuyaache matokeo yatamnenea!, tena hakuna hata haja ya kumsukuma mlevi! anayesema hakujafanyika kitu!.
Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!
Nimeshiriki nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi, na niliendelea kushiriki chaguzi zote za vyama vingi, toka ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025 huku nikiwafunza vijana wa leo, busara zilizomo ndani ya ngano za lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Wakati wetu tulifundishwa hadithi, vitendawili, nahau, na tamathali za semi.
Mada ya leo ni ya tamathali za semi hii ya Kiswahili isemayo "Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo“, ni sawa na ile semi inayosema "Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno"
Ada ya mja hunena, ada ni matendo, mja ni mtu, kiumbe wa Mwenyeezi Mungu, Ada ya mja hunena, ni matendo ya mtu anayotenda yananena, yana sauti, yana msemea, badala ya mtu kusema kwa maneno, nimefanya hiki au nimefanya kile, wewe tenda, fanya kitu cha kuonekanikani, halafu matokeo ya matendo yako, au matokeo ya ulichokifanya ndio yakusemee!, ukifanya jambo jema zuri la kuonekanika, huna haja ya kusema, umefanya nini, acha watu waone kilichofanyika, halafu hicho kilichofanyika ndio kinakuenea. Neno muungwana ni kitendo sio kauli au maneno "mimi muungwana", tenda uungwana, halafu hayo matendo yako ya uungwana au kiungwana ndio yakunenea na kukusemea, fulani ni muungwana!.
Binadamu siku zote, huwa hawana mema, sio watu wote ni watu wema, kuna wengine ni mahasisidi, hasidi huwa hana sababu!, kuna watu sio wana wema, hata uwatendee mema makubwa kiasi gani, ipo siku, watakutenda tuu!, ndio maana. Waswahili wanamsemo wa "Tenda wema uende zako, usisubirie shukrani", na mahali penye wema, kuna msemo, “pema usijapo pema, ukipema, sii pema tena”, ukitenda jambo jema, usijisifu kwa jema hilo, ukijisifu, hilo jema litatafutiwa ubaya!.
Nimeleta mada hii baada ya kuangalia mubashara kupitia TBC, uzinduzi wa daraja la JPM, Kigongo - Busisi, nikakumbuka daraja la Tanzanite, nikakumbuka flyover ya Tazara, Interchange ya Ubungo, Mradi wa JNHPP, nikakumbuka reli ya SGR, serikali kuhamia Dodoma, Ikulu ya Chamwino, mashule, mahospitali, mabarabara kibao, midege ya ATCL tulioinunua kwa kupiga tanchi!, na maendeleo mengine mengi makubwa ya kuonekanika, nikajisemea kimoyo moyo, “kiukweli Yule Kaka yangu, alikuwa na uthubutu mkubwa!, kuna baadhi aliyatekeleza wala hayakuwemo kwenye ilani, ila pia kuna yaliyokuwemo kwenye ilani, akaachana nayo kwasababu sio kipaumbele chake.
Pamoja na wema wote huo, ulipofika muda wa kutwaliwa, Kaka alitwaliwa na Dada akaingia na kukamilisha yale mema makubwa mazuri ya kuonekanika anayoyatenda mja huyu aliyepo sasa, kwanza kwa kukamilisha yale ya mtangulizi wake, kisha kujumlisha na ya kwake anayotenda, kiukweli kabisa, matendo yake yamekidhi haja maridhawa kuiko maneno!, hivyo Watanzania tuwe waungwana, anastahili kushukuriwa kwa kupewa shukrani ya asante stahiki!.
Kitendo cha mtu kufanyiwa wema mkubwa hivi, halafu kuwa mtovu wa fadhila, kuwa mtovu wa shukrani, kutomshukuru mtu kama huyu ni kujichumia tuu bure ile dhambi! ya utovu wa fadhila na utovu wa shukrani!
Watanzania walio wengi ni waungwana sana, ni wastaarabu sana, na ni watu wa shukrani na kukumbuka fadhila, sio watovu wa shukrani kivile!, hivyo utakapo wadia ule muda wa kutoa shukrani, Watanzania watampatia shukrani zake stahiki!.
Wakati wote, mema haya, makubwa na mazuri haya yakiendelea, kuna walevi, wamelewa na wanaiga kelele sana kuwa hakuna chochote kilichofanyika!, kuna msemo mwingine wa Kiswahili, unaitwa "kumsukuma mlevi". Unamuona mlevi amelewa chakari, anatembea kwa kuyumba yumba, yaani ni amelewa tilalila!, ukimsukuma kidogo tuu, ni anakwenda chini, na jinsi pombe zilivyomzidia, akienda chini, anaweza hata kudondoka mtaroni, akashindwa kuinuka ikawa ndio mtolee!, mtu ameondoka jumla!.
Kufuatia shukrani za Watanzania kwa mja huyu, kwa kilichofanyika, hakuna kabisa sababu ya kumsukuma huyu mlevi, mja wetu, usimsukume kabisa, huyu mlevi, mwache aendelee kutembea kwa kupepesuka na pombe zake, atajiangukia mwenyewe, bora lawama za kutomsaidia mlevi kwa kumwacha akapepesuka hadi akaanguka mwenyewe, kuliko fedheha ya kumsukuma mlevi akaanguka, na ile anguka yake ikawa ni ile anguka ya mtolee!. Lawama utabebeshwa wewe kwa kumsukuma!.
Asante stahiki kwa huyu mja aliyepo ni ile asante ya ile siku ya siku, ni unachukua, unaweka, !, ..
Hivyo namshauri aliyepo, awape tuu kila wanachokitaka, hata kama hawastahili, ali mradi, wameomba, wanapiga makelele sana, yanatukosesha usingizi, wapewe tuu!
Wasipopewa, baada ya Watanzania kuonyesha shukrani zao kwa yaliyofanyika, mtakuwa mmewapa uhalali wa lile jambo letu lile, watasema yule aliyepita sio amepita kwasababu alistahili, watadai ni amepita kwasababu, amesimama na vivuli, mshindani wa ukweli, amefanyiwa figisu ya kubambikiwa kesi mbaya ili kuhalalisha kumhifadhi pahala salama kupisha jambo letu, hivyo aliyeshinda, ameshinda kwasababu ameshindanishwa na kivuli, au vivuli!.
Naendelea kushauri, kale ka simba ka Kizimkazi, kaondolewe tuu kwenye ile cage, katatusumbua sana kwa kupigiwa kelele kutoka karibu kila kona!.
Hebu tuwape tuu wanachotaka, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki, mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea lile tukio lile kutokea!, tusipojirekebisha hii 2025, tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!.
Mwenye macho na aone,
Mwenye masikio asikie!
Mungu Ibariki Tanzania.
Mzee Pasco