Kwa kauli hii, Je Kikwete ni Dikteta??

RayB

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
2,751
196
Wadau inasemekana Kikwete alitoa kauli hii kama sehemu ya hotuba yake kwa bunge:

"Hata hao ambao hawakuichagua CCM, serikali yao ni hii hii ambaye rais wao ni mimi... hata hao waliosusia, watakwenda; watarudi,"

Ukiangalia ni kauli iliyojaa vitisho kwa ambao hawakuchagua CCM na kwa wabunge wa CHADEMA. Anaonyesha ni jinsi alivyo mroho wa madaraka na kuonyesha kuwa yuko proud sasa kuwa yeye ni Rais na watu watake wasitake watamtii tu. Je hizi kauli si huwa zinatolewa na madikteta? Iko wapi kauli ya kuwa 'ushindi' wake ni ushindi wa wote??? Je huu ni mwanzo tu wa kuona true colors za huyu bwana?
 
Rais wa nchi ni rais wa watu wote. Kwa mantiki hiyo, hakuna kipengele kinachoonyesha JK ni dikteta. Ni siasa.
 
Wadau inasemekana Kikwete alitoa kauli hii kama sehemu ya hotuba yake kwa bunge:

"Hata hao ambao hawakuichagua CCM, serikali yao ni hii hii ambaye rais wao ni mimi... hata hao waliosusia, watakwenda; watarudi,"

Ukiangalia ni kauli iliyojaa vitisho kwa ambao hawakuchagua CCM na kwa wabunge wa CHADEMA. Anaonyesha ni jinsi alivyo mroho wa madaraka na kuonyesha kuwa yuko proud sasa kuwa yeye ni Rais na watu watake wasitake watamtii tu. Je hizi kauli si huwa zinatolewa na madikteta? Iko wapi kauli ya kuwa 'ushindi' wake ni ushindi wa wote??? Je huu ni mwanzo tu wa kuona true colors za huyu bwana?

Kauli zake hazijajaa vitisho, bali ni kutojiamini. Hayuko proud na chochote, roho inamuuma sana 2, sababu kama angekuwa anajiamini angenyamaza 2, na aone kama hamna kilichotokea, lakini kwa kujisemesha semesha inaonyesha jinsi gani hajiamini. Kitendo cha wapiganaji kutoka nje kinamaanisha hawautambui ushindi wake, hivyo ushindi wake si wa wote.
 
Wadau inasemekana Kikwete alitoa kauli hii kama sehemu ya hotuba yake kwa bunge:

"Hata hao ambao hawakuichagua CCM, serikali yao ni hii hii ambaye rais wao ni mimi... hata hao waliosusia, watakwenda; watarudi,"

Ukiangalia ni kauli iliyojaa vitisho kwa ambao hawakuchagua CCM na kwa wabunge wa CHADEMA. Anaonyesha ni jinsi alivyo mroho wa madaraka na kuonyesha kuwa yuko proud sasa kuwa yeye ni Rais na watu watake wasitake watamtii tu. Je hizi kauli si huwa zinatolewa na madikteta? Iko wapi kauli ya kuwa 'ushindi' wake ni ushindi wa wote??? Je huu ni mwanzo tu wa kuona true colors za huyu bwana?

Unauliza majibu?, kupindua maamuzi ya wapiga kura ni udikteta tangu hapo. Wananchi wanachagua wanayemtaka, JK anaitumia NEC kubadilisha maamuzi ya wananchi huu ni udikteta sawa na kupindua serikali ya wananchi.
 
alisema watarudi tu kwake, hata wakienda watarudi, hawana kwa kwenda. that means lazima watarudi wapige goti kwake tu.
 
Sina uwakika na kauli hii kama kweli alitoa,( sikuwepo, sina data kamili) ila kama alitoa, inaiweka ccm mahali pabaya mwaka 2015. Alafu ni kauli iliyomtoka( nifikiriavyo), hakuitoa nadhani, na pili hana cha kutafuta kipindi kijacho( he has nothing to lose). Naamini, yeye mwenyewe raisi hakuamini macho yake kuona vituko hivi mbele yake, ila naamini ndiyo njia sahihi ya kujengeka, kikwete ameanza kukomaa na ana komazwa kikweli kweli, ccm wataanza kuwa makini.( unajua paka akiondoka, panya huwa wanaenda ovyo ovyo).
 
Kama kweli alitoa kauli hiyo mbele ya mabalozi walioalikwa na kuhudhuria hilo bunge, nadhani nitalinganisha wasiwasi uliompata kuwa sawa na wakati aliposema hahitaji kura za wafanyakazi. Na hii ni sawa kabisa na kuwakumbusha wafanyakazi wale wale kuwa msimamo wake ni ule ule. Kwamba niliwaambia na sasa niko magogoni? Ulimi wa binadamu hatari kubwa.
 
Wadau inasemekana Kikwete alitoa kauli hii kama sehemu ya hotuba yake kwa bunge:

"Hata hao ambao hawakuichagua CCM, serikali yao ni hii hii ambaye rais wao ni mimi... hata hao waliosusia, watakwenda; watarudi,"

Ukiangalia ni kauli iliyojaa vitisho kwa ambao hawakuchagua CCM na kwa wabunge wa CHADEMA. Anaonyesha ni jinsi alivyo mroho wa madaraka na kuonyesha kuwa yuko proud sasa kuwa yeye ni Rais na watu watake wasitake watamtii tu. Je hizi kauli si huwa zinatolewa na madikteta? Iko wapi kauli ya kuwa 'ushindi' wake ni ushindi wa wote??? Je huu ni mwanzo tu wa kuona true colors za huyu bwana?

Hata kwenye hotuba yake mbele ya aliowaita 'wazee wa dsm' wakati akiwatishia wafanyakazi wasigome, alitumia maneno yenye maana hiyo hiyo kwamba hata watumishi wagome vipi lazima watarejea mezani kwa mazungumzo eti majibu yapo serikalini na siyo kwingineko.

Hizo ni kauli za kiongozi mwenye majivuno na kiburi na ndiyo hulka za viongozi wa kiimla. Kwa chadema atacheza ngoma itamshinda asidhani hao ni watumishi wake anaowalipa mshahara.
 
Naomba:
1. Afute kesi zote za kisiasa za wabunge na viongozi wa CHADEMA kwa sababu hata CCM Arusha waliandamana bila kibali lakini hawakuchukuliwa hatua yoyote,
2. Asisaini Sheria ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya kwa kuwa ina kifungu cha kuzuia watu kutoa maoni kwa uhuru kinyume na Katiba,
3. Aruhusu maandamano yote ya amani badala ya kutoa taarifa feki za kiintelijensia za Polisi ili kuhalalisha kunyima watu uhuru wa kuelezea hisia zao,
4. Awachukulie wahalifu wote hatua za kisheria kuliko kuwaacha wengine "wapumzike" huku wengine wakikamatwa kila siku na kufunguliwa mashtaka,
5.....
Otherwise.....
 
mkuu L.justice1 kabla hujamlaumu JK ni Dikteta , naomba unipe definition ya Dikteta ...
 
Back
Top Bottom