Kwa kasi hii ya Magufuli, Upinzani unakuwa kama ndo unaanza!

Upinzani unatakiwa kuwepo na si kuua upinzani usaidia serikali kuwa macho muda wote kwa kuhofia kupoteza madaraka!
 
Kama sio upinzan sidhani kama kasi ingekuwepo . Tushukuru pia kwa kuwa na vyama vya upinzani
 
Ukiwa huna cha kupost kaa kimya. hii ni takataka.
Wale vijana hawashabikii ccm bali mtu mmoja yaani ni Magufuli na Majaliwa. Mbona mbeya wamefanya usafi na wala hawakushangilia hizo taka zako.
Sasa unakomenti katika takataka basi wewe ndo takataka!kaa kimya kama huna mchango!
 
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 UMOJA NI USHINDI

12. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa; ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

13. Sambamba na kupambana na tatizo la rushwa, Serikali pia zitatakiwa kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa umma.

Kwa haya mawili ya ILANI ya CCM wapinzani wafunge midomo ati Rais Magufuli anatekeleza ya upinzani. Kila Mtanzania awajibike ipasavyo mahala pake pa kazi kabla TINGATINGA alijampitia.

WATAISOMA NAMBA WAZEMBE NA MAFISADI
 
Kwa kasi hii ya Rais JPM inaweza ikaharibu upinzani katika hii nchi ni leo baada ya kushuhudia leo vijana kariakoo wakiwa wamepagawa!na Waziri mkuu,pia nilipokuwa Ferry vijana uvumilivu uliwashinda nakusema mafisadi watafute pakwenda!Na ujanja alioutumia JPM nikufanya yale wapinzani wamekuwa wakiyasema siku zote!Hivyo kuwa M4C kunaanza kudhoofisha upinzani hivyo kunatakiwa kuwepo na mbinu mbadala ya kushindana na hii kasi ya JPM. Leo wale vijana wa Kariakoo ni wale waliokuwa wakizomea mtu yeyote anayevaa nguo za CCM. Leo ndo wamekuwa washabiki wa CCM!

Nadhani hujui maana na jukumu la upinzani. Kajifunze tena. Kudhoofisha upinzani maana yake ni kuua demokrasia na hiyo ina madhara makubwa kwa Watanzania wote. Upinzani ni afya ya demokrasia maana tunajua upungufu wa mfumo wa chama kimoja. Hivyo, siyo kitu cha heri kuomba nguvu ya upinzani kudhoofika - maana yake serikali na chama tawala watafanya watakavyotaka na haki za watu zitaminywa ili kuziba mianya ya kukosoa au kugundua maovu yanayoendelea chini ya mfumo tawala. Acha kabisa!
 
Kwa haya mawili ya ILANI ya CCM wapinzani wafunge midomo ati Rais Magufuli anatekeleza ya upinzani. Kila Mtanzania awajibike ipasavyo mahala pake pa kazi kabla TINGATINGA alijampitia.

WATAISOMA NAMBA WAZEMBE NA MAFISADI

Lakini si haya wapinzani wamekuwa wakiyapigia kelele sana bungeni, lakini wamekuwa wakishindwa kwa vile kupitisha hoja kunafuata wingi wa kura na wabunge wengi wanatoka CCM. Unakumbuka wakati wa kupitisha Sheria ya Manunuzi ya Umma (ambayo Rais Magufuli mwenyewe amekiri ina mapungufu makubwa), wapinzani walikosoa vipengele kadhaa wakataka vibadilishwe wakakataliwa na sheria ikapita bila mchango wa kutosha kutoka upinzani. Leo sheria hiyohiyo inakosolewa na Rais. Je, upo hapo?
 
Nataka kuwaasa wapinzani kusoma alama za nyakati na kubadilika kulingana na siasa inavyobadilika.

BAADA YA MTEMI WAO KUUKOSA URAISI, WALIJIPANGA SANA KUPINGA NA KUDHOOFISHA UTAWALA WA RAIS MAGUFULI KAMA HASIRA YA KUANGUKA KWAO NDIYO MAANA KILA SIKU WANASUBIRIA BAYA LOLOTE LITOKEE ILI WAPATE HOJA YA KUITISHA MDAHALO LAKINI BADO SERIKALI INASONGA MBELE.

SASA IMEFIKIA MAHALI WANAPINGA NA MENGINE AMBAYO WALIKUWA WANAYATAKA WAO!

KUMBUKA KABLA YA DR. SLAA KUIKACHA CHADEMA, NA LOWASA KUPOKELEWA CDM, CHADEMA WALIKUWA WAMEMPANIA SANA LOWASA ENDAPO ANGEPITISHWA NA CCM. ILA KWAKUWA CCM HAWAKUMPITISHA LOWASSA IKAWA NDO MWANZO WA CDM KUSHINDWA MAANA HATA MUDA WA KU EDIT ZILE CD ZILIZOANDALIWA ZINAZOSEMA LOWASA NI FISADI, HAUKWEPO.

UPINZANI SOMENI ALAMA ZA NYAKATI, MLIYOTEGEMEA YATASHINDIKANA KWA RAISI MAGUFULI YAMEWEZEKANA SASA MNAPOTEZA MUDA KWA YALE MLIOJIANDAA NAYO NA WANANCHI WANAMKUBALI RAISI WAO.
 
Kwa hiyo tumerudi kwa one party state kama China na Cuba? Ngoja tunyoshe ma chuen lai yetu basi.
 
!!NAFKIRI KATIKA ORODHA DUNIANI YA MARAISI WAONGO NA WANASHINDWA KUPATA MBINU ZA KUWAONGOPEA WANANCHI MAGU NI NAMBA MOJA KIUFUPI NAMUAMBIA MAGU HANA ALICHOKIFANYA BALI NI MAIGIZO NA POROJO NYIIINGI TUNATAKA KUONA MABADILIKO HALISIA SIO MIPANGO YA SANAA!!
 
Kasi ya utendaji kazi wa rais wetu mpendwa imemduwa bwana Mbowe na kukubaliana kuwa upinzani haupo tena.

CCM shika hatamu turudishe heshima yetu iliyopotezwa na Mzee wa misafali.

Big up Magufuli aka burudoza.
 
Kasi ya utendaji kazi wa rais wetu mpendwa imemduwa bwana Mbowe na kukubaliana kuwa upinzani haupo tena.

CCM shika hatamu turudishe heshima yetu iliyopotezwa na Mzee wa misafali.

Big up Magufuli aka burudoza.
Naona zile mbegu za mmeo zimeacha kukuumiza umekuja kivingine toa poroja zako shughulika na mmeo tu siasa huziwezi
 
Back
Top Bottom